Karibu Arusha24tv kutazama kilicho Andikwa katika Magazeti ya leo November 25 ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24tv. Mwisho.
Author: Geofrey Stephen
Siha, Baraza la madiwani Halmshauri ya Siha mkoani Kilimanjaro limeomba mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira vijiji (RUWASA )Wilayani humo,wanapotekeleza miradi ya maji wahakikishe miundombinu ya mabomba inaingia kina kirefu ili miundombinu hiyo isiweze kuharibiwa wakati mitambo ya inayotengeneza barabara I siweza kufikia na kuharibi Maeneo hayo Haya yamejiri kwenye Baraza la kawaida la madiwani wa halmshauri hiyo lilifanyika katika ukumbi wa halmshauri hiyo na kuhudhuria na Wadau mbalibali wa maendeleao wakiwamo Viongozi wa Dini. Katika taarifa yake aliyoitoa katika Baraza hilo November 22 mwaka huu,Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Dancani Urasa,ametaka RUWASA kuzingatia utaratibu huo ili kuepuka gharama…
Na Mwandishi wa A24tv Arusha. Jumla ya wateja 100 wamefanikiwa kushinda kitita cha Shilingi milioni 10 kutoka kwa benki ya NMB kupitia droo yake ya pili ya kampeni ya Mastabata la kibabe lililochezeshwa jana katika tawi la Clock tower jijini Arusha. Washindi hao wamejinyakulia Kila mmoja Shilingi 100,000 katika Kampeni hii ya Mastabata la kibabe inayoendeshwa na benki ya NMB kwa wiki 12, kwa lengo la kuhamasisha matumizi ya fedha kidigitali. Akizungumza wakati wa kuzindua kampeni hiyo mikoa ya kanda ya Kaskazini, Meneja mwandamizi wa NMB kitengo cha kadi Manfredy Kayala amesema lengo ni kuunga mkono jitihada za serikali katika…
Na Mwandishi Wetu, Arusha Wanawake Jamii za Asili Nchini wanakutana jiji Arusha kujadili changamoto zao ikiwepo athari za mabadiliko ya Tabianchi. Wanawake hao kutoka jamii za wahadzabe, Wamasai, wabarbaigi,wadatoga na waakei wanasema mabadiliko ya tabia nchi yameleta ukame katika maeneo mengi ya jamii hizo na hivyo kuathiri maisha yao. Akifungua Kongamano la siku mbili la wanawake wa jamii za Asili, Mkurugenzi wa shirika la utafiti na maendeleo ya jamii (CORDS) Lilian Looloitai amesema kuwa wanawake wa jamii za Asili wanakabiliwa na athari za mabadiliko ya Tabianchi yaliyopelekea kuwepo na vikwazo vya kiuchumi na kijamii. Amesema mabadiliko ya Tabianchi yameathiri maisha…
Karibu Arusha 24Tv kutazama Habari kubwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania leo November 23 mwaka 2024 mbele na nyuma Hii ni A24tv . Mwisho .
Na Mwandishi wa A24tv. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda Novemba 21, 2024 amepongeza shirika la Mapadre la kazi ya Roho Mtakatifu(ALCP/OSS) kwa kuchangia katika huduma za kijamii ikiwemo elimu nchini. Amesema hayo katika halfa ya Jubilei ya miaka 50 tangu kuanzishwa kwa shirika hilo mwaka 1974 iliyofanyika katika makao makuu ya shirika Sabuko Sanya juu, Wilaya ya Siha Mkoani Kilimanjaro Mkenda ametoa pongezi hizo kwa niaba ya serikali kwa kazi kubwa ambayo shirika linafanya nchini za kijamii na kuomba kanisa hilo liendelee kuliombea taifa kudumisha amani, umoja, mshikamano . Amesema serikali ya awamu ya sita…
Na Bahati Siha . Wakazi wa Siha wa mkoani Kilimanjaro wametakiwa kuuchukulia uchaguzi wa serikali za mitaa kwa ukubwa wake na kuutendea haki kwa kuchagua viongozi watakaokuwa kiungo na sehemu ya suluhisho la changamoto zinazowakabili. Haya yamesemwa Tumsifu Kweka mjumbe wa mkutano mkuu wa Taifa pia mjumbe mkutano mkuu wa mkoa,wakati wa uzinduzi wa kampeni za uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya SanyaJuu Wilayani humo , Kweka amesema uchaguzi huo ni muhimu na ni lazima ufanyike kwani viongozi watakaopatikana ni kiungo muhimu pia watakuwa na majukumu makubwa ya kujua hali na maisha ya wananchi…
Na Mwandishi wa A24tv. Baraza la Vyuo Vikuu vya Jumuiya ya Afrika Mashariki (IUCEA) limekutana na Wadau pamoja na Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania ili kutoa mafunzo mbalimbali ambayo yatahusika katika ufungamanishaji wa elimu ya juu katika ukanda huo na kuwaeleza wadau juu ya fursa mbalimbali katika jumuiya hiyo. Akizungumza Novemba 20, 2024 Jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema katika jumuiya ya Afrika Mashariki wamekubaliana kwa pamoja kufungamanishwa Elimu ya juu ili kuondoa tofauti kwa elimu inayotolewa katika ukanda huo. Aidha Prof. Nombo amesema makubaliano ya hatua hiyo yatafungua fursa…
Karibu Arusga24tv kutazama habari kubwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania Novrmber 22 mwaka 2024 mbele na Nyumba Hii ni A24tv. Mwisho .
Na Richard Mrusha Dar es laam. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa ameipongeza Wizara ya Madini kwa juhudi mbalimbali inazofanya za kuiendeleza Sekta ya Madini kufikia asilimia 9.0 katika kuchangia kwenye Pato la Taifa huku sekta ikikua kwa asilimia 11.3. Ameyasema hayo, leo Novemba 19, 2023 wakati wakufungua Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2024 unaendelea katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es salaam. Waziri Mkuu Majaliwa amesema kuwa uwepo wa Sera nzuri zenye ushawishi mazingira salama yenye utulivu na amani uwepo wa masoko ya uhakika yaliyounganishwa na…