Author: Geofrey Stephen

Na Bahati Siha Siha ,Serikali imetoa mita 20 za majaribio za kulipia kabla kwa Bodi ya maji Lawate Fuka Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro Mita hizo zimetolewa kwa lengo la kuongeza kipato kwa Taasisi na pia kupunguza malalamiko kwa wateja ambao bao udai ya kubambikiwa bili za maji. Meneja wa bodi hiyo Elihuruma Masawe Akizungumza na waandishi wa habari walipofika kwake,Amesema umuhimi wa kuwepo kwa mita hizo wakati wake umefika ili kuepukana na malalamiko kwa wateja wa kudai kubambikiwa bili za maji “Ni kweli kupunguza malalamiko kwa wateja wetu kudai kubambikiwa bili za maji tumeona kufunga mita hizi za kulipia…

Read More

Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe.Angellah Kairuki, Amefungua Maonyesho ya Sita ya kili fair jijini Arusha akiwa ameambatana na  Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhe. Mudrick Ramadhan Soraga. Pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christin Makonda kutembelea mabanda kwenye Maonesho ya Kimataifa ya Utalii ya Karibu- Kili Fair 2024 yanayofanyika kwenye viwanja vya Magereza Kisongo leo Juni 07, 2024. Awali Waziri Kairuki amezindua maonesho hayo msimu wa tisa wa maonesho yalishirikisha zaidi ya makampuni 400 ya utalii kutoka ndani na nje ya Tanzania, yakiwa na lengo la kuhamasisha Utalii Tanzania. Karibu…

Read More

Na Geofrey Stephen  ARUSHA  Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI(AFYA)Dkt Wilson Mahera amesema serikali ipo mbioni kuajiri watumishi wapya wa sekta hiyo ikiwa ni mpango mahususi wa kuboresha sekta ya afya nchini ili kuondoa tatizo la upungufu wa watumishi hususani wahudumu  ngazi ya jamii . Dkt Mahera amebainisha hayo jijini Arusha, wakati akifungua mafunzo ya siku tano yanayofanyika katika Chuo cha Afya CEDHA ,kwa Timu ya uendeshaji huduma ya Afya kutoka Mkoa wa Tanga (RHMT),waratibu wa Afya mama na Mtoto Ngazi ya Halmashauri (CHMT) na wataalamu wa TEHAMA wa Halmashauri zote mkoa huo.  Mafunzo hayo yamefadhiliwa na shirika la Maendeleo la Ujerumani…

Read More

Mbunge wa Hai (CCM), Saashisha Mafuwe amesema Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mambo mengi jambo ambalo wanauhakika katika chaguzi zijazo watafanya vizuri. Haya ameyasema wakati wa ziara Katibu Mkuu wa Chamacha Mapinduzi (CCM)Dk Emanuel Nchimbi Wilayani Hai katika muendeleze wa ziara yake kufuatilia utekelezaji wa ilani,kusikiliz kero za Wananchi na kuangaza maandalizi ya chaguzi zijazo. Mafuwe amesema katika Jimbo hilo ambalo kwa miaka mingi limekuwa likiongozwa na upinzani amedai haikupata maendeleo. Miongoni mwa wabunge walioongoza ni Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chadema. “Tulikuwa na watu hapa miaka 25 hatukuona walichokifanya, leo maendeleo ambayo tumayafanya ni…

Read More

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Mnamo Juni 05, 2024 saa 7:20 mchana huko katika eneo la Mbembela, Kata ya lyunga Jijini Mbeya katika barabara kuu ya Mbeya Tunduma, Gari namba T.979 CVV na likiwa na Tela namba T.758 BEU Scania ikiendeshwa na Dereva aliyefahamika kwa jina la Ross Mwaikambo [40] likitokea Shamwengo likiwa limepakia kokoto, aligongana na Gari namba T.167 DLF Toyota Coaster iliyokuwa ikiendeshwa na dereva asiyefahamika kisha kugongana na Gari namba T.120 DER Toyota Harrier iliyokuwa ikiendeshwa na Dokta.Robert Francis Mtungi [48] Mkazi wa Isyesye Aidha, Lori hilo liliendelea kugonga Guta namba MC 660 BCR iliyokuwa ikiendeshwa na…

Read More

Na Geofrey Stephen . Ikiwa leo tarehe 05.06.2024 ni maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambapo Kitaifa yamefanyika Jijini Dodoma, Taasisi ya Utafiti wa Wanyamapori Tanzania (TAWIRI) imebainisha mchango mkubwa wa wadudu mbalimbali akiwemo nyuki katika Mazingira. Akitoa elimu ya wadudu kwa wanafunzi wa Shule ya Msingi NALOPA waliotembelea Makao Makuu ya TAWIRI Mtafiti Alphoncinah Mponzi amesema, wadudu wana mchamgo mkubwa katika mazingira ambapo wanasaidia uchavushaji wa mimea kwa zaidi ya asilimia 80%. “Nyuki ni mchavushaji mkuu wa kuendeleza uwepo wa mimea mbalimbali katika uhifadhi” ameeleza Mtafiti Mponzi Aidha, Mtafiti Mponzi amesema mbali na uchavushaji wadudu wanasaidia uozeshaji wa…

Read More