Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24tv kilimanjaro . Ofisi ya Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za kulevya (DCEA) Kanda ya Kaskazini imeshiriki Kikao cha Mwaka cha Maafisa Ustawi wa Jamii kuanzia tarehe 18 hadi 20 Septemba 2024 kilichofanyika Ukumbi wa CCP Moshi mkoani Kilimanjaro. Lengo la Kikao hiko ni kuwakutanisha Maafisa Ustawi wote nchini kujadili afua mbalimbali za kuwasaidia watu waliopo kwenye Makundi Maalum kamavile kundi la waraibu wa dawa za kulevya. Kauli mbiu ya mwaka huu ni _”Tanzania bila Ukatili Inawezekana, Imarisha Mahusiano Chanya ya Familia”_. Kikao kilifunguliwa na Naibu wa Waziri wa Fedha Mh Hamad Chande…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv .Arusha Benki ya NMB imefanikiwa kukabidhi udhamini wa vifaa vya michezo kwa ajili ya wachezaji 150 wanaotarajia kushiriki mashindano ya kimataifa ya Diplomatic Golf 2024. Michuano hiyo inayotarajia kuanza kutimua vumbi kwa siku mbili kuanzia Septemba 21-22, 2024 katika viwanja vya Kili Golf vilivyoko Mkoani Arusha yana lengo la kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia watoto wanaotoka katika mazingira magumu. Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Songea Mississippi (SOMI) na klabu mwenyeji ya Kili Golf, jumla ya mashimo 36 yataamua mshindi kutoka kwa washiriki wote 150 kutoka nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki pamoja na wachezaji…

Read More

JESHI LA POLISI NCHINI LIMEMPONGEZA KWA NA KUTAMBUA KAZI YAKE NZURI YENYE UMAIRI MKUBWA BAADA YA KUSOGEZA BUS LILO PARK VIBAYA JIJINI ARUSHA . AKIONGEA NA VYOMBO VYA HABARI DCP RAMADHANI NG’ ANZI AMESEMA KWAMBA Askari Polisi wa Kike aliendesha Basi WP Koplo Sheila nimempongeza kwa Niaba ya IGP kwa kuliletea sifa nzuri Jeshi la Polisi wakati akitekeleza majukumu yake ya Usalama Barabarani. WAKATI HUO HUO AKIWA JIJINI ARUSHA KAMANDA NG’ ANZI AMEENDESHA OPERESHENI KABAMBE YA UKAGUZI WA MAGARI MABOVU .  Arusha. Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Nchini Naibu Kamishna wa Polisi DCP Ramadhan Ng’anzi amefika Jijini Arusha na…

Read More

Na Geofrey Stephen Tanga . Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Mhandisi Juma Hamsini, akiwa na Menejimenti ya Halmashauri (CMT), leo Jumatano Septemba 18, 2024, amefanya kikao kazi na Watendaji wa Kata, Waganga Wafawidhi, Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu, chenye lengo la kufahamiana, kuweka mikakati ya pamoja, na kutatua changamoto za kiutendaji. Katika kikao hicho, Mhandisi Hamsini amewataka viongozi hao kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati, na kwa kuzingatiwa kwa ubora, ili jamii inufaike na mipango ya Serikali ya kuwasogezea huduma kwa karibu. Aidha amehimiza uwajibikaji kwa watumishi, na utoaji wa huduma iliyo bora kwa jamii. Mwisho .

Read More

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewaagiza  wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha  wanasimamia zoezi la ubainishaji wa watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kupata fursa ya elimu. Akifungua maadhimisho ya miaka 30 ya elimu jumuishi  Patandi Jijini Arusha Mhe. Mchengerwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama kufuatlia wazazi wanaowaficha watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kupata elimu kama stahiki ya mtoto wa Kitanzania. “Nawaelekeza Viongozi wote wa Mikoa na Halmashauri nchini kusimamia zoezi la ubainishaji na utambuzi wa awali wa watoto kwa wakati ili kubaini wenye mahitaji maalumu,…

Read More

Na Mosses Mashala . Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ina kila sababu ya kuanzisha mfumo wezeshi kwenye biashara zinazochipukia zenye uwezo wa kukua kwa haraka ili kustawisha maisha ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipofungua mkutano wa tatu wa pamoja wa taasisi ya Utafiti na Uchambuzi wa Sera za Kijamii na Uchumi Zanzibar, (ZRCP) leo tarehe 17 Septemba, 2024 kwenye ukumbi wa hoteli ya Madinat Al Bahar Mkoa wa Mjini Magharibi. Aidha Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Zanzibar ina wajasiriamali vijana wenye vipaji wanaochipukia…

Read More

Jumuhiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Wilayani ya Siha mkoani Kilimanjaro,wachagua wajumbe kata ya Ormelili na Songu Jumuhiya ya maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro,imewatambulisha wajumbe wa kamati hiyo kwa Viongozi wa kata ya Ormelili na Songu Wilayani humo na kupewa majukumu. wanayotakiwa kusimamia ikiwa ni pamoja kutunza amani na kuibua maovu kwenye jamii viongozi wa kata hizo wakisema kwamba wajumbe hao wamekuja wakati muafaka na kwamba itasaidia kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya unyanyasaji kijinsia ikiwamo ubakaji na ulawiti na mimba kwa wanafunzi Mbali na hilo pia itasaidia kuwadhibiti wauza madawa ya kulevya ikiwamo…

Read More