Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv . Kwa ufupi SMAUJATA mkoani Kilimanjaro weweka mkakati wa mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili ikiwamo ubakaji na ulawiti vinavyozidi kuongeza Moshi,Viongozi wa Taasisi huru ya Shujaa wa maendeleao na Ustawi wa jamii Tanzanian (SMAUJATA) mkoani Kilimanjaro wameweka mkakati wa kuendelea na mapambana dhidi ya vitendo vya ukatili ikiwa ni pamoja na ulawiti na ubakaji ambavyo vimekuwa vikiongezaka kwa kutoa elimu sehemu mbali mbali ikiwamo shuleni ,vyuoni ,sokoni na pia kuanzisha vilabu mashuleni vya kupinga ukatili huo. Haya yamejiri katika kikao cha mpango kazi 2024 na 2025 ya kujiwekea mpango mkakati kwa ajili ya kuendelea…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Tanzania na Kenya zimekubaliana kuendelea kutatua vikwazo vya kibiashara visivyo vya kiushuru kwa kuwa na Mpango wa pamoja wa kuwianisha tozo, ada , ushuru, ada na sheria au taratibu zinazoathiri biasharabaina ya pande hizi mbilmasharti mengine yanayoathiri biashara pamoja na kuwezesha ufanyaji biashara mpakani kwa saa 24 ili kukuza biashara baina ya nchi hizo kila siku, kila mwezi na kila mwaka. Aidha, amebainisha kuwa Nchi hizo zimekubaliana kuhakikisha kuwa .Sheria za Tanzania  hazizuii wafanyabiashara wa Kenya kufanya biashara Tanzania na Sheria za Kenya hazizuii wafanyabiashara wa Tanzania kufanya biashara nchini Kenya. Naibu Waziri wa Mambo…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv. _Kunufaisha zaidi ya wachimbaji 5000 -Wamshukuru Rais Samia kwa kuwaendeleza wachimbaji wadogo _Waziri Mavunde awataka wachimbaji kuongeza uzalishaji baada ya kupata Leseni _Kwasasa wazalisha madini yenye thamani ya Bilioni 101 kwa miezi nane(8) Serikali ya Awamu Sita, chini ya uongozi wa *Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan* imetekeleza ombi la siku nyingi la Wachimbaji w Wadogo Wilayani Songwe kwa kuwatengea eneo la uchimbaji na kuwakabidhi jumla ya Leseni ndogo *37* zilizopo eneo la Kata ya Saza kutoka Leseni hodhi namba *RL0009/2014* ya iliyokuwa Kampuni ya Bafex Tanzania Limited. Hayo yameelezwa leo Machi 23, 2024 na Waziri wa…

Read More

Na Mosses Mashala . Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ubora wa Quran ni muhimu katika maisha ya duniani na akhera. Amesisitiza umuhimu wa Wazazi na Walezi kuhamasisha watoto na vijana kutekeleza mafundisho ya Quran kwa kuisoma na kuhifadhi. Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika fainali za Mashindano ya 20 ya Kimataifa ya Quran Tajweed yaliyoandaliwa na Taasisi ya Khidmatulquran Islamic kwa kushirikisha nchi mbalimbali zikiwemo Msumbiji, Indonesia, Uturuki, Pakistan, Bangladesh, Misri, Comoro, Morocco, Afrika Kusini, Iran na Tanzania ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam tarehe 23 Machi…

Read More

Na Lilian Kasenene,Same MAKAMU wa Rais Dk Philip Mpango ameziagiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanaendelea kuhifadhi maeneo mapya ya hifadhi za misitu pamoja na kuongeza mashamba ya miti. Pia amewataka wakala wa huduma za Misitu nchini TFS kuhakikisha kila Halmashauri inakuwa na vitalu vya miti kuanzia ngazi za vijiji hadi kata ambapo Halmashauri za miji zitengeneza bustani za kijani kwaajili ya kupumzikia na mazoezi. Makamu wa Rais huyo alisema hayo wilayani Same mkoani Kilimanjaro wakati wa maadhimisho ya siku ya misitu duniani na siku ya upandaji miti kitaifa yaliofanyika wilayani humo yenye kauli mbiu ‘Misitu na Ubunifu’. ” Vijiji vyote…

Read More

BRYSON MSHANA, RUANGWA Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa leo Machi 22, 2024 amaezindua ripoti ya Mpango wa Matumizi ya Ardhi ya Vijiji Wilaya ya Ruangwa mkoni Lindi na kutoa vyeti 18 vya ardhi ya kijiji. Waziri Mkuu amefanya uzinduzi huo katika Mkutano wa wadau wa kujadili utekelezaji mradi wa uboreshaji usalama wa milki za ardhi, uliohusisha wadau wa masuala ya ardhi kutoka maeneo mbalimbali ya wilayani Ruangwa. Waziri Mkuu amesema kuwa lengo la Serikali ni kupima ardhi yote nchini ili wananchi wakiwemo wanavijiji ili waweze kuitumia ardhi hiyo kufanya shughuli zao za kiuchumi. Aidha, Wakuu…

Read More

Na Mosses Mashala. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema familia ya Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi imepata faraja kubwa kutokana na Dua Maalum zilizofanywa Bara, Visiwani na nje ya nchi katika Misikiti mbalimbali kwa ajili ya kumuombea Hayati Mzee Mwinyi. Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa na Dua Maalum ya kumwombea Hayati Alhajj Mzee Ali Hassan Mwinyi Misikiti wa Al Jumaa Masjid Kitumbini Dar es Salaam tarehe: 22 Machi 2024. Aidha Rais Dk.Mwinyi ameushukuru uongozi wa Msikiti wa Al Jumaa Kitumbini…

Read More

Na Mosses Mashala . Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar na kuwasili Jijini Dar es Salaam tarehe 22 Machi 2024. Rais Dk.Mwinyi atashiriki Mashindano ya Tajweed ukumbi wa JNICC na Mashindano ya Kimataifa ya kuhifadhi Quran yatakayofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa yaliyoandandaliwa na Taasisi ya Al Hikma.Foundation Mwisho 

Read More

Kwa ufupi: Waliokuwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji katika halmashauri ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro katika kipindi cha mwaka 2009 hadi 2019 wametoa siku 30 kwa halmashauri hiyo kuhakikisha wanalipa madeni ya posho zaidi ya Sh 200milioni wanazodai. Hai.Waliokuwa wenyeviti wa vijiji na vitongoji katika halmashauri ya Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro katika kipindi cha mwaka 2009 hadi 2019 wametoa siku 30 kwa halmashauri hiyo kuhakikisha wanalipa madeni ya posho zaidi ya Sh 200milioni wanazodai. Wenyeviti hao ambapo ni zaidi ya 350 wanadai kutolipwa posho zao tangu mwaka 2010 hadi 2019 licha ya kupelekea malalamiko yao kwa maandishi katika…

Read More