Na Geofrey Stephen Tanga . Mkurugenzi wa Jiji la Tanga, Mhandisi Juma Hamsini, akiwa na Menejimenti ya Halmashauri (CMT), leo Jumatano Septemba 18, 2024, amefanya kikao kazi na Watendaji wa Kata, Waganga Wafawidhi, Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu, chenye lengo la kufahamiana, kuweka mikakati ya pamoja, na kutatua changamoto za kiutendaji. Katika kikao hicho, Mhandisi Hamsini amewataka viongozi hao kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati, na kwa kuzingatiwa kwa ubora, ili jamii inufaike na mipango ya Serikali ya kuwasogezea huduma kwa karibu. Aidha amehimiza uwajibikaji kwa watumishi, na utoaji wa huduma iliyo bora kwa jamii. Mwisho .
Author: Geofrey Stephen
WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mohamed Mchengerwa amewaagiza wakuu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha wanasimamia zoezi la ubainishaji wa watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kupata fursa ya elimu. Akifungua maadhimisho ya miaka 30 ya elimu jumuishi Patandi Jijini Arusha Mhe. Mchengerwa amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya kupitia Kamati za Ulinzi na Usalama kufuatlia wazazi wanaowaficha watoto wenye mahitaji maalum ili waweze kupata elimu kama stahiki ya mtoto wa Kitanzania. “Nawaelekeza Viongozi wote wa Mikoa na Halmashauri nchini kusimamia zoezi la ubainishaji na utambuzi wa awali wa watoto kwa wakati ili kubaini wenye mahitaji maalumu,…
Karibu Arusha24tv leo September 18 kutazama kilicho Andikwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24tv . Mwisho .
Na Mosses Mashala . Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema Zanzibar ina kila sababu ya kuanzisha mfumo wezeshi kwenye biashara zinazochipukia zenye uwezo wa kukua kwa haraka ili kustawisha maisha ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipofungua mkutano wa tatu wa pamoja wa taasisi ya Utafiti na Uchambuzi wa Sera za Kijamii na Uchumi Zanzibar, (ZRCP) leo tarehe 17 Septemba, 2024 kwenye ukumbi wa hoteli ya Madinat Al Bahar Mkoa wa Mjini Magharibi. Aidha Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Zanzibar ina wajasiriamali vijana wenye vipaji wanaochipukia…
Jumuhiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Wilayani ya Siha mkoani Kilimanjaro,wachagua wajumbe kata ya Ormelili na Songu Jumuhiya ya maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro,imewatambulisha wajumbe wa kamati hiyo kwa Viongozi wa kata ya Ormelili na Songu Wilayani humo na kupewa majukumu. wanayotakiwa kusimamia ikiwa ni pamoja kutunza amani na kuibua maovu kwenye jamii viongozi wa kata hizo wakisema kwamba wajumbe hao wamekuja wakati muafaka na kwamba itasaidia kuongeza nguvu ya mapambano dhidi ya unyanyasaji kijinsia ikiwamo ubakaji na ulawiti na mimba kwa wanafunzi Mbali na hilo pia itasaidia kuwadhibiti wauza madawa ya kulevya ikiwamo…
Karibu Arusha24tv leo September 17 kutazama kilicho Andikwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24tv. Mwisho .
Na Geofrey Stephen Arusha . Waziri wa nchi Ofisi ya Rais, Tawala za mikoa na serikali za Mitaa TAMISEMI, Mhe. Mohamed Mchengerwa ametangaza kuwa jumla ya Vijiji 12, 333, mitaa 4,269 na Vitongoji 64, 274 vitashiriki uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27, 2024. Akizungumza Jijini Arusha mapema leo Jumatatu Septemba 16, 2024 kwenye Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Waziri Mchengerwa amewaambia wanahabari kuwa kwenye orodha hiyo kumejumuishwa maeneo yaliyokuwa yamefutwa awali kwa mujibu wa tangazo la serikali ambayo pia yalihusisha Tarafa ya Ngorongoro mkoani Arusha. “Matangazo haya yanajumuisha maeneo yaliyokuwa…
Na Geofrey Stephen Arusha . Asasi zisizo za kiraia nchini zimetakiwa kuangalia namna ambavyo wataweza kujitegemea katika kuendesha shughuli mbalimbali za kijamii sambamba na kuendelea kujenga uelewa wa kutosha katika kuchochea uboreshaji katika shughuli za kijamii. Hayo yamesemwa mkoani Arusha na Mwenyekiti wa bodi ya AZAKI ,Mercy Silla wakati akifunga wiki ya AZAKI iliyokuwa ikiendelea kwa muda wa wiki moja mkoani Arusha. Silla amesema kuwa, kukutanisha asasi hizo wiki nzima wameweza kujadili maswali mbalimbali ya kuboresha katika utendaji kazi sambamba na kujifunza zaidi kutoka kwa wenzao wa nje ya nchi. Amefafanua kuwa,ni wajibu wao kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele ili…
Karibu Arusha24tv kutazama kilicho Andikwa katika Magazeti ya leo September 14 ya Tanzania mbele na nyuma. Hii ni A24tv . ⁶ Mwisho .
Na Mosses Mashala. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendeleza juhudi za kuimarisha Michezo kwa lengo la kuinua vipaji vya vijana. Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo tarehe 14 Sept 2024 katika Uwanja wa Gombani Mkoa wa Kusini Pemba baada ya kushuhudia Fainali ya Michuano ya Yamle Yamle kati ya timu ya Ponchinki City na Wete City. Aidha Rais Dk.Mwinyi amelitaka Shirika la Utangazaji Zanzibar ZBC kuendelea kuimarisha Michuano hiyo ambayo sasa imekuwa na sura ya kitaifa na kuunga Mkono kila Mwaka. Katika Mchezo huo wa Fainali timu ya Ponchink City imeibuka na…