Author: Geofrey Stephen

Na Mosses Mashala Zanzibar . RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewashukuru Jumuiya ya Zawiyatu Qadiria Tanzania kwa kumuombea Dua Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi. Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa Msikiti wa Masjid Ngamia Welezo Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 15 Machi 2024. Aidha Rais Dk.Mwinyi amehimiza umuhimu wa kuendelea kuiombea Dua Nchi na kudumisha amani na utulivu.

Read More

Na Mosses Mashala . Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole Ikulu Zanzibar kutoka kwa Mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Hafidh Ameir kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi, Mwenyekiti wa CCM Taifa Mstaafu, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe: 29 Februari 2024, Dar es Salaam na kuzikwa tarehe: 02 Machi 2024, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja . Mwisho .

Read More

Mwandishi wetu,Arusha. Wakulima zaidi ya 300 kutoka mikoa ya Geita Iringa Mbeya Morogoro Mwanza Shinyanga na Tabora wametakiwa kuacha tabia ya kununua mbegu minadani badala yake wanunue katika mawakala waliosajiliwa. Akizungumza katika mafunzo ya wakulima yaliyotolewa na wataalamu wa sayansi ya mimea wa kampuni ya Balton Tanzania inayoingiza na kusambaza mbegu nchini Tanzania Afisa Mfawidhi wa taasisi ya Kuthibiti Ubora wambegu Tanzania, Kanda ya Kaskazini, Dk Munguatosha Ngumuo alisema ni muhimu kununua mbegu zilizothibitishwa. Dk Ngomuo alisema wakulima wanapaswa kuacha kilimo cha mazoea badala yake wajifunze kulima kisasa kwa kutumia mbegu bora ambazo zimethibitishwa. Mkurugenzi Mtendaji wa Balton Tanzania Chris…

Read More

Na Lilian Kasenene,Morogoro Shirika la Uhifadhi Tanzania(TANAPA) kwa kushirkiana na Mamlaka ya usafiri wa anga nchini(TCAA) na mashirika 14 ya ndege wameanza kuchukua hatua za kuimarisha zaidi usalama na usafiri wa anga ndani ya hifadhi za taifa baada ya idadi ya watalii kuongezeka kutumia usafiri huo ili kuzifikia hifadhi mbalimbali kwa shughuli za utalii. Afisa uhifadhi mkuu anayesimamia viwanja vya ndege kutoka Tanapa Chritine Bgoya amesema hayo katika kiwanja cha ndege cha Kikoboga kilichopo kwenye hifadhi ya taifa ya Mikumi wilayani Kilosa Mkoani Morogoro wakati akizungumza na waandishi wa habari, ambapo washiriki 19 walihudhuria Bgoya amesema wote kwa pamoja wamekutana…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv .Arusha Mbunge wa Jimbo la Monduli Fredrick Lowassa amewasihi na kuwaomba watendaji wa Serikali Wilayani humo kusimamia Mradi wa Maji Unaotarajiwa kuanza hivi karibuni itakayogharimu billioni 20.3 ,wa Vijiji 13. Hayo yanajiri baada ya Kampuni ya JANDU PLUMBER ya Jiji la Arusha kufika Jimboni hapo kwa Lengo la kujitambulisha kwa Viongozi wa Chama na Serikali Rasmi Mradi huo kuanza Mradi huo unafuatia Ahadi za Mbunge huyo kwenye Uchaguzi mkuu 2020, Ambapo Hayati Rais John Pombe Magufuli alilipokea ikiwa ni hitaji la Mbunge huyo ,Ambapo miaka miwili baadaye Rais wa Awamu wa sita Dkt Samia Suluhu Hassan…

Read More

Na Geofrey Stephen Dar . Jaji Mahakama kuu divisheni ya Ardhi jaji Hemedi ametoa onyo kali na kutishia hati ya kuwakamata washtakiwa wawili ambao ni Joanita Kazinja pamoja na Hadija Kalulu kwa kosa la kudharau amri ya mahakama. Hatua hiyo imekuja baada ya washtakiwa kutokufika mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi yao msingi ya kubadilisha hati kinyune na utaratibu kwa Mfanyabiashara maarufu Matunda Hata hivyo wakili wa Kamishna wa ardhi Dar es Salaama kupitia kwa wakili wake aliomba huruma yake mahakama kupitia jaji kwamba atawaleta tarehe itakayopangwa Pamoja na hayo kamishna anadaiwa kuendelea kukiuka na kuzuia (SEARCH) ya kujua nani…

Read More

NA; MWANDISHI WETU – DODOMA Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulika na masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Mhe. Jenista Mhagama amekabidhi vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni Mbili za kitanzania kwa watekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Kilimo na Uvuvi (AFDP) Mapema leo tarehe 12 Machi, 2024 katika viwanja vya Ofisi hizo zilizopo Mtumba Jijini Dodoma. Akikabidhi vifaa hivyo ambavyo ni Magari, pikipikiza miguu miwili na mitatu (guta) kwa wawakilishi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Wizara ya Kilimo, Wakala wa Mbegu (ASA), Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI) na Taasisi za Udhibiti wa Ubora…

Read More