Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24tv. Waziri wa Viwanda na Biashara,Mhe Dkt. Ashatu Kijaji amesema Serikali inaendelea na mchakato wa kuandaa mfumo mmoja wa ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara nchini ili kuondoa kero ya taasisi mbalimbali za Serikali kukusanya kodi. Alitoa kauli hiyo Mei 10, 2024 jijini Mbeya wakati wa Mkutano wa Majadiliano kati ya Sekta umma na Sekta binafsi uliokuwa na lengo la kujadiliana namna ya kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyabiashara katika Mkoa huo Aidha. Dkt. Kijaji alisema kero hiyo imekuwa ikilalamikiwa kwa muda mrefu na wafanyabiashara pamoja na wadau mbalimbali kuwa ilikuwa ikichangia kuua biashara na kufukuza wajasiriamali. “Kilio hiki…

Read More

Na Mosses Mashala . Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itaendelea kushirikiana na Kanisa la Kianglikana na Taasisi nyingine za dini kwa kudumisha amani na utulivu . Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Kiongozi wa Kanisa la Kianglikana Duniani , Askofu Mkuu Justin Welby na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar tarehe 11 Mei 2024. Rais Dk.Mwinyi amemshukuru Askofu Justin Welby kwa ujio wake Zanzibar. Naye Askofu Justin Welby amempa pole Rais Dk.Mwinyi kutokana na kifo cha Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi Vilevile ujumbe…

Read More

Doreen Aloyce, Zanzibar Shangwe na Ndelemo vimetawala mara baada ya Maaskofu na waumini wa Dayosisi ya Zanzibar, kumpokea Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby alipowasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa Zanzibar. Akiongoza jopo la Maaskofu na waumini wa waliotoka ndani na nje ya Dayosisi Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Tanzania Maimbo Mndolwa amesema ujio wake ni wa faraja kubwa na furaha kwa wakristo kote nchini. Aidha Askofu Mkuu wa Canterbury Justin Welby amewasili nchini Tanzania kupitia Dayosisi ya Zanzibar, kwa lengo la kutembelea na kuona maeneo ya kihistoria mahali lilipo Kanisa Kuu la Kristo Mkunazini Unguja yaliyotumika kufanya biashara…

Read More

Na MossesMashala . Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaomba Waumini wa Dini ya Kiislamu kuendelea kuwaombea Dua Viongozi ili watimize majukumu yao na kutekeleza ahadi walizoahidi. Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika sala ya Ijumaa Msikiti wa Qubaa Mbweni Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe 10 Mei 2024. Pia Rais Dk.Mwinyi amewatembelea Wazee akiwemo Mbunge wa zamani Jimbo la Amani , Mzee Hassan Rajab nyumbani kwake Kisauni na Mjumbe wa Baraza la Wazee CCM Kisiwandui, Bi Maryam Hengwa nyumbani kwake kwa Mchina Mkoa wa Mjini Magharibi.

Read More

Na Mwandishi wetu,Katavi Watalii wa ndani na nje ya nchi wameombwa kutembelea hifadhi ya Taifa ya Katavi ili kujionea vivutio lukuli vya Utalii . Hifadhi hiyo pia imewaalika wawekezaji wa ndani na nje kwenda kuwekeza katika hifadhi hiyo ambayo inafursa nzuri za uwekezaji wenye kuleta faida. Mhifadhi Mwandamizi wa hifadhi hiyo, ,Manendo Maziku akizungumza na waandishi wa habari juu ya hali ya utalii katika hifadhi hiyo alisema kuna vivutio vingi ila bado watalii hawajaviona. Maziku alisema mtu atakapo tembelea hifadhi hiyo atapata fursa ya kupumzika na kujifunza mambo mbalimbali ambapo katika hifadhi nyingine hayapo. ”Mfano unapoingia katika lango la hifadhi…

Read More

Siha, Halmshauri ya Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro imepewa kongole kwa kufanya vizuri katika ukusanyaji mapato ya ndani ambapo kwa sasa imefikia asilimia 93 Mbali na hilo pia ripoti ya Mdhibiti na Mkuguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG), inaonyesha kwamba halmshauri siha imepata hati safi. Muwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Gasper Ijiko Akizungumza kwenye kikao cha kawaida Baraza la hilo kilichofanyika katika ukumbi wa halmshauri hiyo,Amesema Siha ni miongoni mwa Wilaya inayo upa Mkoa nafasi nzuri kwenye ukusanyaji wa mapato. “Nipongeze Halmashauri kwa ukusanyaji mzuri wa mapato,kama ambavyo mnafahamu tumepewa mkakati na maelekezo ya ukusanyaji…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Kliniki ya Malalamiko iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,Paulo Makonda, imeanza kuzaa matunda kufuatia mjane Maryam Yahya Husein Mkazi wa jijini Dar es salaam aliyedai kudhulumiwa mali za Marehemu mumewe, kupatiwa ufumbuzi. Maryamu alileta malalamiko yake mbele ya Mawakili kutoka chama cha Mawakili Tanganyika TLS, wanaosikiliza kero mbalimbali za wananchi katika ofisi ya mkuu huyo wa Mkoa na kueleza namna anavyohangaishwa kupata haki ya mali za marehemu muwe  licha ya kushinda kesi mahakamani mara kadhaa akipambania haki  yake. Akiongea katika viwanja hivyo mara baada ya kupatiwa msaada wa kisheria, Maryamu alisema aliolewa na marehemu  aliyemtaja…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv. Siha,Baraza la Madiwani Halmshauri ya Siha mkoani Kilimanjaro,limeomba Serikali kupitia (TARURA)isaidie kukarabati miundombinu mbali mbali ya barabara zilizoharibiwa vibaya na mvua za masika zinazoendelea kunyesha na kusababisha gharama za usafiri kuongezaka Pamoja na uharibifu wa miundombinu hiyo pia baadhi ya mashamba ya wakulima yamejaa maji na kuharibu mazao ikiwamo mahindi na maharage, hivyo kufanya baadhi ya Wananchi kukosa chakula cha kutosha. Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Dancani Urasa akisoma taarifa katika kikao cha kawaida cha Baraza hilo lilifanyika katika ukumbi wa halmshauri,Amesema hali ni mbaya mvua hizo zimekata kabisa mawasiliana baadhi ya maeneo Amesema kwa kipindi hiki…

Read More