Author: Geofrey Stephen

Na GEOFREY STEPHEN ARUSHA Nchi ya Somalia imejiunga Rasmi kuwa mwanachama wa nane wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki katika makao Makuu ya EAC Jijini Arusha na kuelezwa kuwa itasaidia suala Zima la msukumo wa changamoto za ajira kwa Nchi wanachama pamoja na kupanua soko la pamoja . Aidha Kujiunga kwa Somalia ni kutokana na kikao cha Wakuu wa nchi kilichoketi  November 24 mwaka Jana jijini Arusha,kukubali Nchi hiyo kujiunga na jumuiya ya Afrika Mashariki. Akiongea na waandishi wa habari Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo Dkt.Peter Mathuki katika sherehe fupi ya kupandisha bendera na kupokea hati za unachama wa…

Read More

Na Wandishi wa A24Tv. Moshi,Baraza kuu la WaislamuTanzania (BAKWATA), mkoa wa Kilimanjaro limesema litafanya semina ya elimu ya Ndoa kwa viongozi kuanzi ngazi ya Msikiti,Kata na Wilaya baada ya kugundua kwamba jambo elimu ya Ndoa imekuwa ndogo nakusababisha migogoro kuongezeka na familia kusambaratika Haya yamesemwa na Hussein Chifupa Kadhi wa mkoa huu wakati wa uzinduzi wa jengo la Ofisi ya BAKWATA Moshi mjini Mara baada ya kufanyiwa ukarabati ,na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwamo wa Dini. Akizungumza Mara baada ya uzinduzi huo,amesema watafanya ziara Wilaya zote mkoani hapo kwa lengo la kutoa elimu ya hiyo kutokana na baadhi ya…

Read More

Na Richard Mrusha Katavi Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi na wenye kampuni za uwakala wa utalii wametakiwa kujitokeza kuwekeza katika sekta ya utalii hasa kanda ya kusini hususani katika Hifadhi ya taifa ya Katavi. Wito huo umetolewa Machi mosi, 2024 na Mhifadhi Mkuu, Utalii na Mipango Kanda ya Kusini, Jonathan Kaihura mbele ya wanahabari waliotembelea hifadhi zilizoko kusini mwa Tanzania kujionea vivutio ndani ya hifadhi hizo. Moja ya sababu ya kutolewa wito huo hasa kwa hifadhi ya Katavi ni kuwapo kwa vivutio vya kutosha lakini havina msukumo wa kutosha kwa wawekezaji ambao ndio chachu ya kuvutia watalii. Hifadhi…

Read More

Na Mosess Mashala Zanzibar. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwa bega kwa bega tangu Mzee Mwinyi alipoanza kuugua mwezi Novemba alipopelekwa Uingereza kwa matibabu. Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo leo katika hitma na Dua Maalum ya kumuombea aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi ilyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika viwanja vya maonesho Nyamanzi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja tarehe 3…

Read More

Na Mwandiwhi wa A24tv . Wafanyabiashara wadogo mkoa Kilimanjaro wametakiwa kujitokeza muda utakapofika wa kujisajili na kupata vitambulisho ambavyo vitawasaidia mbalibali ikiwa ni kufanyabiashara bila ushumbufu wowote Hayo yalisemwa na Wilesteven Kavishe katibu wa shirikisho la umoja wa machinga Tanzanian mkoa wa Kilimanjaro (SHIUMA) ,wakati wa mkutano wa Wafanyabiashara hao uliofanyika ujumbi wa Big Shark Bomang’ombe. Katibu wa shirikisho hilo Wilesteven Kavishe Akizungumza na Wafanyabiashara hao Akizungumza katika mkutano huo ambao umejadili mambo mbali mbali ya maendeleao ikiwamo uchaguzi wa Serikali za mitaa na ujio wa Mwenge wa uhuru,amewataka Wafanyabiashara muda utakapofika wajisajili na kupata vitambulisho hivyo “Ni kweli tunategemea…

Read More

Buruani Mzee wa Ruksa Mzee Mwinyi , Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akiwasili katika Uwanja wa Uhuru, Jijini Dar es Salaam katika shughuli ya kuaga Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awamu ya pili Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi leo Machi 1, 2024. Mwili wa Rais Mstaafu wa awamu ya piliya  Jamhuri Muungano wa Tanzania Hayati Alhaj Ali Hassan Mwinyi ukiwa katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya viongozi na wananchi kutoa heshima ya mwisho leo Machi 1, 2024 . Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango…

Read More