Author: Geofrey Stephen

Na Doreen Aloyce,Dodoma Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi amewataka wataalamu waelekezi kutoka Kamapuni za DMG na TANSHEQ walioshinda zabuni ya Mkataba wa Upembuzi Yakinifu wa Ununuzi wa Meli za uvuvi wa Bahari Kuu na Ujenzi wa Viwanda vya Kuchakata Samaki,kukamilisha upembuzi kwa wakati ili Serikali ianze ujenzi wa meli katika Bahari Kuu na Viwanda vya kuchakata samaki. Dkt . Yonazi ametoa kauli hiyo Februari 27,2024 Jijini Dodoma baada ya zoezi la utiaji saini wa Mikataba ya kufanya upembuzi yakinifu wa kijenga Meli za Uvuvi wa Bahari Kuu na viwanda vya kuchakata samaka vitakavyojengwa…

Read More

Na mwandi wa A24tv Hai Siha,Serikali imeshauri kutoa elimu ya matatizo ya Afya ya akili ili jamii iweze kufahamu matatizo wanayopitia yanausiana na Afya ya akili au mambo mengine ili waweze kusaidika Haya yamejiri wakati wa mafunzo ya siku moja kuhusu matatizo ya Afya ya akili kuwajengea uwezo Jeshi la Polisi Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro ambayo yameandaliwa na Uchumi Bank iliyopo Wilayani humo. Edward Mwendamseke ambaye ni mwanasaikolojia mtaalamu wa matatizo hayo ,Akizungumza katika mafunzo hayo yaliyofanyika kituoni hapo amesema elimu itasaidia jamii kufahamu dalili matatizi ya Afya ya akili “Ni kweli kwa hali iliyopo kwa sasa ni muhimu jamii…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha. Mahakama imepiga hatua kubwa katika usikilizaji wa mashauri hususani mashauri ya mlundikano kutoka asilimia tano (5) kwa mwaka 2022 hadi kufikia asilimia mbili (2) kwa mwaka 2023. Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani ameyasema hayo jijini Arusha wakati akitoa maneno ya utangulizi akimkaribisha Mgeni Rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania katika hafla ya ufunguzi wa Mkutano wa mwaka wa Majaji Wafawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania. “Tangu mwaka 2022 ambapo kikao kama hiki kilifanyika hali ya utoaji haki kwa Mahakama Kuu imekuwa bora zaidi. Aidha amesema kuwa, muda wa wastani unaotumika tangu shauri…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv . Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Serikali itashughulikia changamoto zote za wafanyabiashara wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa bandari ya Malindi ikiwemo kufanya kazi usiku kwa kuwekewa taa na kazi kuendelea siku ya jumapili. Rais Dk.Mwinyi amesema hayo akizungumza na Jumuiya ya ushirika wa Majahazi na Wafanyabiashara katika bandari ya Malindi pia amezungumza na Wafanyabiashara wa soko kuu la Darajani katika mwendelezo wa ziara yake maalumu ya kutembelea masoko na kusikiliza changamoto zao Mkoa wa Mjini tarehe: 26 Februari 2024. Aidha Rais Dk.Mwinyi amewaomba wafanyabiashara kutopandisha bei ya vyakula…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki Dua ya khitma ya kumuombea Marehemu Mzee Masauni Yussuf Masauni, Baba Mzazi wa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe.Hamad Yussuf Masauni ambae amefariki tarehe: 23 Februari 2024 na kuzikwa makaburi ya Mwanakwerekwe tarehe: 24 Februari 2024. Dua hiyo imefanyika Msikiti wa Fatma Kilimani, Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe: 25 Februari 2024. Mwisho .

Read More

Na Mwandishi wa A24tv. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameondoa msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani(VAT) kwenye bidhaa ya sukari ili kuwasaidia wananchi kuelekea Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kutopanda bei ya bidhaa hiyo. Rais Dk.Mwinyi amesema hayo akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko kuu la Jumbi na Soko la samaki Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi tarehe:26 Februari 2024 katika ziara yake maalumu ya alipotembelea masoko na kusikiliza changamoto zao. Aidha, Rais Dk.Mwinyi amewaomba wafanyabiashara kutopandisha bei ya vyakula kiholela bila ya sababu za msingi kwa kupandisha mara mbili ya bei ili kuwasaidia…

Read More

Na. Richard Mrusha Katavi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amewataka Makamanda wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) kuratibu maeneo yao vizuri na kusimamia sheria za uhifadhi kama zilivyopitishwa na Bunge ili maliasilia zilizomo ziendelee kuleta tija kwa taifa, ameyasema hayo jana Februari 25.02.2024 aliposimama kuwasalimia wananchi wa kijiji cha Sitalike akiwa katika safari ya kikazi kuelekea kijiji cha Mpimbwe kilichopo Jimbo la Kavuu Mkoani Katavi. Akiwa amesimama kusikiliza kero katika kijiji hicho cha Sitalike kilichopo mpakani mwa Hifadhi ya Taifa Katavi, wananchi walimuomba aseme neno ili wapate fursa ya kuvua samaki…

Read More