Author: Geofrey Stephen

Na Mosses Mashala . Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole Ikulu Mnazi Mmoja kutoka kwa Luteni Jenerali Mstaafu Samuel Ndomba ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Mzinga kwa niaba ya uongozi wa shirika hilo,   kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi . Rais Dk.Mwinyi ameshukuru uongozi wa shirika hilo kwa kuja kumfariji. Mwisho .

Read More

Na Mwandishi wa A24tv. Waziri Wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera ,Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama ametoa wito kwa Baraza la Wafanyakazi. wa Ofisi hiyo,kupitia taarifa ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2023/24 na makadirio ya bajeti ya mwaka 2024/25. kwa umakini ili kuona yale yaliyotekelezwa kwa mwaka uliopita wa fedha na kuongeza ubunifu utakaowezesha rasilimali kidogo zilizotengwa kuleta matokeo makubwa zaidi kwa mwaka ujao wa fedha. Amesema kwa kufanya hivyo wataisaidia Ofisi hiyo  kufikia malengo na watamwezesha kila mtumishi kuwajibika ipasavyo na kwa weledi ili kupata mafanikio ya pamoja. Mhagama ametoa kauli hiyo Machi 18, 2024 jijini Dodoma…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv Siha Wananchi wa Siha mkoani Kilimanjaro Wamesema wana kila sababu ya kumpongeza mbunge wa Jimbo hilo Goodwin Mollel kwa kutatua changamoto mbalimbali za Wananchi ikiwa ni pamoja na kutoa fedha kwa wagonjwa wanaozuiliwa Hospitali kwa kushindwa kulipa gharama za matibabu wanazodaiwa. Mbunge wa Jimbo la Siha mkoani Kilimanjaro akisalimiana na Wakazi wa Sanya juu Wilayani humo Haya yamejiri akiwa viwanja vya Rex Sanya juu, wakati wa ziara yake kuongea na wananchi na pia kusikiliza kero zao zinazowakabili ili kuzipatia ufumbuzi Wakizungumzia wakiwa katika viwanja hivyo wamempa kongole mbunge huyo kwa mchango wake wa hali na mali…

Read More

Jina langu Selemani mkazi wa Mombasa, Kenya, nilikuwa nafanya kazi ya ulinzi nyumbani kwa Bosi wangu, nilifanya kazi hiyo kwa miaka zaidi ya 15 na niliipenda sana lakini mkasa niliyokuja kukutana nao ndio ulinifanya kuachana na kazi hiyo licha ya kumshinda Mahakamani. Kamwe siwezi kusahua tukio la kusingiziwa wizi na Bosi wangu kitu kilichopelekea kusota Mahakamani kwa miaka mingi hadi pale ambapo Jaji alisoma hukumu na kuonekana sina hatia. Hivyo nikawa nimeshinda kesi hiyo ingawa kila mtu alijua ningefungwa kutokana aliyenishtaki alikuwa mwenye uwezo mkubwa kifedha. Nakumbuka usiku mmoja nikiwa katika lango la Bosi wangu nilisikia harufu ambayo sikuweza kubaini…

Read More

Na Mosses Mashala Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole Ikulu Migombani kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wamasai waishio Zanzibar (ERETO), Ndg. Thomas Makau Lepachu na ujumbe wake kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe: 29 Februari 2024, Dar es Salaam na kuzikwa tarehe: 02 Machi 2024, Mangapwani, Mkoa wa Kaskazini Unguja . Jumuiya hiyo wamemkabidhi Mbuzi na Kondoo ikiwa ni sehemu ya rambirambi yao kwa utamaduni wao. Mwisho .

Read More

Na Mosses Mashala . Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole Ikulu Mnazi Mmoja kutoka kwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa upande wa Zanzibar wakiongozwa na Mohamed Aboud Mohamed , Leyla Burhan Ngozi  na Muhandisi Nasri Ally kufuatia kifo cha Baba yake Mzazi, Mwenyekiti wa CCM Taifa Mstaafu, Rais Mstaafu wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mzee Ali Hassan Mwinyi aliyefariki dunia tarehe: 29 Februari 2024, Dar es Salaam na kuzikwa tarehe: 02 Machi 2024, Mangapwani, Mkoa wa…

Read More