Author: Geofrey Stephen

By A24 Tv Mtaalii mmoja mwenye asili ya China amefariki dunia na wengine sita wamejeruhiwa baada ya gari la Watalii lenye namba za usajili T603 DCL mali ya Kampuni ya Yonda Africa walilokuwa wanalitumia, kupata ajali likiwa njiani kurudi hotelini kilomita moja kutoka Lobo Wildlife Lodge katika Hifadhi ya Taifa Serengeti. Taarifa iliyotolewa usiku huu na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) imesema “Majira ya saa 10 jioni July 28,2024 gari la Watalii lenye namba za usajili T603 DCL mali ya Kampuni ya Yonda Africa lilipata ajali likiwa njiani kurudi hotelini kilomita moja kutoka Lobo Wildlife Lodge katika Hifadhi…

Read More

Na Mwandishi Wetu-DODOMA Waziri wa Madini Mhe Anthony Peter Mavunde amepiga marufuku kwa wamiliki wa Leseni za uchimbaji mdogo wa Madini kuingiza wageni kutoka nje ya Nchi kwenye leseni zao bila kuwa na mikataba au makubaliano yaliyopitishwa kwa mujibu wa Sheria. Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Jijini Dodoma July 28,2024 wakati akizungumza na Wanahabari kuhusu Mwendendo wa makusanyo ya maduhuri yatokanayo na rasilimali madini Nchini kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024 na Katazo la Wageni kuungia kwenye PMLs bila kuwa na makubaliano ya msaada wa kiufundi(TSA). Na kupiga marufuku kwa Wageni wenye leseni kubwa za biashara ya madini hususan…

Read More

Na Richard Mrusha MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA)iliyo chini ya Wizara ya Afya, imetoa taarifa kwa Umma ufafanuzi kuhusu uvumi juu ya Dawa ya Paracetamol inayodaiwa kubabua ngozi. Kwa mujibu wa taarifa hiyo kwa Umma liyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa TMDA, DKT. Adam Fimbo Imebainisha kuwa, imebaini uwepo wa taarifa inayosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu uwepo wa dawa aina ya Paracetamol ambayo imeandikwa P 500 na kudaiwa kubabua ngozi kama inavyooneshwa (pichani). Akinukuu taarifa hiyo inayosambazwa mitandaoni: “Dawa hiyo inadaiwa kuwa ni ‘’paracetamol mpya nyeupe sana na inayong’aa, madaktari wanashauri kuwa ina virusi vya “Machupo”, inayochukuliwa kuwa…

Read More

Na Bahati Hai Wananchi Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro wanaalikwa kwenye Uzinduzi wa Mashindano ya West CHAMPIONS LEAGUE yatakayo anzakutimua vumbi Juma pili Julay 28 mwaka huu,Saa saba Mchana katika Uwanja wa Kilimahewa Matadi West Kilimanjaro Hayo yamesemwa leo na ELI Pius mwasisi wa mashindano hayo mwaka wa tatu ,ambapo amesema ya uzinduzi itakuwa kati ya Zinduka fc na Kware kutoka Wilayani Hai Zinduka FC imerudi Wale Mashabiki wa Zinduka wafike kwa Wingi kujakuiona Zinduka Mpya yenye Nguvu Mpya na Kasi ya 4G BURUDANI KEDEKEDE ZITAKUWEPO .TUTAKUWA NA WASANII WAKUMBWA WATAKAO PAFOMU KWENYE JUKWAA .WASANII KAMA MR VOICE POLELA ,DULLA NATION…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv. Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa amesema Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 inasisitiza suala la upatikanaji wa huduma bora ya chakula na lishe kwa Wanafunzi Shuleni ili kuwaepusha kukatiza masomo kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo njaa Dkt. Lyabwene amesema hayo leo Julai 25, 2024 jijini Dodoma katika Kongamano la Kitaifa la Utoaji Chakula na Lishe Shuleni, akisisiza kuwa kauli Mbiu ya Kongamano hilo inayosema *_Huduma ya chakula na lishe shuleni kwa afya na elimu bora_* inaakisi matakwa ya Sera ya Elimu na hivyo ni muhimu kuzingatia.      Kamishna wa…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv Arusha Taarifa fiche kutoka vyanzo vya ndani zinaeleza kwamba ushiriki wa wachezaji wa Riadha katika mashindano ya Olympic ya mwaka huu 2024 Paris Nchini Ufaransa huenda kikosi Cha timu ya Tanzania iliyo tarajiwa kwenda kwenye mashindano hayo licha ya maandalizi ya safari na Mazoezi kwa wachezaji safari inaelezwa huenda ikawa imeota mbawa kufuatia uvumi kupitia mitandao ya kijamii na makundi ya Whatsapp ya wadau wa Riadha nchini. Miongoni mwa taarifa zinabainisha kuwa dosari ya safari hiyo kusua sua ni kwasababu ya sintofahamu iliopo juu ya matumizi ya vifaa, vilivyo kabidhiwa katika Kambi hiyo hivi karibuni ikiwemo…

Read More