Author: Geofrey Stephen

GEofrey Stephen  ARUSHA MTANDAO wa Watetea wa haki za binadamu Tanzania(THRDC)umeomba kukutana na Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kuzungumzia hatima ya masuala ya utekaji na ukatili yanayoendelea nchini pamoja na kumkumbusha mikataba ya kimataifa ya kupinga ukiukwaji wa haki za binadàmu. Akiongea na vyombo vya habari katika mkutano mkuu wa 13 wa wanachama wa mtandao THRDC unaoendelea katika wiki ya AZAKI jijini Arusha, mratibu wa Taifa wa Mtandao wa kutetea haki za Binadamu, Onesmo Ole Ngurumwa alisema mkutano huo umelenga kuangazia masuala mbalimbali ikiwemo kupitia na kuidhinisha taarifa ya nusu muhula ya hali ya haki za binadamu ,utekelezaji…

Read More

Na Bahati .Siha Mashindano ya West Champion Ligi yanatarajiwa kufikia tamati September 15 mwaka huu katika uwanja wa kilima hewa Matadi Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro Timu zitakazo cheza Fainali hiyo ni Timu ya Roseline kutoka West Kilimanjaro Wilayani humo na timu ya Kware fc kutoka Wilayani Hai mkoani hapa Ambapo mgeni rasmi atakuwa Antony Mallya mdau mkubwa wa maendeleao Wilayani humo, mashindi wa tatu mechi yao itachezwa September 14 Mwaka huu, kati timu ya Nafco na Zinduka Fc kutoka Wilaya Siha. Eli Pius mwanzilishi wa lig hiyo Akizungumza na waandishi wa habari,amewataka Wananchi Wilayani humo, kujitokeza kwa wingi kwenye…

Read More

Mwandishi wetu,Longido Shirika la Wanahabari la usaidizi wa.jamii za pembezoni(MAIPAC) linatajia kuzindua mradi kabambe wa kuelimisha juu ya athari za ukeketaji kwa watoto wa kike katika jamii ya kifugaji ya kimasai ikiwa ni pamoja na kuwajengea wanawake uwezo wa kutetea haki zao. Mradi huo unafadhiliwa na shirika la Cultural Survival na unatarajiwa kusaidia pia kupaza sauti za vijana wanaopinga vitendo vya ukeketaji. Mkurugenzi wa Shirika la MAIPAC Mussa Juma alitoa taarifa hiyo katika ziara iliyofanywa na Asasi za kirai katika wiki ya Asasi hizo iliyofanyika wilayani Longido . “MAIPAC imebaini kuwa watoto wa miaka miwili hukeketwa katika Jamii ya…

Read More

Na Mwandishi  wa A24tv Arusha. Serikali imefanikiwa kupokea vifaa tiba vyenye thamani ya Shilingi milioni 6.5 kutoka kwa Benki ya NMB kwa ajili ya kusaidia utoaji wa huduma za afya kwa wagonjwa. Vifaa hivyo ni mashuka 100, viti mwendo (2) chuma za kutundikia dripu (5) pamoja na Vitanda na magodoro (8) ikiwemo vitanda vitano vya kulaza wagonjwa na vitatu vya kuwapumzisha kwa ajili ya vipimo. Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo Wilayani Monduli, Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Serikali na Ofisi ya Makao Makuu ndogo ya NMB-Dodoma, Vicky Bishubo amesema, lengo la msaada huo ni…

Read More

Na bahati Hai. wanaotoa vibali vya ukataji mit Wilayani i Hai waonywe kuchochea uharibifu wa mazingira Jumuhiya ya watumia maji na uhifadhi wa mazingira mto Kware Wilayani Hai mkoani Kilimanjaro ,wamesikitishwa na utoaji wa vibali vya kukata miti bila kufuata utaratibu hivyo kuhujumu harakati za kutunza mazingira. Hatua hiyo imekuja baada ya Jumuhiya hiyo kubaini miti kadhaa ikiwamo miruka na miringaringa imekatwa katika chanzo cha maji mto Kishenge kitongoji cha Maiputa Kata ya Masama Magharibi pembezoni wa Bondo la mama sawa,uku kibali kikionekana kutoka ofisi moja ya Serikali Wilayani humo. Mwenyekiti wa Jumuhiya hiyo, Wilfred Masawe ,akizungumza na waandishi…

Read More