Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv. RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ametoa wito kwa wadau mbalimbali kutambua umuhimu wa ushirikiano ili kufikia malengo kwa kuwekeza rasilimali fedha katika kuimarisha utafiti, kuboresha miundombinu ya afya, na kuhakikisha upatikanaji matibabu sawa kwa wagonjwa wa saratani nchini. Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika jukwaa la uwekezaji linalolenga kuimarisha huduma za saratani nchini, ukumbi wa Hoteli ya Hyatt Regency Dar es Salaam tarehe:06 Februari 2024. Vilevile Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa kupitia ushirikiano kati ya Serikali, sekta binafsi, watafiti na wataalamu wa tiba kunaweza kubadilisha taswira za huduma za matibabu ya…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv .Zanzibar. Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na sekretarieti ya kamati maalum, sekretarieti za Mikoa na Wilaya CCM Zanzibar katika kikao chake cha kwanza na watendaji hao ukumbi wa Afisi kuu CCM Kisiwandui tarehe: 5 Februari 2024. Aidha, Makamu Mwenyekiti CCM Dk.Mwinyi amesema kazi kuu ya Chama cha siasa ni kushinda chaguzi za dola. Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Mwinyi amempongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kusimamia vema Chama cha Mapinduzi na kukiimarisha.…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv . Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa bodi ya wadhamini Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) Mhe.Mama Mariam Mwinyi ametoa wito kwa jamii kutumia mbinu mbalimbali za kuimarisha lishe kwa watoto na mama wajawazito ambazo zitachangia hatua za awali za ukuaji wa mtoto tangu mimba inapotunga, wakati wa ujauzito na baada ya kuzaliwa hadi kufikia umri wa miaka miwili. Mama Mariam Mwinyi amesema hayo katika mkutano wa wadau wa masuala ya afya na lishe kupitia mradi wa lishe unaotekelezwa kwa mashirikiano kati ya Wizara ya Afya Zanzibar, Taasisi ya Benjamin Mkapa na…

Read More

TAARIFA KWA UMMA Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mzee Ali Hassan Mwinyi amepelekwa hospitali akiugua maradhi ya kifua. Anaendelea kupata matibabu chini ya uangalizi wa karibu wa madaktari. Kutokana na ushauri wa madaktari wake, familia imeona ni vyema apate faragha akiwa anapatiwa matibabu. Hivyo Familia inaiomba jamii kumkumbuka kwenye Dua, Sala, na Maombi. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amjaalie shifaa ya haraka Mzee wetu pamoja na wagonjwa wengine wote wanaokabiliwa na maradhi mbali mbali. Abdullah Ali Mwinyi Msemaji wa Familia

Read More

Na GEOFREY STEPHEN ARUSHA . Wanafunzi katika Kata ya Ngarenaro Jijini Arusha wametakiwa kutokaa kimya dhidi ya vitendo vya Ukatili wa kijinsia pindi vinapotokea au kuona viashiria vyake na badala yake watoe taarifa kwenye ofisi za serikali ama kituo chochote cha Polisi. Wito huo umetolewa leo Februari 02, 2024 na Mkaguzi Kata ya Ngarenaro Jijini Arusha, Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Tadey Tarimo wakati akitoa elimu juu ya ukatili wa kijinsia katika shule ya Msingi Swift Juniour Academy School iliyopo mtaa wa kambi ya fisi katika kata hiyo. A/INSP Tarimo amewatoa hofu wanafunzi hao na kuweleza kuwa, Polisi siyo adui bali…

Read More

Na. Anangisye Mwateba- Dodoma Serikali imewezesha ujenzi wa viwanda saba (7) vya kuchakata na kufungasha asali katika Wilaya za Sikonge, Mlele, Nzega, Tabora, Manyoni, Kibondo na Bukombe vitakavyotumika kuongezea thamani asali inayozalishwa na kuuzwa katika masoko ya ndani na nje ya nchi. Haya yamebainika wakati Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) akijibu swali la Mhe. Athuman Almas Maige Mbuge wa Tabora Kaskazini katika kikao cha cha tatu cha Mkutano wa 14 wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaondelea jijini Dodoma aliyetaka kujua Je Serikali ina mpango gani wa kufanya asali kuwa moja ya zao la…

Read More