Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24tv .Africa Kusini . Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafisa Wakuu wa Biashara (STO) wa Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) amezisisitiza Nchi wananchama wa Mkataba huo kushirikiana kwa usawa kurekebisha sera zinazowezesha kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi hizo. Mwenyekiti huyo wa STO Dkt. Abdallah ameyasema hayo Januari 26, 2024 alipokuwa akifungua Mkutano wa 16 wa Kamati ya Maafisa Wakuu wa Biashara wa AfCFTA unaofanyika Durban, Afrika Kusini, kuanzia tarehe 26 hadi 29 Januari 2024 ukiongozwa na Tanzania, ambayo ni Mwenyekiti wa AfCFTA kwa mwaka huu…

Read More

Na Mwandishi wetu,Babati. Kampuni ya Uwindaji wa Kitalii ya EBN Hunting Safari Ltd ambayo inafanya shughuli zake katika kitalu cha uwindaji cha Hifadhi ya Jamii ya wanyamapori ya Burunge wilayani Babati imetoa gari aina ya land cruiser ili kusaidia shughuli za uhifadhi na Kupambana na ujangili katika eneo la Burunge WMA. Gari hilo ambalo limegharimu shilingi 205 milioni limekabidhiwa na Katibu wa EBN Hunting Safari Ltd , Charles Sylvester kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Babati,Anna Mbongo ambaye nae aliwakabidhi viongozi wa Burunge WMA. Akizungumza wakati wa kukabidhi gari hilo, Sylvester amesema gari hilo ni sehemu ya makubaliano ya…

Read More

Na mwandishi wetu Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameeleza kuwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan anataka kuona viongozi wote wanatatua kero na changamoto za wananchi na kwamba anasikitishwa na baadhi ya viongozi ambao hawatatui changamoto za wananchi mpaka pale anapofanya ziara katika maeneo mbalimbali nchini. Dkt. Biteko amesema hayo tarehe 25 Januari, 2024 wakati akizungumza na wananchi katika Kijiji cha Magodi na Kigandini wilayani Mkinga mkoani Tanga mara baada ya kuwasha umeme katika vijiji hivyo ambao umesambazwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Katika ziara yake kwenye Vijiji hivyo, aliambatana na Mkuu wa Mkoa…

Read More

Na Richard Mrusha Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde ametoa Wito kwa Kampuni, Taasisi na Watu binafsi wanaotarajia kushiriki Mkutano wa Mining Indaba kuhakikisha wanaiweka Tanzania katika ramani ya dunia kwa kutangaza utajiri wa madini na fursa za kiuwekezaji zilizopo. Amesema kutokana na fursa mbalimbali katika Sekta ya Madini kuanzia kwenye shughuli za utafiti, uchimbaji, utoaji huduma migodini na uongezaji thamani madini ni alama tosha ya kuitambulisha Tanzania kwa sauti moja kwa wadau mbalimbali watakaoshiriki katika mkutano huo mkubwa. Waziri Mavunde ameyasema hayo wakati akifungua kikao maalum cha wadau wanaotarajia kushiriki katika mkutano wa Mining Indaba utakaofanyika kuanzia tarehe 5…

Read More

Na Mwandishi wetu kiteto Wanamchi wa Eneo la Nderekeshi wilayani simanjiro  mkoani Manyara wamelalamikia Barabara ya Kiteto Simanjiro kutopitika kwenda mkoani Arusha hali ya barabara eneo ni mbaya wananchi hao ambao asilimia kubwa ni wakulima na wafugaji wameomba viongozi wa mkoa  Manyara Mbunge pamoja na Meneja wa Tan Roads kusikia kilio chao . Wananchi hao wamesema kwamba  hakutakuwepo na usafiri wilaya hizi mbili Nairero kuna mahali kilimani inataka kukatika jambo litakalo sababisha watu kupoteza maisha . Kwa sasa mabus yanatokea kiteto yanaingia Arusha usiku saa moja au saa kumi na mbili kuanzia walipo anza safari muda wa saa 12.00 alfajiri.…

Read More

Na Richard Mrusha Kitulo AFISA Mhifadhi mkuu wa Kanda ya Kusini Jonathan Kaihura Ametoa wito Kwa watanzania kujenga tabia ya kutembelea vivutio mbalimbali vilivyopo katika hifadhi zetu hapa nchini na hasa hifadhi ya Taifa ya kitulo iliyopo katika mikoa ya Njombe wilayani Makete. Na Mkoa wa Mbeya wilaya ya Rungwe na mbeya vijijini Amesema kuwa mara zote pamekuwa na dhana ya kwamba wanaopaswa kutembelea na kufanya utalii ni wageni kutoka nie ya Tanzania jambo ambalo si sawa hivyo nivema wakajenga tamaduni ya kufanya utalii kwenye hifadhi mbalimbali hapa nchini . Kaihura ametoa wito huo Leo January 22 ,2024 wilayani makate…

Read More