Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24tv. Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula amesema jumla ya Shule 96 za Sekondari teule zitaanza utekelezaji wa kutoa masomo ya Amali, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mitaala mipya ya elimu iliyoboreshwa. Dkt. Rwezimula ametoa kauli hiyo Januari 08, 2024 mkoani Morogoro wakati akifungua mafunzo kwa walimu kutoka shule teule 28 za serikali na 68 zisizo za serikali ambazo zitaanza kutoa elimu ya sekondari mkondo wa Amali katika awamu ya kwanza. Dkt. Rwezimula amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwani maono yake yameleta msukumo mkubwa na kupelekea kuwa na Sera ya…

Read More

Na mwandishi wetu Zanzibar Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, amefungua Jengo la Afisi ya Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) lililoko eneo la Madema, Zanzibar na kupongeza mafanikio na ushindi wa kufanikisha miradi hiyo muhimu kwa maendeleo ya Zanzibar. Dkt Biteko amesema, kuelekea Kilele cha Mapinduzi ya Zanzibar, watu waliopewa dhamana ya kusimamia miradi hiyo ambayo Serikali imepeleka fedha nyingi, wafanye kazi kwa uaminifu kwani watatatoa hesabu si tu kwa waliowaweka madarakani, au Wananchi bali kwa Mwenyezi Mungu, hivyo wafanye kazi kwa uaminifu mkubwa. “Nitoe wito kwenu ZAWA hakikisheni mnawahudumia vema Wazanzibari, ili waone fahari…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv . Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) alitoa wito kwa Watanzania kuacha kununua bidhaa zinazotoka nje ya nchi Ilihali zinazalishwa nchini na kwa viwango vyenye ubora unaokidhi mahitaji ya soko la ndani na nje. Aliyasema hayo Januari 6,2024 Dar es Salaam baada ya kutembelea Viwanda vya Motisun (IMMI Steel) vinavyozalisha bidhaa mbalimbali ikiwemo bati, nondo, plastiki, juisi na rangi. Aidha Dkt. Kijaji pia alosema vipo viwanda nchini vinavyozalisha bidhaa zenye ubora unaostahiki na kwamba Watanzania waache kukimbilia nje ya nchi,badala yake wanunue bidhaa zinazozalishwa nchini. “Tanzania ina viwanda vinavyotengeneza bidhaa nzuri zisizo na…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Balozi . Dkt. Moses Kusiluka amesema Serikali itaendelea kutoa ushirikiano katika ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Viwanda zaidi ya 200 unaoendelea kutekelezwa katika eneo la Kwala Kibaha Mkoani Pwani. Katibu Mkuu Kiongozi Kusiluka ameyasema hayo Januari 5,2024 akiongozana na Mawaziri na Wakuu wa Taasisi mbalimbali katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Mradi huo unaotarajiwa kuwa na viwanda zaidi ya 200 uliopo katika eneo la Kwala Mkoani Pwani. Amesema Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan inaunga mkono…

Read More