Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24tv . RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema amewahi kufanya kazi na Hayati Edward Lowassa kwa vipindi tofauti katika Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya awamu ya tatu na awamu ya nne. Amesema taarifa ya msiba huu ameipokea kwa masikitiko makubwa, pia anatoa pole kwa niaba ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na wananchi wote kwa ujumla. Rais Dk. Mwinyi ameyasema hayo alipofika nyumbani kwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Hayati Edward Lowassa, akiwa na Mama Mariam Mwinyi, kwa lengo la kuwafariji wanafamilia wa marehemu akiwemo Mama Regina Lowassa, Masaki,…

Read More

Na. Anangisye Mwateba-Dodoma Wizara ya Maliasili na Utalii imekamilisha mchakato wa kufanya tathmini ya malipo ya kifuta jasho/ machozi ambapo kiasi cha shilingi Bilioni Moja na Milioni Mia Sita zinatakiwa kulipwa kupitia Wizara ya Fedha. Haya yamebainika wakati Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula akijibu swali la Mhe. Dkt. David Mathayo David(Mb) aliyetaka kujua lini Serikali itafanya mapitio ya Sheria na Kanuni za fidia kwa waathirika wa wanyamaporir ili kulipa fidia ya gharama halisi tofauti na sasa. Aidha, Wizara imekamilisha mapitio ya Kanuni za Kifuta Jasho/Machozi na kuiwasilisha Wizara ya Fedha ili kuona uwezekano wa kuongeza viwango…

Read More

Doreen Aloyce, Dodoma Naibu Waziri wa Afya Dkt. Godwin Mollel amewataka wananchi kuepuka matumizi yasiyo sahihi ya vidonge vya kuzuia mimba maarufu kama P2 ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza pale dawa hizo zinapotumika bila utaratibu ikiwemo mvurugiko wa hedhi. Dkt. Mollel amesema hayo leo Jijini Dodoma kwa niaba ya Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu wakati akijibu swali Namba 163 ambapo swali hilo limeulizwa na Mbunge wa Viti Maalum, Dkt. Thea Medard Ntara aliyeuliza Je, kuna mpango gani wa kuruhusu Sayana Press kama njia ya Uzazi wa Mpango badala ya kutumia P2 bila utaratibu. Amesema P2 ni njia ya dharura…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amesema, serikali inajivunia ushirikiano mzuri uliopo kati yake na taasisi za dini ambao umedumu kwa muda mrefu katika nyanja mbalimbali na inatambua na kuthamini mchango mkubwa wa Kanisa katika utoaji wa huduma za jamii, hususan elimu, afya na maji. Aidha ameiagiza Wizara ya Afya kuhakikisha inatatua changamoto zinazokwamisha ubia baina ya serikali na Hospitali ya Arusha Lutheran Medical Center kutatuliwa haraka iwezekavyo.   Dkt Mpango amebainisha hayo wakati aliposhiriki Ibada ya kuwekwa Wakfu na Kuingizwa kazini kwa Askofu Mteule Dkt Abel Godson Mollel na msaidizi wake Mchungaji Lareiton Lukumay…

Read More

Na Mwndishi wa A24tv . Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali inaendelea kutoa kipaumbele kwa wanaosoma masomo ya Sayansi ikiwemo kutoa ufadhili wa masomo ili kuongeza hamasa kwa Vijana wa kitanzania wakiwemo wasichana kupenda kusoma masomo hayo. Prof. Mkenda ametoa kauli hiyo Februari 11, 2024 mkoani Arusha katika Siku ya Kimataifa ya Wanawake na Wasichana katika Sayansi, ambapo amesisitiza kuwa serikali pia itaendelea kuwekeza katika mazingira mazuri kwa ajili ya Vijana kupata fursa mbalimbali katika nyanja za Sayansi za masomo na kuendeleza ubunifu ili kuendana na kasi ya teknolojia duniani na hata soko la ajira…

Read More

Na GeofreyStephen . Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Stephen Mbundi akiongoza ujumbe wa Tanzania kushiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) kilichofanyika jijini Arusha tarehe 09 Februari 2024. Mkutano huo ulijumuisha Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kutoka Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo DRC na Sudani kusini uliongozwa na Südani Kusini kama Mwenyekiti. Ujumbe wa Tanzania…

Read More