Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen Arusha . Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zimekubaliana kuimarisha ushirikiano wao katika nyanja ya biashara na uwekezaji na kuingia mikubaliano kwa pamoja kama EAC na Jumuiya nyingine za kikanda na kimataifa ili kukuza biashara na kuimarisha ushindani wa EAC katika soko la dunia. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb.) alipokuwa akiongea na vyombo vya habari mara baada ya kushiriki Mkutano wa Baraza la Mawaziri la Kisekta wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) uliofanyika Februari, 9, 2024 jijini Arusha, Tanzania. Aidha, amebainisha kuwa Nchi hizo zimekubaliana kusaidia…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv . Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameshiriki dhifa ya chakula cha mchana iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan kwa heshima ya mgeni wake Rais wa Poland Mhe.Andrzej Sebastian Duda. Ikulu Dar es Salaam tarehe :09 Februari 2024. Katika hafla hiyo Rais Dk.Mwinyi amesalimiana na viongozi mbalimbali wa Serikali, Vyama vya siasa, Dini na Wastaafu. Aidha baada ya kushiriki hafla hiyo Rais Dk.Mwinyi anatarajiwa kurejea Zanzibar. Mwisho

Read More

Mwandishi wetu, MAIPAC maipacarusha20@gmail.com Chato. Hifadhi ya Taifa ya Burigi -Chato, Sasa ipo tayari kupokea malfu ya watalii baada ya Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA) kukamilika miundombinu ya barabara na mawasiliano ambayo awali ilikuwa ni shida. Hifadhi hii iliyonzishwa mwaka 2019 ,kiasi cha sh bilioni 3.3 tayari zimetumika kuimarisha miundombinu yake ili watalii wa ndani na nje waweze kutembelea . Mkuu wa hifadhi hiyo, Kamishna Msaidizi Ismaili Omari akizungumza na waandishi wa habari za Utalii na Uhifadhi waliotembela hifadhi hiyo, alisema wanaalika watalii kutoka ndani na nje ya nchi kutembelea hifadhi hiyo. ” Shirika la hifadhi za Taifa (TANAPA…

Read More

Mwandishi wetu.babati Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Anna Mbogo amewahamasisha Viongozi wa vikundi 10 vilivyomo katika eneo la jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapiri ya Burunge kuhifadhi kumbukumbu zao za fedha Kwa usahihi ili kuepusha migogoro itakayosababisha vikundi hivyo kuvunjika. Ameyasema hayo Leo February 7 wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku tatu Kwa Viongozi wa vikundi hivyo, iliyoandaliwa na Taasisi ya Chemchem Association inayofanya shughuli za uhifadhi katika Jumuiya ya Hifadhi Burunge iliyopo mkoani Manyara. amesema kuwa baadhi ya mambo yanayosababisha vikundi kuvunjika ni pamoja na kuto kutunza kumbukumbu Kwa usahihi na kutumia fedha za kikundi bila utaratibu…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv . Serikali imetoa wito kwa Watanzania kuwekeza zaidi katika viwanda vya maziwa nchini kutokana na kutolewa kwa kodi nyingi katika viwanda vya bidhaa hiyo pamoja na kuwepo kwa soko la ndani na nje ya nchi. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe Februari 7, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Viti maalum mkoa wa Tabora, Mhe. Jacqueline Kainja, lililohoji Mpango wa Serikali kutenga fedha ili kuanzisha viwanda vya maziwa ili kuwaondolea wafugaji adha ya kupoteza maziwa. “Ni kweli kuna upotevu wa maziwa kwa Mkoa wa Arusha na Mikoa mingine, Mkakati…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv. Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameagiza taasisi zinazo husika na sheria kukamilisha mchakato wa utungaji wa sheria ili kuanza kazi kwa Mahkama Maalum ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu uchumi kwa mwaka huu. Rais Dk.Mwinyi amesema hayo katika kilele cha Maadhimisho ya siku ya Sheria Zanzibar katika viwanja vya Mahkama kuu Tunguu, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe 07 Februari 2024. Aidha Rais Dk.Mwinyi ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuchukua hatua za kuimarisha mhimili wa Mahkama na Taasisi zote za Sheria ili ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi, hatua hizo ikiwemo…

Read More

Na mwandishi wetu Capetown Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali amesema Tanzania imelenga kuwa Kitovu cha Madini Barani Afrika sababu ambayo imepelekea Serikali kuendelea kuboresha mazingira ya uwekezaji katika Sekta ya Madini. Ameongeza kwamba, Wizara imeweka utaratibu wa kukutana na kampuni kubwa na za kati zilizowekeza katika miradi ya madini nchini kila robo ya mwaka ili kujadili na kutatua kero ambazo zinaweza kusababisha ucheleweshaji wa masuala yanayohusu uwekezaji na kuongeza kuwa, tayari wizara imekwishateua maafisa maalum ambao ni mabalozi wa kila mradi hiyo. Mahimbali ameyasema hayo Februari 6, 2024 wakati akichangia katika mdahalo maalum uliolenga kujadili ufunguaji wa fursa…

Read More