Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24tv. Kreta, Arusha. Serikali kupitia wizara ya Maliasili na Utalii kwa mara ya kwanza imepokea Faru weupe 17 kutoka kampuni ya AndBeyond ya nchini Afrika Kusini kwa lengo la kuimarisha shughuli za uhifadhi, utafiti na elimu katika eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Akipokea faru hao katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika kreta ya Ngorongoro tarehe 4 machi, 2025 Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Balozi, Dkt. Pindi Chana (Mb) amesema mradi wa kuwaleta faru weupe  Tanzania unalenga kuimarisha shughuli za uhifadhi na kupanua wigo wa watafiti ambao kupitia faru hao watasaidia  kutoa elimu kwa  wananchi na…

Read More

Siha, Watu wasijulikana wamehujumu miundombinu ya Tanesco Kitongoji cha Ekwenywa Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro kwa kung’oa nguzo mbili ndogo za umeme na kutoweka nazo Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti, wamesema tukio hilo limetokea February 18, 2025 na kusababisha usumbufu kwa Wananchi wa maeneo hayo “Ni kweli upepe unapokuja zile waya zinatikisika usababisha taa kuzima na kama wapo mashine kwa ajili kushanga unga huduma inasitishwa ku to okana na moto kutotulia “wamesema Wananchi hao. Jeremia Mollel mkazi wa eneo hilo anasema siku ya tukio aliona gari ya Tanesco likiwa na watumishi katika kitongoji hicho ,walifika na kupanda juu…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv Hai, Wananchi wanaoenda kupata huduma hospital ya wilaya Hai mkoani Kilimanjaro,Wametakiwa kutoa taarifa kwa Viongozi wa hospital hiyo pindi wanapopata changamoto yeyote kutoka kwa watumishi wa hospital hiyo ikiwamo ya lugha chafu kwa wagonjwa Hayo yamesemwa na Mganga Mkuu wa Wilaya Itikija Msuya February 27 wakati wa ziara ya Mbunge wa Jimbo hilo Saashisha Mafuwe,kuongea na Wananchi kuhusu yale aliyoaidi kuyafanya katika ilani ya chama( CCM) yamekifikia wapi, pamoja na kusiliza kero za Wananchi haona , Ambapo kero mmoja wapo waliyo zungumza Wananchi wa kata ya Bondeni ilikuwa ya Hospital ya wilaya hiyo ,ikiwamo ukosefu wa…

Read More

Na Mosses Mashala . Mke wa Rais wa Zanzibar, Msarifu na Mwenyekiti wa Bodi ya wadhamini ya Zanzibar Maisha Bora Foundation (ZMBF) , Mhe.Mama Mariam Mwinyi amesema takriban wananchi 5,000 wamepatiwa huduma za afya jumuishi kwa watu wa makundi yote hususan Wanawake, Watoto, Vijana na Watu wenye ulemavu kupitia kambi za matibabu za Afya Bora, Maisha Bora chini ya ZMBF. Mariam Mwinyi amesema hayo alipozindua Kampeni ya “We Are Equal” (yaani kwa Kiswahili Tupo Sawa) inayoratibiwa na Taasisi ya Maendeleo ya Wake wa Marais wa Afrika (OAFLAD) na kufunga kambi ya nne ya matibabu ya “Afya Bora, Maisha Bora” katika…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha. MRADI wa Tanzania ya Kidijitali unaofadhiliwa na Benki ya Dunia(WB) umefikia asilimia 80 ya utekelezaji wake huku lengo likiwa ni kuweka mazingira wezeshi, kutoa huduma bora na miundombinu wezeshi kwa wananchi ili wanufaike. Aidha mradi huo ambao unasimamiwa na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma umefanikisha kupeleka wataalamu 50 kusoma shahada ya pili na wengine 400 kupata mafunzo. Akizungumza jana Jijini Arusha, Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Mafunzo na Huduma za Tehama kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ,Mohammed Mshaka,wakati wa kufunga kikao cha kufanya tathimini…

Read More

MAAFISA Raslimali watu na utawala wamehimizwa kutumia mifumo ya sasa ya kazi kwa kuzingatia misingi ya kidigitali ili kurahisisha utendaji wao na hivyo kuondokana na mfumo wa zamani wa kutumia karatasi kujaza taarifa ambao hauna tija Hayo yamesemwa na Issa Sarboko Makarani,ambae ni Mkurugenzi wa mipango,Sera na Utafiti wa mafunzo ,Wizara ya mawasiliano,uchukuzi na mawasiliano Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,alipokuwa akifungua mafunzo ya kimataifa ya Maafisa Raslimali watu na utawala kutoka mataifa mbalimbali wanaokutana jijini Arusha kwenye kikao cha siku mbili. Amesema kuwa mifumo ya utendaji kazi Ulimwengu imebadilikana mazingira ya kazi nayo yamebadilika hivyo maafisa hao hawana budi kuhakikisha wanatumia…

Read More