Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv . Waziri wa Vjwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji(Mb) ametoa rai kwa vijana wa Tanzania kuendelea kujielimisha na kupata ujuzi mbalimbali ili kuwa tayari kuajiriwa na viwanda mbalimbali vinavyoendelea kujengwa nchini kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza nchini hususani katika kujenga viwanda. Ameyasema hayo Desemba 11, 2023 alipotembelea Kiwanda cha Saturn Corporation limited kilichopo Kigamboni Dar es salaam lengo la kuangalia ujenzi unaoendelea katika Kiwanda hicho kinachounganisha magari ya SINOTRUCK aina ya Howo na Tipper “Tuliahidi uko nyuma na Mheshimiwa Rais amesema…

Read More

Na Richard Mrusha Simanjiro UONGOZI wa Kampuni ya Franone Mining and Games limetd inayojishughulisha na uchimbaji madini ya vito ( Tanzanite) imeungana na watanzania wengine na Serikali katika kuchangia mahitaji mbalimbali ya chakula Kwa wahanga wa mafuriko wilayani Simanjiro mkoani Manyara . Akizungumza na waandishi wa Habari Disemba 10,2023 Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Vitus ndakize Amesema kuwa wameguswa sana na tukio hilo hivyo wao kama watanzania waliowekeza kwenye uchimbaji wa madini na wao wameona wachangie watanzania wenzao ambao wamepatwa na majanga hayo Kwa kutoa bidhaa mbalimbali. Amesema miongoni mwa vitu ambavyo wamechangia na kukabidhi Kwa mkuu wa Wilaya Dkt.…

Read More

Na John Mhala,Monduli Mfanyabiashara Maarufu wa Madini ya Tanzanite Mkoani Arusha,Sanare Mollel maarufu kwa jina la Muller mkazi wa Kijiji cha Moita Bwawani kata ya Moita Bwawani wilayani Monduli Mkoani Arusha anatuhumiwa kuwapiga na kuwajeruhi wananchi na wafanyakazi wa idara ya ardhi Halmashauri ya Monduli na kuwatishia kwa silaha aina ya bastola kwa hatua yao ya kwenda katika Kijiji hicho na kupima ardhi ya eneo la malisho ekari 7000 kuwa eneo la makazi bila lidhaa ya wananchi. Akizungumza na waandishi wa habari,Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} Kata ya Moita Bwawani Loseriani Loibanguti Kimbele alisema kuwa Mulle aliamua kufanya hivyo na…

Read More

Na Richard Mrusha Dodoma. MAKAMU wa Rais Dkt. Philip leo Desemba 10,2023 akiwa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma ambako ameshiriki Ibada ya jumapili ameitaka Mitandao ya kijamii Nchini itumike vizuri pasipo kupotosha Umma. Dkt. Mpango ameongeza kuwa mitandao ya kijamii ni mizuri na ni mibaya hasa ikitumika vibaya inapotosha Umma na kutumia nafasi hiyo kuwataka isitumike vibaya. “Ahsanteni sana kwa kuniombea yamesemwa mengi na wengine wamesema mimi ni mzuka, zaburi ya 118 aya ya 17 inasema sitakufa bali nitaishi na kuyasimlia matendo makuu ya MUNGU kwa hiyo Mitandao ni mizuri lakini…

Read More

Na Richard Mrusha Dodoma AFISA Utumishi wa Chama cha walimu Taifa CWT Neema Ezekia Amesema maadhimsho ya siku ya walimu Duniani Kwa utaratibu wa Chama hicho taifa yanafanyika kila baada ya miaka minne na mwaka huu yalikuwa yafanyike Novemba 4,2023 Kwa ratiba iliyokuwa imepangwa. Amesema kuwa maadhimisho ambayo yamefanyika katika ngazi za Wilaya ni Kwa utaratibu ukizingatia siku hiyo ni siku ya walimu Duniani lakini kitaifa lazima yaadhimishwe kitaifa na yaratibiwe na ngazi ya juu ya Chama hicho. Neema ameyasema hayo Disemban 8 ,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kutolea ufafanuzi kuhusu Malalamiko na shutuma zinazoletwa…

Read More

Na Ahmed Mahmoud Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha kimepongeza waandaaji wa mbio za Mount Meru Marathon Kwa kujitolea vifaa mbalimbali kusaidia Uzazi Salama kwa wakinamama wasio na uwezo wa kununua vifaa vya kujifungulia. Akiongea Mara baada ya kuwakabidhi vifaa hivyo katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru na kuzindua Bonanza hilo la kesho katika viwanja vya Ngarenaro Katibu wa itikadi na Uenezi Mkoa wa Arusha Saipulan Ramsey Jijini Arusha amesema Mount Meru Marathon imeonyesha kuunga Ilani ya CCM. Amesema katika Ilani yao ukurasa wa Tano inaeleza kuimarisha huduma za mama na mtoto na niwapingeze kwa kugusa ibara ya 8…

Read More