Author: Geofrey Stephen

HABARI PICHA Na mwandishi wetu Dkt. Yonazi aridhishwa na maandalizi ya Kuelekea Siku ya UKIMWI Duniani Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ametembelea mabanda mbalimbali na kujionea maandalizi yaliofanywa na wadau mbalimbali kuelekea Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yatakayofanyika 1 Disemba,2023 katika Viwanja vya Morogoro Sekondari ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa(mb) Kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Jamii Iongoze Kutokomeza UKIMWI” Aidha ametumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kujitokeza katika maadhimisho hayo na kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Wito umetolewa kwa watafiti na wanataaluma nchini kujikita katika kufanya tafiti zenye tija kwa Taifa na zinazoleta majawabu kwenye changamoto zinazoikabili jamii inayowazunguka. Wito huo umetolewa leo na Naibu Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA) Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam, Prof. Epaphra Manamba; alipomwakilisha Mkuu wa Chuo katika ufunguzi wa Kongamano la Kitaaluma la Vitivo linalowahusisha wanataaluma na wanafunzi wa shahada ya Uzamili IAA katika kuwasilisha tafiti zao, machapisho na kufanya mijadala ya kina. Prof. Manamba amesema kupitia kongamano hilo wanafunzi wamewasilisha tafiti zinazolenga kuangalia Taifa kwa baadaye kwenye maeneo ya Uchumi,Bima,Utalii, Fedha,…

Read More

Na Anangisye Mwateba-Arusha Naibu Waziri wa Maliasili na utalii Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) amewataka wanataaluma waliopo katika vyuo vya misitu kutumia taaluma za kupata suluhisho la migogoro ya mipaka kati ya hifadhi za misitu na makazi ya wananchi. Mhe. Kitandula ameyasema hayo alipokuwa kwenye ziara ya kutembelea Taasisi ya Elimu ya Misitu Olmotonyi jijini Arusha na kuongeza kuwa wanataaluma hao wanategemewa na Taifa kutokana na maarifa wanayoyapata vyuoni. Aidha, Mhe. Kitandula ameongeza kuwa kwa sasa wizara ya maliasili na utalii iko kwenye mkakati wa kuunganisha vyuo vyote vilivyo chini ya wizara ya maliasili ili viwe chini ya Chuo kimoja lengo…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv . huyo wa Kijiji Pendeza anahisa asilimia 75  na Kijiji kinamiliki hisa asilimia 25 lakini shughuli zote za uendeshaji zinafanywa na Pendeza na uzalishaji ukipatikana kila mmoja anapaswa kupata haki yake kwa mujibu wa mkatana. Alisema madini ya ruby yanayozalishwa yanapaswa kuwekwa mezani ili bodi ya usimamizi wa mgodi ya Kijiji ijue na kabla ya mgao na shughuli zote zisimamiwa na maofisa wa Wizara ya Madini kabla ya serikali kuchukua kodi yake. Waziri Kiruswa aliwataka waendesha shughuli za uchimbaji kushirikiana na Bodi ya Kijiji yenye wajumbe tisa katika shughuli za kila siku na uzalishaji ukipatikana ili kuondoa…

Read More