Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24tv Lushoto Novemba 24, 2023. Mahakama ya Kisasa Wilayani Lushoto itakayotumika kwa shughuli za Kimahakama pamoja na kuwa sehemu ya utoaji Mafunzo kwa wanafunzi watakaopita katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama (IJA) kilichopo Wilayani Lushoto inatarajiwa kujengwa muda wowote kuanzia sasa. Kauli hiyo imetolewa na Mgeni Rasmi Jaji Mkuu wa Tanzania *Mhe. Profesa Ibrahim Hamis Juma* alipokuwa alihutubia katika Mahafali ya 23 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama (Institute of Judicial Administration) – IJA yaliyofanyika leo tarehe 24/11/2023 chuoni hapo. Wanafunzi wapatao 800 wa ngazi mbalimbali ikiwemo Shahada wamehitimu leo. Mhe. Jaji Mkuu emeeleza kufurahishwa na wazo…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha  Zoezi la kuchukua Fomu limefungwa Rasmi jana November 23 Majira ya Saa kumi kamili za jioni huku  Makada wapatao 83 wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Arusha wakirejesha Fomu za kuwania nafasi ya mwenyekiti wa ccm mkoani  wa Arusha iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti Marehemu ZELOTHE STEPHEN  ZELOTHE.  Akiongea na vyombo vya habari baada ya zoezi hilo la kurejesha fomu kukamilika katibu wa ccm Mkoa ,Mussa Matoroka alisema kuwa jumla ya wanachama 88 walijitokeza kuchukua fomu lakini waliofanikiwa kurejesha ni 83. Alisema mwitikio ulikuwa mzuri ikiwa ni haki ya msingi ya kila mwanachama wa chama…

Read More

Na Richard Mrusha Mirerani Wafanyakazi wa Kampuni ya wawekezaji wazawa Franone Mining and Games Campany LTD,inayochimba Madini ya Tanzanite eneo la Kitalu C,Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara wamempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania DKT.Samia Suluhu Hassan kwani wameweza kupata ajira tofauti na ilivyokuwa awali. Wakizungumza kwenye mgodi huo hivi karibuni walimshukuru mwekezaji huyo kwa kuwapatia ajira ambapo huko nyuma hawakuwa na kazi ya kufanya kwa ajili ya kuwapatia kipato lakini sasa hivi wamekuwa na uhakika wakujipatia kipato kinachotokana na hiyo kazi.⅕ kwa upande wake Nai leyani ambaye ni kiongozi wa kikundi cha akina mama wanaofanya…

Read More

Na Anangisye Mwateba-Arusha Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeutaka Uongozi na watumishi wa Chuo cha Utalii Kampasi ya Arusha (NCT) kuwa wabunifu katika kuandika maandiko yanayoendana na hali halisi ya biashara ya utalii Duniani, kwani kutakapokuwa na maandiko ya kisasa yanayoshawishi uboreshaji wa biashara ya utalii ndivyo tutakavyo kuza biashara ya utalii na kuongeza mchango wa pato la taifa kutoka katika Chuo cha Utalii Tanzania Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) alipokuwa akiongea na watumishi wa chuo hicho kilichopo maeneo ya Sakina Jijini Arusha Mhe. Kitandula aliongeza kuwa ili chuo hicho kiwe…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Morogoro Waziri wa Elimu, Sayansi na teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema serikali inatambua umuhimu wa Mabaraza ya Wahitimu na Jumuiya mbalimbali katika Vyuo Vikuu, katika kuchangia Maendeleo ya miradi mbalimbali katika Vyuo husika. Prof. Mkenda ametoa kauli hiyo Novemba 22, 2023 mjini Morogoro wakati akihutubia Baraza la Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Mzumbe ambapo amesema serikali inajivunia michango ya Wajumbe wa Baraza hilo, ikiwemo mchango wa ujenzi wa mabweni kwa ajili ya Wanafunzi Ndaki ya Mbeya. “lakini pia nawapongeza kufikia katika hatua za mwisho za kuanzisha mfuko wa ufadhili kwa ajili ya kusaidia wanafunzi wasio na…

Read More

Na Geofrey Stephen.Arusha  Naibu katibu Mkuu ofisi ya Rais Tamiseni anayeshughulikia Afya dkt  Charles Mahera amewataka wakuu wa vyuo vya Afya hapa nchini kuongeza jitihada za kufundisha nidhamu ,wadilifu na hofu ya mungu kwa wahudumu wa afya (Nesi)ambao alidai  wanaongoza kuwa na Lugha mbaya kwa wagonjwa na kusababisha vifo. Dkt Mahera ameyasema hayo jijini Arusha wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa wakuu wa vyuo vya afya vya serikali kutoka mikoa mbalimbali nchini yanayofanyika katika chuo cha Afya cha CEDHA. Naibu waziri alisitiza kuwa ni wajibu wa watoa huduma za afya kuwa na weledi utakaoendana na kasi ya uboreshaji wa…

Read More

Uwekezaji Mkubwa wa Emirates ni Mapinduzi katika Uhandisi wa Ndege. Kwa hatua ya kimapinduzi iliyojikita katika miundo mbinu ya anga, Emirates shirika kubwa la anga la kimataifa, limetangaza mipango ya uwekezaji wa dola za Marekani milioni 950. Uwekezaji huu mkubwa una nia ya kujenga kituo cha uhandisi cha hali ya juu katika Dubai World Central (DWC), katika tasnia ya anga. Eneo la mradi huu linaukubwa wa mita za mraba milioni 1, linawakilisha juhudi kubwa katika sekta ya ndege, na kuimarisha sifa ya Dubai kama kitovu cha teknolojia na huduma za anga za kisasa. Kilichoundwa kwa umakini mkubwa kusaidia ndege za…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv Arusha Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Arusha kimefungua pazia kwa wanachama wake   kuziba nafasi ya mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti wake ZELOTHE STEVEN ZELOTHE baada ya kufariki  Oktoba 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Akiongea na vyombo vya habari katibu wa CCM mkoani Arusha Musa Matoroka alisema kuwa nafasi hiyo kwa sasa ipo wazi na wanachama wa ccm wanapaswa kuchukua fomu zilizoanza kutolewa leo makao makuu ya chama hicho mkoani Arusha kwa ajili ya mchakato wa kuziba pengo hilo.  “Kuanzia jana tarehe 21 fomu za kuwania nafasi ya…

Read More