Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24tv Arusha Chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Arusha kimefungua pazia kwa wanachama wake   kuziba nafasi ya mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mwenyekiti wake ZELOTHE STEVEN ZELOTHE baada ya kufariki  Oktoba 26 mwaka huu jijini Dar es Salaam. Akiongea na vyombo vya habari katibu wa CCM mkoani Arusha Musa Matoroka alisema kuwa nafasi hiyo kwa sasa ipo wazi na wanachama wa ccm wanapaswa kuchukua fomu zilizoanza kutolewa leo makao makuu ya chama hicho mkoani Arusha kwa ajili ya mchakato wa kuziba pengo hilo.  “Kuanzia jana tarehe 21 fomu za kuwania nafasi ya…

Read More

Na Anangisye Mwateba-Moshi Watumishi wa Chuo Cha Viwanda vya Misitu (FITI) wametakiwa kusimamia misingi ya maadili, miongozo na taratibu za kiutumishi ili wawe watumishi bora wenye kuleta tija katika chuo hicho. Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) alipokuwa akiongea na watumishi wa chuo hicho kilichopo katika Manispaa ya Mji wa Moshi mkoani Kilimanjaro. Mhe. Kitandula amewaasa watumishi hao kuacha kutamani mafanikio ya haraka na badala yake kuwa chachu au sehemu ya mafanikio yatakayopatikana chuoni hapo. Amewapongeza watumishi hao waliokitumikia chuo hicho kwa muda mrefu kwa sababu wamekilea na kukitunza chuo hicho. Mheshimiwa Kitandula pia…

Read More

Na John Mhala,Longido Naibu Waziri wa Madini,Dkt Steven Kiruswa na Mbunge wa Jimbo la Longido Mkoani Arusha amewataka Watendaji wote ngazi ya Kitongoji ,Kijiji ,Kata na Wilaya kuhakikisha wanafuatilia na kusimamia utekelezaji wa miradi yote ya Maendeleoa katika wilaya ya Longido Mkoani Arusha ili Serikali iweze kuiamini wilaya hiyo na kuendelea kupeleka fedha za Miradi. Dkt Kiruswa alisema hayo jana wakati akiwa mgeni rasmi katika Harambee ya Ujenzi wa ofisini ya Chama Cha Mapinduzi{CCM} Wilaya ya Longido ambapo awamu ya kwanza zilihitahika shilingi milioni 49  lakini katika harambee hiyo makusanyo yalivuka malengo na kufanikiwa kukusanya shilingi milioni 40.5 fedha taslimu…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omar Kipanga amesema serikali imeendelea kufanya uwekezaji mkubwa katika Taasisi za Elimu ya Juu nyanja ya tehama ili kusaidia kuzalisha wataalam wengi na mahiri watakaosaidia maendeleo ya uchumi wa kidigitali. Mhe. Kipanga ametoa kauli hiyo leo Novemba 17, 2023 jijini Arusha wakati akifungua Maadhimisho ya Miaka 6 ya Kituo cha Umahiri katika TEHAMA Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM AIST), ambapo amesema ustawi wa baadaye wa uchumi wa Afrika utategemea kiwango cha uwekezaji katika sayansi, teknolojia na uvumbuzi. ‘’Suala la ubunifu litaendelea…

Read More