Na Mwandishi wa A24tv Arusha. Serikali imewaagiza waajiri wa Sekta zote nchini kuhakikisha wataalam wanaofanya shughuli za ununuzi na ugavi wanakuwa na sifa sitahiki kama ilivyoainishwa kwenye Sheria Na. 23 ya mwaka 2007 iliyoanzisha Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), pamoja na miongozo inayotolewa. Maagizo hayo yametolewa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), wakati akifungua Kongamano la 14 la Wataalam wa Ununuzi na Ugavi linalofanyika katika ukumbi wa AICC, jijini Arusha. Dkt. Nchemba alisema kuwa anasikitishwa na kuwepo kwa baadhi ya Wataalam wanaofanya kazi pasipo kuwa na sifa stahiki na bila kusajiliwa na Bodi…
Author: Geofrey Stephen
Na Geofrey Stephen Monduli. Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Kilimatinde Wilayani Arumeru Mkoani Arusha na wananchi wa Kijiji cha Moita Bwawani Wilayani Monduli wanamtuhumiwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Moita Bruno Mollel kwa kumega ardhi ya malisho ekari 3,000 kuwa eneo la makazi bila ridhaa ya wananchi. Wakizungumza katika Mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na watu zaidi ya 150 uliofanyika katika Kijiji cha Moita Bwawani walisema na kuiomba serikali kusitisha zoezi hilo kwa kuwa Mwenyekiti Mollel hajali wananchi wenye mifugo kwani eneo hilo lilitengwa kwa ajili ya malisho ya mifugo. Mmoja wa wananchi hao aliyejitambuylisha kwa jina la Ndoipo Mollel maarufu…
Na Mwadishi wa A24tv . Director maarufu wa video mbalimbali ikiwemo za Wasanii wa Bongofleva ambaye pia ni Mtoto wa kwanza wa Muhubiri maarufu wa Arusha wa Kanisa la Ngurumo ya Upako Dr. GeorDavie, Nic Davie maarufu Nisher amefariki saa nane na dakika tisa usiku wa kuamkia leo December 12,2023. Familia ya Dr. GeorDavie imethibitisha kutokea kwa msiba huo wa Kijana wao Nisher na kusema msiba unafanyika katika nyumba ya matamko Kisongo Jijini Arusha na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye. Mwisho .
Na Mwandishi wa A24Tv . Waziri wa Vjwanda na Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji(Mb) ametoa rai kwa vijana wa Tanzania kuendelea kujielimisha na kupata ujuzi mbalimbali ili kuwa tayari kuajiriwa na viwanda mbalimbali vinavyoendelea kujengwa nchini kwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan amewakaribisha wawekezaji mbalimbali kuja kuwekeza nchini hususani katika kujenga viwanda. Ameyasema hayo Desemba 11, 2023 alipotembelea Kiwanda cha Saturn Corporation limited kilichopo Kigamboni Dar es salaam lengo la kuangalia ujenzi unaoendelea katika Kiwanda hicho kinachounganisha magari ya SINOTRUCK aina ya Howo na Tipper “Tuliahidi uko nyuma na Mheshimiwa Rais amesema…
Leo December 12 karibu Arusha24tv kutazama kilicho Andikwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24tv . Mwisho .
Na Richard Mrusha Simanjiro UONGOZI wa Kampuni ya Franone Mining and Games limetd inayojishughulisha na uchimbaji madini ya vito ( Tanzanite) imeungana na watanzania wengine na Serikali katika kuchangia mahitaji mbalimbali ya chakula Kwa wahanga wa mafuriko wilayani Simanjiro mkoani Manyara . Akizungumza na waandishi wa Habari Disemba 10,2023 Meneja Mkuu wa kampuni hiyo Vitus ndakize Amesema kuwa wameguswa sana na tukio hilo hivyo wao kama watanzania waliowekeza kwenye uchimbaji wa madini na wao wameona wachangie watanzania wenzao ambao wamepatwa na majanga hayo Kwa kutoa bidhaa mbalimbali. Amesema miongoni mwa vitu ambavyo wamechangia na kukabidhi Kwa mkuu wa Wilaya Dkt.…
Karibu Arusha24Tv leo December 11 kutazama kilicho Andikwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24tv . Mwisho.
Na John Mhala,Monduli Mfanyabiashara Maarufu wa Madini ya Tanzanite Mkoani Arusha,Sanare Mollel maarufu kwa jina la Muller mkazi wa Kijiji cha Moita Bwawani kata ya Moita Bwawani wilayani Monduli Mkoani Arusha anatuhumiwa kuwapiga na kuwajeruhi wananchi na wafanyakazi wa idara ya ardhi Halmashauri ya Monduli na kuwatishia kwa silaha aina ya bastola kwa hatua yao ya kwenda katika Kijiji hicho na kupima ardhi ya eneo la malisho ekari 7000 kuwa eneo la makazi bila lidhaa ya wananchi. Akizungumza na waandishi wa habari,Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} Kata ya Moita Bwawani Loseriani Loibanguti Kimbele alisema kuwa Mulle aliamua kufanya hivyo na…
Na Richard Mrusha Dodoma. MAKAMU wa Rais Dkt. Philip leo Desemba 10,2023 akiwa katika Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege Jijini Dodoma ambako ameshiriki Ibada ya jumapili ameitaka Mitandao ya kijamii Nchini itumike vizuri pasipo kupotosha Umma. Dkt. Mpango ameongeza kuwa mitandao ya kijamii ni mizuri na ni mibaya hasa ikitumika vibaya inapotosha Umma na kutumia nafasi hiyo kuwataka isitumike vibaya. “Ahsanteni sana kwa kuniombea yamesemwa mengi na wengine wamesema mimi ni mzuka, zaburi ya 118 aya ya 17 inasema sitakufa bali nitaishi na kuyasimlia matendo makuu ya MUNGU kwa hiyo Mitandao ni mizuri lakini…
Karibu Arusha 24Tv leo December 10 kutazama kilicho Andikwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24tv . Mwisho