Author: Geofrey Stephen

Na Richard Mrusha Dodoma AFISA Utumishi wa Chama cha walimu Taifa CWT Neema Ezekia Amesema maadhimsho ya siku ya walimu Duniani Kwa utaratibu wa Chama hicho taifa yanafanyika kila baada ya miaka minne na mwaka huu yalikuwa yafanyike Novemba 4,2023 Kwa ratiba iliyokuwa imepangwa. Amesema kuwa maadhimisho ambayo yamefanyika katika ngazi za Wilaya ni Kwa utaratibu ukizingatia siku hiyo ni siku ya walimu Duniani lakini kitaifa lazima yaadhimishwe kitaifa na yaratibiwe na ngazi ya juu ya Chama hicho. Neema ameyasema hayo Disemban 8 ,2023 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari na kutolea ufafanuzi kuhusu Malalamiko na shutuma zinazoletwa…

Read More

Na Ahmed Mahmoud Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha kimepongeza waandaaji wa mbio za Mount Meru Marathon Kwa kujitolea vifaa mbalimbali kusaidia Uzazi Salama kwa wakinamama wasio na uwezo wa kununua vifaa vya kujifungulia. Akiongea Mara baada ya kuwakabidhi vifaa hivyo katika hospitali ya Rufaa ya Mount Meru na kuzindua Bonanza hilo la kesho katika viwanja vya Ngarenaro Katibu wa itikadi na Uenezi Mkoa wa Arusha Saipulan Ramsey Jijini Arusha amesema Mount Meru Marathon imeonyesha kuunga Ilani ya CCM. Amesema katika Ilani yao ukurasa wa Tano inaeleza kuimarisha huduma za mama na mtoto na niwapingeze kwa kugusa ibara ya 8…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha. Wahitimu wa Taaluma mbalimbali nchini wameshauriwa kutowekeza katika maarifa ya darasani Pekee kwenye kutekeleza majukumu yao badala yake kuwa na utashi utakao wawezesha kubadili mitazamo hasi ya Jamii na hivyo kutokuwa chanzo Cha mitafaruku katika maeneonyao ya kazi . Hayo yamebainishwa katika mahafali ya Saba ya Chuo kikuu Cha Mtakatifu Agustino Tawi la Arusha. Ambapo Askofu wa Jimbo kuu katoliki la Singida EDWARD MAPUNDA Akiwatunuku Astashahada,  Stashahada na Shahada ambao  wanafunzi wa fani mbali mbali chuoni hapo. Amesema kwamba wanafunzi walio pata elimu chuoni hapo wanapaswa kuepuka athari  zitokanazo na kasumba ya waajiri na wanataaluma kuzingatia…

Read More

Na Geofrey  Stephen Arusha Benki ya CRDB imezindua Matumizi ya Kadi ya American Express moja ya kampuni kubwa za huduma za malipo duniani katika mtandao wa Benki CRDB mkoani Arusha. Akizindua Matumizi hayo Mkuu wa mkoa wa Arusha bw.John Mongela alisema kuwa mfumo wa malipo ni moyo wa uchumi wowote ule kote duniani na ufanisi wake ni muhimu kwa maendeleo endelevu. Alisema kuwa Miundombinu imara ya malipo inarahisisha sio inawezesha kufanyika kwa miamala bali pia inachochea ukuaji wa kiuchumi, na inaongeza ujumuishi wa kiuchumi kwa Wananchi. “Katika uchumi wa dunia ya leo unaoendelea haraka, ambapo teknolojia ya kidijitali imeshika hatamu,…

Read More

Na Mwandishi wetu Dodoma na Halle- Ujerumani Wizara ya Madini imepata fursa muhimu ya kutangaza Madini ya Lithium na Madini mengine Mkakati ambayo nchi imebarikiwa kuwa nayo katika Kongamano la LithiumDays23 linalofanyika kila mwaka mjini Halle nchini Ujerumani. Katika kongamano hilo, Tanzania imepewa heshima ya kushiriki kwa njia ya mtandao na ana kwa ana ambapo Mkurugenzi wa Sera na Mipango Wizara ya Madini Augustine Olal kwa niaba ya Katibu Mkuu amewaongoza Wataalamu wa Wizara kushiriki kwa njia ya mtandao kutoka Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma. Aidha, katika kongamano hilo, Tanzania imepata nafasi muhimu ya kujitangaza kama nchi ijayo mshirika…

Read More