Na Geofrey Stephen Arusha . Thomas Loy Ole Sabaya amechaguliwa kwa kishindo kua Mwenyekiti Mpya wa chama hicho Mkoa kwa kupata idadi kura 463 huku mpinzani wake wa karibu Daniel Palagyo akipata kura 374 kati ya kura 951 huku Moja ikiharibika. Uchaguzi huo umekuja kufuatia kifo cha aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Arusha Marehemu Zelothe Stephen aliyefariki octoba 26 Jijini Dar es salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. Akiongea mara baada ya kuchaguliwa Sabaya amewashukuru sana wajumbe akisema CCM hii ndio domokrasia maana kijana wangu amenikimbiza na kuonyesha ukomavu hivyo nitashirikiana na Wanachama wote kuanzia ngazi ya kitongoji kuhakikisha Mradi…
Author: Geofrey Stephen
Leo tarehe 4 Mwezi December karibu Kutazama kilicho Andikwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania mbele ne nyuma Hìi ni A24tv . Mwisho .
Jumapili ya leo December 3 karibu Arusha24tv kutazama kilicho Andikwa katika magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24Tv . Mwisho .
Na Mwandishi wa A24tv . Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Serikali inawatarajia Wahitimu katika mafunzo ya elimu kuwa mabalozi wa utekelezaji wa Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014 Toleo la 2023. Prof. Mkenda ametoa rai hiyo Disemba Mosi, 2023, Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakati akizungumza kwenye mahafali ya 31 ya Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM). “Katika kipindi hiki, tunawategemea sana kwenda kutusaidia kutekeleza mageuzi ambayo yameanishwa katika Sera mpya ya Elimu, pamoja na jukumu la kufundisha mtaenda kusimamia mabadiliko ya elimu nchini” Alisema Prof. Mkenda. Amesema Serikali imeanza mchakato wa…
Na mwandishi wetu Arusha. Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), imewataka wafanyabiashara kuhakikisha kuwa wanasajili logo zao kabla ya kuanza kuzitumia ili kuepuka usumbufu wa kuibiwa logo na wafanyabiashara wengine na kisha kujikuta katika mgogoro wa kibiashara. Afisa Usajili wa BRELA Bi. Julieth Kiwelu ameeleza hayo Desemba,1, 2023, Maafisa hao walipowatembelea baadhi ya wafanyabiashara wa jijini Arusha ili kujua changamoto wanazozipata wakati wa kupata huduma mbalimbali za Taasisi kwa lengo la kuzipatia ufumbuzi. Wakiwa katika Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO), Bi. Kiwelu amesema pamoja na kwamba huduma zote za BRELA zinatolewa kwa njia ya mtandao, bado kuna…
Karibu Arusha24Tv leo December 2 kutazama kilicho Andikwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24tv . Mwisho .
Na Mwandishi wa A24tv . Katibu Mkuu Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Mhandisi Zenna Ahmed Said, ametoa wito kwa wanawake wote wanaojihusisha na biashara kushiriki Kongamano la Pili la Wanawake katika Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (AfCFTA) linalotarajiwa kufanyika tarehe 06 hadi 08 Disemba, 2023 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam. Katibu Mkuu Kiongozi huyo amayasema hayo Novemba 30,2023 akiwa katika kikao cha maandalizi ya Kongamano hilo ambalo Tanzania ni mwenyeji na linaandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kushirikiana na Sekretarieti ya…
Doreen Aloyce, Dodoma Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara (Mb) Exaud Kigahe amesema Serikali kwa kushirikiana na Halmashauri zote nchini ipo tayari kuwasaidia wafanyabiashara na wajasiliamali katika nyanja mbalimbali ili waweze kutimiza ndoto zao za kiuwekezaji na kibiashara. Mheshimiwa Kigahe ameyasema hayo ,Disemba Mosi Mwaka 2023 Jijini Dodoma wakati akifungua Kongamano la Biashara na Uwekezaji la Jiongeze lililoandaliwa na Wasafi Media. Aidha amesema katika kutatua changamoto hiyo Serikali imeanzisha kitengo kamili kinachoshughulikia maswala ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara katika kila Halmashauri kote nchini. Sanjari na hilo,amebainisha,kuwa Serikali imeanzisha Dirisha la Kielektroniki la Kuwahudumia Wawekezaji mahala pamoja (Tanzania Electronic Investment Window)…
Na Mwandishi wa A24Tv . WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amebainisha kuwa, elimu inayotolewa kupitia masomo ya dini ni tofauti na ile ya masomo mengine kwani elimu hiyo inahusisha masuala ya imani na hugusa zaidi hisia. Prof. Mkenda alisema hayo Novemba 30, 2023 katika uzinduzi wa Tanzania Islamic Studies Teaching Association (TISTA) pamoja na makabidhiano ya muhtasari na kitabu cha kwanza cha mwanafunzi cha Elimu ya dini ya Kiislamu, tukio lililofanyika katika ukumbi wa Mfalme Mohamed BAKWATA makao makuu Kinondoni Dar es Salaam. “Mitaala ya dini ni ya kipekee, ni tofauti na mitaala ya somo la…
December 1. Tunakaribisha kutazama kilicho Andikwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24tv . Mwisho