Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen SHIRIKA lisilo la kiserikali la Mimutie Women Organization limeiomba serikali kuchukua hatua kali kwa mashirika yasiyo ya kiserikali yanayochochea migogoro ya ardhi wilayani Ngorongoro mkoani Arusha . Aidha shirika hilo limeiomba serikali kukaa meza moja na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, NGO’s na Wananchi waishio wilayani humo kujadili mgogoro usiokoma wa mipaka ambao unaendelea kuwaumiza jamii ya kifugaji hasa wanawake na watoto Mkurugenzi wa shirika hilo, Rose Njiro alisema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jijini Arusha na kusema kuwa serikali inapaswa kuchukua hatua kali kwa NGO’s Pamoja na wanasiasa wakiwemo madiwani ambao wamekua ni changamoto kuzikichochea migogoro ya…

Read More

Na. WAF – Dodoma Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu leo Oktoba 23, 2023 amezindua rasmi bodi mpya ya ushauri ya Wizara ya Afya (MAB) kwa Mamlaka ya Dawa na Vifaa Tiba (TMDA) ambayo inawajumbe Saba. Waziri Ummy wakati akizindua bodi hiyo mpya amewataka wajumbe hao kuimarisha usimamizi wa TMDA katika upande wa dawa, vifaa na vifaa tiba ili kusiwepo na upotevu wa aina yoyote wa vifaa tiba hivyo. “Kazi kubwa mnayotakiwa kufanya ni ufuatiliaji wa mara kwa mara wa bidhaa duni na bandia zinazoingia kwenye soko ili zisiwafikie wananchi wakazitumia”. Amesema Waziri Ummy Lakini pia wakati akifungua bodi hiyo…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Arusha Kishindo cha wiki ya Asasi za Kiraia (AZAKI) yaanza kunguruma Jijini Arusha mapema leo  ikiwa na wadau wa kutosha  na  kuanza kuamasisha jamii kupokea mabadiliko ya  teknolojia na kutumia katika kunufaisha jamii . Mkurugenzi  wa Foundation for Civil Society Francis Kiwanga akiongea katika mkutano huo amesema kuna kila namna kukubali teknolojia katika kutambua changa moto zake na faida zake ambazo zimekua chachu ya maendeleo kwa watanzania na jamii kubwa Duniani Mkurugenzi Mtendaji wa Foundation for Civil Society Francis Kiwanga akizungumza na vyombo vya habari katika ukumbi wa simba Aicc  Mada nyingine ni ujumuishwaji na uwezashaji…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv Vijana wa familia za wakazi wa Vijiji vilivyoshamiri kwa kilimo cha bangi mkoani Arusha vya Kisimiri na Lesinoni wilayani Arumeru wametakiwa kuondokana na imani potofu ya kwamba bangi ndiyo kilimo kinachoweza kuwanyanyua kiuchumi kwa kuwapatia kipato cha kumudu mahitaji yao ya lazima yakiweo ada ya masomo. Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Nchi(DCEA) imelazimika kuendesha elimu juu ya madhara ya matumizi na biashara ya Dawa za Kulevya kwa wanafunzi 1,141 na walimu 45 pamoja na baadhi ya viongozi wa vijiji hivyo. Elimu kwa kundi hilo la vijana imekuja baada ya Mamlaka ya Kudhibiti…

Read More

Na Geofrey Stepehen Arusha Naibu Waziri wa Uchukuzi David kihenzile aridhishwa na maendeleo, usimamizi na maboresho yanayoendelea kwenye uwanja wa ndege wa Arusha ikiwemo jengo jipya la abiria na sehemu ya kuruka na kutua ndege. Akizungumza Jijini Arusha wakati wa muendelezo wa ziara zake za kuongea na Uongozi na Kukagua Miradi ya maendeleo inayotekelezwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Viwanja vya ndege Tanzania(TAA) amesema Tanzania ni ya pili Kwa kuwa na vivutio vingi vya utalii duniani ambapo asilimia 80 ya watalii hupita kaskazini huku Arusha ikitumika kama lango hivyo ukilishwaji wa Run way yenye mita 1880 Toka 1680 za awali…

Read More

Geofrey Stephen Hai. Kamati ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imekipongeza Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) Kampasi ya Kikuletwa  ilioko Hai Mkoani Kilimanjaro kwa hatua nzuri ya ujenzi wa majengo matatu yaliyopo Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro ambayo yanatarajiwa kuwa kituo cha umahiri katika nishati jadidifu. Pongezi hizo zimetolewa wilayani humo na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo,Husna Sekiboko kwaniaba ya wabunge wa kamati hiyo walipotembelea kampasi hiyo ili kukagua maendeleo ya ujenzi wa majengo yanayotarajia kukamilika Januari 15,2024 . Majengo hayo yanayogharimu dola za kimarekani 16,250,000.00 zilizotolewana Benki ya Dunia (WB)…

Read More

Na Richard Mrusha NAIBU Waziri wa madini Dkt.Steven Kiruswa amefungua mkutano wa siku tatu wa wakandarasi waliowekeza katika madini yanayopatikana chini ya sakafu ya bahari kuu 2023 na utajadili agenda mbalimbali kuhusu masuala ya utafiti ,uchimbaji ,na utunzaji wa Mazingira yaliyo chini ya sakafu ya bahari kuu. Amesema mkutano huo ni kuendelea na utekelezaji wa Article 145 kwenye UNCLOS 1982 na makubaliano ya mwaka 1994 kuhusu shughuli za uchimbaji wa madini kwenye sakafu ya bahari. DKT Kiruswa ameyasema haya leo octoba 22, 2023 jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano huo ambapo Amesema pamoja na kuwa nchi wanachama wa umoja…

Read More

Na Geofrey Steohen Arusha. Taasisi mbalimbali za kiraia zinatarajia kukutana jijini Arusha kwa kujadili na kutatua changamoto mbalimbali zinazoathiri mifumo ya techenolojia kwa lengo la kuimarisha na kuboresha SEKTA hiyo. Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi wa kituo cha sheria na Haki za binadamu Dkt Anna Henga amesema changamoto inayowaathiri wananchi ni pamoja na kukosekana  kwa mtandao hasa vijini na kukatika kwa umeme mara kwa mara. Na hiyo upelekea jamii kubwa kukosa mawasiliano jambo ambalo linarusha nyuma maendeleo hususani katika kuwasikiana na kuwasilisha changamoto zinazo wakabili kwa kukosa mawasiliano muhimu ya kidigital Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya wiki…

Read More