Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi waA24Rv Dubai, Oktoba 2023 Shirika la Ndege la Emirates linachukua hatua kubwa katika ahadi yake ya uhifadhi wa mazingira na uhifadhi wa wanyama pori kwa kuwasilisha vifaa vya huduma vipya na bure kwa abiria wake wa madaraja ya Premium Economy na Economy katika safari ndefu ulimwenguni. vifaa hivi vya huduma vitakavyopatikana kwenye ndege ni matokeo ya ushirikiano wa pekee na umoja wa wanyamapori, ilioundwa kutoa ufahamu juu ya baadhi ya spishi za wanyama zilizo hatari kupotea zaidi duniani. Uhifadhi wa wanyama pori na mazingira ya asilia umekuwa moyoni mwa Mfumo wa Uhifadhi wa Mazingira wa Emirates kwa muda…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha KIKAO kazi cha Watendaji Wakuu wa Mahakama kutoka   Nchi za Kusini Mwa  Mashariki ya  Afrika (SEAJAA) kitafanyika Oktoba 22, 2023 Jijini Arusha Kikao kazi hicho kitakua na mada mbali mbali ambazo zitawasilishwa ni pamoja  na ajenda za marekebisho ya katiba ya chama hicho ikiwemo uboreshaji wa vyanzo vya fedha, uboreshaji wa mtandao wa chama hicho, Madazingine ambazo zitajadiliwa katika kikao kazi hicho ni pamoja na maswala ya fedha huku nchi 13 za umoja huo zitakazoshiriki mkutano huo ni pamoja  Angola, Botswana, Lesotho, Zanzibar, Shelisheli, Zimbabwe, Malawi, Msumbiji, Eswatini, Zambia, Namibia na mwenyeji Tanzania. Akiongea na mapema…

Read More

 Na Geofrey Stephen ARUSHA  Wakati Taifa likiadhimisha siku ya mwanamke anayeishi kijijini yanayofanyika  kila mwaka oktoba 15 ,mkazi wa kijiji cha Misigiyo wilayani Ngorongoro Mkoa wa Arusha,Veronica Makutiani(29) mambo yamekuwa tofauti ambapo mwanamke huyo. amenusurika kuuawa kikatili kwa kipigo cha baba yake mzazi wakishirikiana na kaka yake kiasi cha ujauzito wake kutoka, wakimlazimisha kurejea kwa  mume wake katili aliyekuwa akimtesa kwa kipigo na kumlaza njaa yeye na watoto wake wawili. Akisimilia mkasa huo kwa uchungu huku akibubujikwa na machozi akiwa amehifadhiwa kwa msamalia mwema Rose Njilo anayefanyakazi shirika la MIMUTIE WOMEN ORGANIZATION la jijini Arusha alisema haamini kama mzazi wake…

Read More

Na. Mwandishi wetu-Dar es salaam Wanafunzi wa chuo cha Taifa cha Utalii nchini Tanzania (NCT) wanatarajiwa kuanza kufanya mazoezi ya utendaji kazi katika nchi za Denmark, Norway, Ujerumani na Sweden. Haya yamebainishwa na Mkuu wa Chuo hicho, Dkt. Florian Mtey baada ya kutembelewa na Mkurugenzi Mkuu wa kampuni ya Bixter.work, Bi. Nataliya Jorgensen na Mkuu wa Kituo cha SUGECO Bw. Revocatus Kimario ofisini kwake jijini Dar es salaam. Dkt. Mtey amebainisha kwamba fursa hii ambayo wanafunzi wa chuo hicho cha Utalii wanaenda kuipata italeta tija katika fani ya ukarimu kwa vile kwa sasa soko la utalii nchini limekuwa kubwa kutokana…

Read More

Na mwandishi wetu Dodoma Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeishauri Serikali kuweka kipaumbele katika kusambaza Vituo vya Nishati ya Gesi Iliyoshindiliwa (CNG) inayotumika katika kuendesha mitambo na magari nchini ili kukabiliana na changamoto za upatikanaji wa mafuta pale zinapotokea. Ushauri huo umetolewa leo Oktoba 18, 2023 jijini Dodoma na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Mhe. Mathayo David wakati Kamati hiyo ilipopokea taarifa ya Wizara ya Nishati, kuhusu hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi wa kuanzisha vituo hivyo. “Tunashauri Serikali iweke kipaumbele katika matumizi ya gesi asilia katika maeneo mbalimbali nchini…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Shule yenye mchepuo wa kiingereza ya Tanganyika School iliyopo Njiro jijini Arusha imewaliza wazazi na kuwaacha katika mataa mara baada ya kukusanya mamilioni ya fedha kwa  kujihusisha na utoaji wa huduma  ya Bima ya Afya kwa wanafunzi kinyume cha sheria bila kusajiliwa na kukusanya sh,milioni 207.6 kwa kipindi cha miaka 10 kuanzia mwaka 2014. Akiongea na vyombo vya habari jijini Arusha Kamishna wa Bima nchini Dkt Baghayo Saqware alisema kuwa shule hiyo imekuwa ikiendesha huduma hiyo kwa kutoza ada ya Bima ya afya ya sh,200,000 kwa mwaka kwa kila mwanafunzi wa shule ya msingi na sekondari…

Read More

Na Geofrey Stephen  Arusha    MAMLAKA ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya Nchini (DCEA) imesaini mkataba wa ushirikiano kati ya Serikali na Sekta binafsi Katika kudhibiti uchepushwaji wa kemikali  bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya ikiwa ni hatua ya kupanua wigo wa kudhibiti ongezeko la dawa hizo Nchini.   Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kukevya (DCEA) Aretas Lyimo alisema kundi la vijana wasomi wa vyuo vikuu ndio linaloongoza kwa matumizi makubwa ya dawa za kulevya ikiwemo uchepushwaji wa kemilaki bashirifu na dawa tiba zenye asili ya kulevya.   Lakini pia…

Read More