Author: Geofrey Stephen

Na Richard Mrusha Kampuni ya SUMAJKT Bottling co. Ltd, inayozalisha maji ya Uhuru Peak Pure Drinking Water, imezindua mikondo miwili ya uzalishaji maji na Muonekano mpya wa chupa za maji ya Uhuru Peak, Akizungumza Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Jenerali CDF Jacob John Mkunda wakati wa uzinduzi wa mikondo miwili ya uzalishaji maji, amesema Serikali ina matarajio makubwa na Jeshi la kujenga Taifa JKT na Jeshi la wananchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatambua na kutembea kifua mbele kutokana na mchango mkubwa unaotokana na shughuli wazifanyazo jeshi hilo hasa katika swala zima la malezi kwa vijana. Jenerali…

Read More

Mwandishi wetu.Babati. Timu 12 za soka la Wanawake na wanaume zimetinga hatua ya robo fainali ya michuano ya chemchem CUP 2023 baada ya kuongoza katika michezo katika Kanda tatu. Timu hizo ni timu za soka za wakubwa ,Timu za vijana na Timu za Wanawake wa soka ambapo kwa mara ya kwanza zimeshiriki michuano hii ambayo ilikuwa inashirikisha jumla ya timu 31. Michuano wa chemchem ambayo mwaka huu inagharimu zaidi ya sh 100 milioni inadhaminiwa na Taasisi ya chemchem ambayo imewekeza shughuli za Utalii na uhifadhi katika eneo la hifadhi ya Jamii ya wanyamapori Burunge wilayani Babati. Katibu wa chemchem CUP,John…

Read More

Na Geofrey Stepben . Eneo la Hifadhi ya Ngorongoro limetangazwa kuwa mshindi katika kipengele cha kivutio bora cha utalii barani Africa (African leading tourist Attractions) na kupewa tuzo na mtandao wa _World travel awards_. Tuzo hiyo imetolewa usiku huu wa tarehe 15 Oktoba, 2023 katika hotel ya _Atlantis The Royal Dubai _ katika nchi za Falme za Kiarabu ambapo Ngorongoro imeshinda tuzo hiyo baada ya kushinda vivutio vingine vya utalii barani Afrika ambavyo ni table Mountain, Hartbeespoort aerial cableway, V& A Waterfront, Ruben Island vya afrika kusini, Ziwa Malawi, Okavango Delta ya Botswana, Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na Pyramis of…

Read More

Na Kassim Nyaki, NCAA Serikali kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) inaendelea na zoezi la uandikishaji wa wananchi wa Tarafa ya Ngorongoro ambao wameunga mkono jitihada za Serikali kuboresha maisha yao ambayo kwa miaka mingi wamekosa fursa mbalimbali za kimaendeleo kwa kuishi ndani ya eneo la Hifadhi ya Ngorongoro. Kwa mujibu wa Kamishna Msaidizi Mwandamizi Mdala Edson Fedes ambae ni meneja mradi huo amebainisha kuwa katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wa zoezi hilo jumla ya kaya 551 zenye watu 3,010 na mifugo 15,321 ziliandikishwa, kuthaminishwa na kuhamishwa ndani ya Hifadhi. Aidha, katika awamu ya pili ya utekelezaji wa…

Read More

Na Richard Mrusha Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Kitaifa mwaka 2023, Abdalla Shaib Kaim, amempongeza Mbunge wa jimbo Kiteto Mkoani Manyara Edward Ole Lekaita kwa kushiriki Kikamilifu kwenye shughuli ya Kitaifa za kuupokea na kukimbiza mwenge wa uhuru ulipokua Wilayani Kiteto hadi kukabidhiwa kwake katika Wilaya ya Simanjiro. Kaimu ameyasema hayo Jana wakati alipokua akiagana na wananchi na viongozi wa Wilaya ya Kiteto kuingia Wilaya ya Simanjiro ambapo amesema kitendo cha Mbunge Lekaita kushiriki shughuli ya Kitaifa sio tu kuuenzi Mwenge wa uhuru bali ni kumuenzi Baba wa Taifa Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere. “Mhe Mbunge Ole Lekaita nakupongeza…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha WAKUU wa Idara za Utawala na Rasilimali watu Katika Utumishi wa Umma, wameelezwa  Moja wapo ya sifa ya Utumishi uliotukuka ni kujifunza na kusikiliza changamoto za watumishi waliopo chini yao na kuzitatua badala ya kukumbilia kufanya mabadiliko makubwa  ya haraka kwenye taasisi walizopangiwa au kuhamishwa. Hayo yameelezwa Oktoba 13 na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Katiba na Sheria Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Haroun Ali Suleimani,alipokuwa akifunga kikao kazi kilichodumu kwa  siku tatu kwenye Ukumbi wa mikutano ya kimataifa,AICC Jijini Arusha. Watumishi wanapewa vyeo watambue kuwa wameongezewa majukumu na sio upendeleo. Amesema…

Read More

Na Richard Mrusha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha wananchi waliopo kwenye vitongoji wanapatiwa umeme ili kuharakisha maendeleo yao kiuchumi. Mhe. Dkt. Biteko ameyasema hayo alipokuwa akiwasha umeme kwenye Kijiji cha Ndalibo, Kata ya Mtanana Wilaya ya Kongwa sambamba na kuzindua kisima cha maji ambacho kitakuwa kikitumia umeme kwa manufaa ya wananchi wa eneo hilo. “Ndugu zangu niwahakikishie, Mhe. Rais Dkt. Samia anapambana usiku na mchana kuhakikisha umeme unapatikana na kuinua hali za maisha ya wananchi waliopo vijijini kwani umeme sio anasa…

Read More