Author: Geofrey Stephen

Na Mwandoshi wa A24Tv Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda amesema Vyuo vikuu havipimwi kwa wingi wa wanafunzi na mapato badala yake tafiti inazofanya zenye kuleta gunduzi, kukuza maarifa na ujuzi katika jamii. Prof. Mkenda amesema hayo jijini Dodoma wakati akizindua Baraza jipya la Chuo Kikuu Huria cha Tanzania na kutoa wito kwa Vyuo vikuu kuzingatia ufanyaji wa tafiti zenye tija nchini ili kuchochea ushindani katika gunduzi mbalimbali ndani na nje ya nchi “Vyuo vikuu havipimwi kwa wingi wa wanafunzi na wingi wa mapato, kuna vipengele vingi vya upimaji ubora wa elimu ya chuo kikuu mojawapo ni…

Read More

Na Geofrey Stephen  Arusha  WANAWAKE wameshauriwa kuondoa mfumo tegemezi unaowarudisha nyuma kinaendeleo, badala yake wajenge tabia ya udhubutu itakayosaidia kuwaimarisha kiuchumi ndani ya familia zao na taifa kwa ujumla. Rai hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya mstaafu BETH MKWASA wakati alipohudhulia maadhimisho ya kila mwezi ya  kusemezana kwa wanawake wakatoliki Tanzania (WAWATA) wa jimbo kuu katoliki la Arusha  yaliyofanyika katika Parokia ya Moyo Safi wa Bikra Maria,Ungalimited jijini Arusha. Mkwasa ambaye kwa sasa ni mfanyabiashara na mwandishi wa habari Mwandamizi mstaafu, alisema Tanzania imejaliwa kuwa na wanawake  wengi wenye nguvu na taifa linawategemea, lakini wengi wao bado wanaishi kwa mfumo…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv-Arusha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii ,Mhe. Dunstan Kitandula(Mb) amesema ili kupambana na uhalifu wa wanyamapori kunahitaji ushirikiano, kuchangia rasilimali fedha na kupashana habari pamojag na kuwa na operesheni za pamoja kikanda Hayo ameyasema wakati akifungua mafunzo kwa Wahifadhi Wanyamapori kutoka katika nchi za Afrika na Asia ambao wamekutana Jijini Arusha kwa lengo la kupeana uzoefu juu ya mbinu mpya na bora za kupambana na changamoto ya ujangili na usafirishaji haramu wa Nyara zitokanazo na wanyamapori na misitu. Mhe. Kitandula aliongeza kuwa wahifadhi wanyamapori wanatakiwa kutambua kuwa utekelezaji wa sheria za wanyamapori kwa ushirikiano ni muhimu…

Read More

Bertha Mollel, Kilimanjaro Zaidi ya wanafunzi 1000 kutoka shule tisa za Arusha na Kilimanjaro wamefanikiwa kupewa misaada ya viti, meza , madawati na vitanda vyote vikiwa na thamani ya shilingi 107.7. Misaada hiyo iliyotolewa na Benki ya NMB, ni pamoja na viti na meza 400, madawati 100 pamoja na vitanda 160 katika shule tatu za msingi, na sita za Sekondari. NMB imetoa misaada hiyo ikiwa ni katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja duniani iliyoanza octoba 2 na itafikia tamati kesho jumapili octoba 8, 2023. Shule za Sekondari zilizopata msaada wa viti na meza kwa upande wa Kilimanjaro ni pamoja…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv . Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko leo Oktoba 8, 2023 ameondoka nchini kuelekea nchini Uganda kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho ya Sherehe za Miaka 61 ya Uhuru wa nchi hiyo. Maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Oktoba 9, 2023 nchini humo Mwisho.

Read More

Na Mwandishi wetu, Arusha . Arusha .Wanafunzi wa shule ya sekondari Oldadai iliyopo kata ya sokon 11 wilayani Arumeru mkoani Arusha wanatarajiwa kuondokana na adha ya maji iliyokuwa ikiwakabili muda  mrefu baada ya kupata ufadhili wa ujenzi wa kisima cha maji  kutoka shirika la Worldserve International Tanzania . Aidha wanafunzi hao walikuwa wakitembea umbali mrefu na wakati mwingine  kupitwa na vipindi vya masomo kwa ajili ya kufuata maji hayo ambayo hayakuwa salama kwa afya zao . Mkuu wa shule hiyo, Loishiye Sironga aliyasema hayo mkoani  Arusha wakati akizungumza katika mahafali ya 31 ya kidato cha nne shuleni hapo  ambapo…

Read More