Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen -ARUSHA Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Paul Christian Makonda ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania [TRA] ,mkoa wa Arusha pamoja na Halmashauri zinazounda mkoa huo kuendelea kufanya kazi kwa ukaribu na wafanyabiashara wa Mkoa huo na kujiepusha na bughudha za ukusanyaji kwa wafanyabiashara. Makonda amebainisha hayo Usiku wa Ijumaa, Februari 21, 2025 kwenye Tuzo za Mlipakodi bora wa mwaka 2023/24 mkoa wa Arusha, Hafla iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mount Meru Jijini Arusha, akiipongeza TRA pia kwa kuendelea kupunguza malalamiko ya kikodi kutoka kwa wafanyabiashara. Katika sehemu ya Hotuba yake Makonda kando ya kuipongeza Halmashauri ya Jiji la…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . MAMLAKA ya hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), imepanga kuadhimisha siku ya Wanawake Duniani, 8 Machi 2025 inayofanyika kitaifa Mkoani Arusha,kwa kupeleka wanawake zaidi ya 800 katika hifadhi zake ili kujionea vivutio mbalimbali. Lengo la kutembelea hifadhi ni kujionea vivutio vingi vilivyoko katika hifadhi hiyo pia ni kujionea kazi kubwa iliyofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza utalii kupitia filamu za Royal Tour na Amazing Tanzania. Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo Februari 22, 2025 Kamishna msaidizi wa Uhifadhi NCAA, Mariam Kobelo alisema safari hiyo itafanyika Mach 7th, 2025 siku moja kuelekea kwenye kilele cha siku…

Read More

Na Mwandishi Wetu WAZIRI wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Jerry Silaa ameeleza kwamba sheria ambayo ilitumiwa na serikali kuishurutisha kampuni ya simu ya Vodacom kusajili asilimia 25 ya hisa zake katika Soko la Hisa Dar es Salaam DSE imekuwa na matokeo mabaya. Slaa ambaye alikuwa akizungumza katika kikao kazi cha serikali na wadau wa sekta mawasiliano alisema njia bora ya kukuza sekta yoyote katika zama za uchumi wa soko huria ni kuacha nguvu ya soko itawale badala ya shuruti. Akifafanua, Silaa alisema kwa kawaida makampuni hujisajili katika masoko ya hisa kama njia ya kuongeza mitaji, ingawa tofauti na ilivyokuwa…

Read More

Siha ,Mganga Mkuu wa hospital ya wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Paschal mbotta,ametoa shukurani kwa Jumuiya ya maridhiano na amani Tanzania (JMAT), Wilayani humo kwa kuona umuhimu wa kukusanya damu vijiji kwa ajili ya wagonjwa wanaofika hospital hapo wakiwamo kina mama wajawazito Haya yemesemwa katika hitimisho ya maridhiano day katika hospital ya Wilaya hiyo, ambapo shughuli mbali mbali zimefanyika ikiwamo kupanda miti, utoaji wa damu na kuwatembea wagonjwa sambamba na kufanya maombi ibada ya kuwaombea wagonjwa Akizungumza na Viongozi Jumuiya hiyo ngazi ya kata , Wilaya na mkoani katika ukumbi wa hospital hiyo , amesema kitendo walichokifanya ni cha kuokoa…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . SERIKALI imemsomea mashtaka 60 ya uhujumu uchumi ,mfanyabiashara na mwekezaji Saleh Salimu Alamry (54) Mkazi wa Njiro Jijini Arusha akikabiliwa na mashtaka ya kuongoza genge la uhalifu, kughushi na utakatishaji fedha haramu kiasi cha dola za kimarekani milioni 8 akiwa mkurugenzi mwenza wa kampuni mbili za uwindaji na utalii ya Sunset Tarangire limited na AIrajhi Holdings LTD. Mwingine aliyesomewa mashtaka ni wakili wa kujitengemea Sheck Mfinanga ambaye anakabiliwa na mashtaka ya kughushi na kuwasilisha nyaraka za uongo. Akisoma mashtaka hayo leo februari 20,2025  mbele ya hakimu mfawidhi wa mahakama ya  hakimu Mkazi Arusha,Erasto Philly ,wakili…

Read More

Siha, Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT),Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Idrisa Mndeme ,amesisitiza Wananchi kata ya SanyaJuu ,kuunda vikundi vya ulinzi shirikishi katika maeneo yao kwa lengo la kukabiliana na vitendo vya uhalifu Ametoa kauli hiyo February 18 2025, kutoka wezi kuongezeka ikiwamo wa fedha maduka kadhaa ya bidhaa eneo la Sanya juu yakiwamo ya nguo kuvunjwa na kuibiwa na watu wanaodaiwa ni vibaka Akizungumza na waandishi wa habari, ametoa rai kuundwa kwa vikundi na kwamba jukumu la usalama wa Wananchi sio la jeshi la Polisi pekee, “Ni kweli jukumu la usalama wa Wananchi sio…

Read More