Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen Arusha Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Arusha imetengua wasimamizi wa mirathi yag bilioni 18.3 ya mali za Marehemu, Melau Mrema aliyefariki mwaka 2017 na kumteua mtoto wa marehemu Randle Mrema kuwa Msimamizi wa mali . Akisoma hukumu hiyo katika shauri dogo namba 170 la mwaka 2022 lililofunguliwa na Randle Mrema pamoja na Lulu Mrema dhidi ya waliokuwa wasimamizi wa mirathi Janeth Kimaro na Viv Mrema ambao pia ni watoto wa marehemu Mrema. Jaji Devota Kamzora alisema kuwa mahakama imezingatia sababu zilizotolewa na waleta maombi ikiwa ni pamoja na waliokuwa wasimamizi wa mali kushindwa kukusanya mali na…

Read More

Na Mwandishi Wa A24Tv  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Dkt Jabiri Bakari, ameahidi kuwa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) itaendelea kuunga mkono wanahabari wa mitandao ya kijamii nchini na kuratibu utatuzi wa baadhi ya changamoto wanazokabiliana nazo huku akisisitiza waandaaji na wapakiaji wa Maudhui mtandaoni kuzingatia kanuni, sheria na miongozo ya Maudhui bora ili kukidhi matakwa ya walaji. Akizungumza katika ziara yake kwenye ofisi za Jukwaa la Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) zilizopo Sinza jijini Dar es Salaam wakati alipofanya ziara yake ikiwa ni sehemu ya TCRA kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa Wateja, Dkt Bakari…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv. Wakati wa ziara ya Ujumbe wa Tanzania nchini Thailand, mbali na kutembelea shughuli za madini, ulipata wasaa wa kukutana na kijana wa Kitanzania Suleiman Kilonda aliyewekeza jijini Bangkok nchini humo kwa kumiliki kiwanda cha kushona na kuchapisha fulana cha Sk Export. Mbali na kumiliki kiwanda, Suleimani amefungua maduka ya kuuza nguo za aina mbalimbali zenye chapa zake za African Man, African Queen, Town Totoz na King Kaka ambapo ameajiri wafanyakazi wapatao 200. Katika mahojiano maalum, Suleiman alisema malengo yake ni kufungua kiwanda kikubwa nchini Tanzania chenye uwezo wa kuajiri watanzania wengi na kutumika kama sehemu ya…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha. Ni Mama Nairo Alisimamisha Jiji la Arusha baada ya kusaini mkataba mnono  na duka la kisasa la kuuza nguo za kike la Cassandra Lingerie la jijini Arusha Mama Nairo wakati wa kusaini dili hilo aliingia  katika viunga vya Hotel ya kitalii ya SG Resort kwa madaha huku akiwa na ulinzi mzito ambao uliwashangaza watu waliofika kushughudia tukio hilo la kistoria . Akizungumza na waandishi wa habari  Oktoba 2, 2023 jijini Arusha, Mkurugenzi wa CASSANDRA LINGERIE, ELIFURAHA MLAKI alisema wanayofuraha kumtambulisha mama NAIRO kama chapa ya sura ya biashara yao kwa lengo la kuleta mapinduzi makubwa ya…

Read More

Na mwandishi wetu, Arusha Wakati shule ya sekondari Sombetini wakilia na uhaba wa madawati 363, Benki ya NMB imefanikiwa kuwakabidhi msaada wa viti na meza 100 vyenye thamani ya shilingi million 10. Msaada huo umetajwa kuwasaidia wanafunzi 100 pa kukalia, huku wakiomba wadau wengine kujitokeza. “Tunashukuru sana kutupunguzia pengo hili kubwa, hakika mmetusogeza sana, kwani tulikuwa na uhitaji wa viti 363 na sasa mmetupa 100 na kufanya idadi ya viti shuleni hapa kufikia 1362 ukiachana na zile 1262 zilizokuwa zinategemewa na wanafunzi wote 1625, msituchoke tukija kuomba vingine 263 zilizobaki” alisema mwalim mkuu wa shule ya Sombetini Bertha John Akizungumza…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha. Wamiliki wa vyombo vya usafiri mkoani Arusha wamekutana kwa  pamoja na Latra Tira na Jeshi la polisi na kufanya mazungumzo zaidi ya  juu ya sheria za usafirishaji. Pichani ni afisa Latra mkiwa Arusha Bwana Joseph Michael Akizungumza na vyombo vya habari mara baada ya kikao hicho afisa wa latra mkoa wa Arusha Joseph Michael amesema kuwa lengo la mazungumzo hayo ni kupeana elimu na  ufafanuzi wa sheria kanuni na taratibu za usalama barabarani.   Amesema kuwa mara baada ya elimu hiyo mkoa wa Arusha unategemewa kuwepo Kwa ufanisa mkubwa na  mabadiliko makubwa katika sekta ya usafirishaji.…

Read More

Na Richard Mrusha Geita. Mkuu wa Idara ya Mosoko kutoka Kampuni ya R.M.Kyando Edger Chifupa amesema Kampuni imedhamiria kuwainua wachimbaji wadogo kiuchumi kwa kuwauzia mitambo ( Mashine ) ya kisasa ya uchimbaji wa Madini Kwa Bei nafuu ili waweze kutimiza ndoto zao kiuchumi. Hayo ameyasema jana wakati wa mahojioano Maalum na vyombo mbalimbali vya habari waliotembelea banda lao kwenye Maonesho ya sita ya Kimataifa na Teknolojia ya Madini yaliyofanyika katika Viwanja vya EPZA Bombambili Halmashauri ya Mji wa Geita 2023. Chifupa amesema Kampuni ya R.M. Kyando inajishughulisha na uuzaji wa Vifaa mbalimbali vya Uchimbaji wa Madini ambapo ipo katika Mikoa…

Read More

Na Mwandishi wa A24tv MKURUGENZI Mkuu wa Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Dkt. Samuel Gwamaka amesema baraza hilo litahakikisha linasimamia kwa ukaribu ujenzi wa Barabara ya Katumba-Lupaso wilayani Rungwe yenye urefu wa Kilomita 35 ili kuhakikisha hauathiri mazingira. Dkt. Gwamaka ameyasema hayo alipoambatana na Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Innocent Bashungwa (Mb) pamoja na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb) kwenye uzinduzi wa Barabara hiyo ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami. Amesema Barabara hiyo inapita kwenye maeneo ya vyanzo vya maji na mito inayotiririsha maji yake kuelekea Ziwa Nyasa na hivyo ni…

Read More