Na.Wizara ya Madini – Chunya. Madini yenye thamani ya shilingi za kitanzania zaidi ya milioni 961 yenye uzito wa kilogramu 6.93 yakamatwa wilaya ya Chunya , Mkoani Mbeya yakitoroshwa kwenda kuuzwa nje ya nchi. Hayo yamebainishwa leo Oktoba 28, 2023 na Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde akiwa katika ziara ya kikazi mkoani Mbeya katika machimbo ya dhahabu wilayani Chunya. Mhe.Mavunde amesema dhahabu iliyokamatwa ina thamani zaidi ya shilingi za kitanzania milioni 961ambapo kama ingetoroshwa Serikali ingekosa mapato ya zaidi mioni 60 . Akizungumza na wafanyabiashara wa Madini katika soko la madini Mbeya Mhe.Mavunde amewataka wafanyabiara wote wa madini kutojihusisha…
Author: Geofrey Stephen
Karibu Arusha 24tv leo October 29 ,2024 kutazama kilicho andikwa katika magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24tv . Mwisho
Mwisho .
Na Geofrey Stephen .Arusha wanachama wa chama cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Arusha ,wafanyabiashara ,viongozi na wananchi, wamejitokeza kwa wingi makao makuu ya ccm Mkoa kusaini kitabu cha Maombolezi cha aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha ZELOTHE STEVEN na kueleza kuwa alikuwa kiongozi shupavu, mnyenyekevu mwenye kujali utu wa watu. Miongoni mwa waombolezaji hao ni pamoja na Mkuu wa wilaya ya Arusha,Felician Mtahengerwa ambaye alisema kuwa mkoa wa Arusha umempoteza kiongozi mwenye sifa zote za uongozi na alijua kulea,Kuongoza na kushauri . “Tumempoteza kiongozi katikati ya watu aliwahi kushika karibia vyeo vyote vya Polisi ,pengo lake ni kubwa sana…
Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt.Solomon Jacob Masangwa anawakaribisha waumini wote pamoja na wadau wa maendeleo kuudhuria katika ibada ya historia ya Kutoa wakfu kanisa la zamani Pamoja na Maduka ya, KKKT Usharika wa Salei / levolosi ,na baadae harambee ujenzi wa shule ya watoto wa jumapili ya (Sunday School .)
Karibu Arusha24tv leo October 28 ,2024 kutazama kilicho andikwa katika magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24rv
Na Wizara ya Madini Dar Es Salaam Ikiwa ni Jitihada za Serikali kuendelea kuweka mazingira rafiki ya kiuwekezaji katika Sekta ya Madini nchini, Wizara ya Madini na Chemba ya Migodi zimekutana Oktoba 27, 2023, ikiwa ni mwendelezo wa utaratibu uliowekwa na Wizara kukutana na Wachimbaji Wakubwa, wa Kati na Watoa huduma migodini kila Robo ya Mwaka kupitia Chemba ya Migodi. Mkutano huo ni wa Pili kufanyika baada ya mkutano wa kwanza uliofanyika mapema mwezi Julai, 2023, yote ikilenga kuleta ukaribu kati ya serikali na wadau wa sekta ya madini pamoja na kujadili kwa pamoja changamoto ili kuondoa vikwazo mbalimbali vinavyozuia…
HISTORIA IMEANDIKWA Na mwandishi wetu Leo saa kumi Alfajiri mtambo wa kuchoronga umeanza kazi rasmi ya utafiti wa HELIUM katika bonde la Rukwa Inaaminika kwamba reserve ya HELIUM iliyopo Mkoani Rukwa ni ya tatu kwa uwingi Duniani nyuma ya Marekani na Qatar,utafiti huu utatupa picha halisi lakini pia utaiweka Tanzania kwenye ramani ya Dunia kama mzalishaji mkubwa wa HELIUM. Gesi ya HELIUM ndio hutumika kwenye vifaa vya ki-eletroniki kama Simu janja(smart phones),viyoyozi,computer, na pia inatumika kwenye kifaa muhimu cha matibabu cha Magnetic Resonance Imaging(MRI). Kazi nzuri ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuweka mazingira rafiki ya uwekezaji imetufikisha hapa…
Arusha kugarishwa na taa za bara barani kila kona. Na Mwandishi wa A24tv. Jiji la Arusha kufungwa taa za Barabarani ili kuongeza usalama wa wananchi na mali zao katika maeneo yao. Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Arusha Maximilian Iranqhe ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya fedha ya Halmashauri ya Jiji la Arusha ilipokuwa ikifanya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo. Mstahiki Meya amesema kutokana na Jiji la Arusha kuwa la kitalii ni muhimu taa za Barabarani kuwepo ili watalii wawekatika mazingira salama zaidi. Amesema kufungwa kwa taa hizo kutaongeza usalama kwa watumiaji barabara hizo. Mradi huo…
Na Geofrey Stephem Arusha Wiki ya Azaki Jijini Arusha Mchungaji wa Kanisa la KKKT Richard Hananja amevunja ukimya juu ya matukio makubwa ya ukatili juu ya wanawake na watoto jambo ambalo limeleta sinto Fahamu kwa wana ndoa kupelekea kufanyanyiana mauwaji ukatili na kupoteza maisha huku familia zao zikibaki na malezi ya upande moja au kukosa kabisa malezi Akizungumza na wadau wa wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Mchungaji Hananja amesema matukio ya wanawake kupoteza maisha kisa mapenzi , ndoa kuvunjika kwa sasa yanaonekana ni fashen jambo ambalo limeonekana jamii kukosa mahadili pia kujiweka mbali na Mungu. Mpaka…