Author: Geofrey Stephen

Na mwandishi wetu Waziri wa Madini nchini Malawi Mhe. Monica Chang’anamuno amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa juhudi na mikakati mbalimbali anayofanya katika kuendeleza Sekta ya Madini nchini. Mhe. Chang’anamuno alitoa pongezi hizo Oktoba 25, 2023 katika hafla ya Usiku wa Madini uliyoambatana na utoaji Tuzo kwa wadau mbalimbali wa Sekta ya Madini waliofanya vizuri ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuthamini mchango wako kwenye maendeleo na ukuaji wa sekta. Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe.Chang’anamuno alisema kuwa mazingira halisi yanaonesha kuwa Rais Dkt. Samia anaendelea kufanya juhudi nyingi sana katika kuendeleza Sekta…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA ,imezifungia laini za simu zipatazo 34,848  zinazodaiwa kuhusika na uhalifu katika kipindi cha Mwezi Julai hadi Septemba mwaka huu. Mkurugenzi Mkuu wa TCRA  Dkt Jabir Bakari amebainisha hayo jijini Arusha wakati akiongea na vyombo vya habari kuhusu mwenendo wa sekta ya mawasiliano katika kipindi cha Robo ya kwanza ya mwaka wa fedha 2023/24. Alisema kuwa  laini za simu zilizofungwa ni zile zilizoripotiwa kupotea ,kuibiwa au kuhusika katika matukio ya uhalifu ikiwemo wizi na utapeli Hata hivyo alisema idadi ya laini zilizofungwa katika kipindi hicho imeshuka kwa asilimia 11.5 kutoka laini 39,394…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Wiki ya Asasi ya Kiraiya imeendelea na vikao vyake Jijini Arusha ambapo leo mapema wametembelea soko la kilombero Jijini Arusha  na kutazama namna wanawake wanavyo jishughulisha na biashara zao za  huuzaji ,Mboga mboga matunda na mahitaji mengine  mbali mbali  muhimu kwa wananchi. Akizungumza na Arusha24Tv Deo Bwire wakili wikili kutoka Asasi ya Kiraiya amesema malengo ni  kutembelea soko hilo ni pamoja na  kusaidia wanawake watoto wa kike  katika kutatua changamoto zinazo wakabili katika  maswala ya ukatili wakiwemo masokoni ambapo asilimia kubwa ni wanawake. Amesema ziara kama hizo ni muhimu katika  kutambua changamoto zao hususani kero za…

Read More

Na Richard Mrusha SERIKALI imesema kuwa inaendelea kuboresha miundombinu mbalimbali ikiwa pamoja na upatikanaji wa umeme wa uhakika pamoja na ujenzi wa miundombinu ya usafirishaji ili kuharakisha ukuwaji uchumi. Imesema kuwa hadi sasa baadhi ya migodi mikubwa ikiwemo Geita Gold Mines Limited (GGML) na STAMIGOLD Biharamulo Mine ambayo ilikuwa haina umeme kwa muda mrefu sasa imeunganishwa na umeme wa gridi ya Taifa Akisoma hotuba hiyo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye alitakiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano wa kongamano la madini la kimataifa lililofanyika Jijini Dar es Salaam Leo Octoba 23 mwaka huu Naibu waziri mkuu DKT.Doto Biteko Amesema…

Read More

Na Richard Mrusha WADAU wa sekta ya madini na wananchi kwa ujumla wameshauriwa kuitumia Taasisi ya TEITI iliyopo chini ya Wizara ya Madini kutambua fursa mbalimbali zinazopatikana. Hayo yamesemwa na Ofisa wa TEITI, Erick Katagory wakati akizungumza na mwandishi wa habari katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam ambapo kunafanyika Jukwaa la Kimataifa la Uwekezaji wa Madini Tanzani. Katagory amesema TEITI inashiriki jukwaa hilo muhimu kwa sekta ya madini, hivyo wanawaomba wananchi na wadau kujitokeza kwa lengo la kupata taarifa za sekta hiyo. Amesema makampuni yote ambayo yameshiriki kwenye mkutano huo ni wadau wa…

Read More

Na Richard Mrusha. Tume ya Madini kwa kushirikiana na Taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Madini leo Oktoba 25, 2023 inashiriki katika Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji Sekta ya Madini unaoendelea katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Viongozi wa Tume wanaoshiriki ni pamoja na Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Profesa Idris Kikula, Makamishna wa Tume ya Madini, Katibu Mtendaji wa Tume ya Madini Eng. Yahya Samamba, Wakurugenzi, Mameneja na Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa. Mkutano huo unafunguliwa na Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto…

Read More

Na mwandishi wetu Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko anatarajia kufungua Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini mwaka 2023, leo jijini Dar es Salaam. Mkutano huo unahudhuriwa na Viongozi, Washiriki na Wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Nchi na unafanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC). Mkutano huo, unatarajiwa kutangaza fursa mbalimbali ya Madini Mkakati na Madini muhimu yaliyopo hapa nchini. Mwisho.

Read More

Na Geofrey Stephen  Arusha Wadau Mbalimbali wanaotumia huduma zitokanazo na Teknolojia wameomba Taasisi za Fedha kurahisisha huduma hizo Kwa watu wenye ulemavu ikiwemo walemavu wa macho Wakizungumza katika Mkutano wa Asasi za Kiraia (Azaki) unaofanyika mkaoni Arusha wadau hao wameomba kupatiwa mfumo shirikishi utakaowasaidia kwenye utumiaji wa Teknolojia katika maeneo Mbalimbali. Renatusi Rupoli ambaye ni mlemavu wa macho kutoka Iringa amesema watu wasioona huwa wanatumia mitandao kwa njia ya sauti ambapo alihoji kwanini kusiwepo na Software kama hizo ambazo zinajumlishwa kwenye Mashine za Kutolea pesa (ATM) Benki Ili kupunguza usumbufu wakutafuta wasaidizi wakati wa kutumia huduma hizo. Mtoa mada katika…

Read More