Author: Geofrey Stephen

Na Richard Mrusha Geita WAKALA wa Majengo Tanzania (TBA) katika mwaka wake wa fedha 2023/2024 inatajia kujenga jengo la ghorofa la biashara na makazi katika Mkoa wa Geita. Akijibu swali la Mbunge wa jimbo la Geita mjini Constantine Kanyasu alipotembelea katika banda hilo katika maonesho ya sita ya tekinolojia ya madini yanayaofanyika katika viwanja vya EPZA bombambili halmashauri ya mji geita ambapo mbunge huyo alitaka kujua endaopo nje ya miradi ya Serikali wakala hao kama wana mpango wowote wakuwekeza miradi kama hiyo Mjini Geita. Akijibu swali hilo Kaimu Meneja Mawasiliano na Masoko – TBA ,Fredrick Kalinga amesema tayari eneo limepatikana…

Read More

Na Geofrey Stephen ,Arusha Katika kuweka Jiji la Arusha katika hadhi ya Kitaifa na Kimataifa Jiji hilo sasa litawekwa taa katika barabara zote na kufungwa CCTV Camera lengo ni kuweka Jiji la Arusha katika hali ya ulinzi na usalama kwa nyakati zote Diwani wa kata ya Daraja mbili Prosper Msofe akionyesha ishara ya kupokea maelekezo kwa mkuu wa wilaya arusha felician Mtehengerwa  Hayo yalisemwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Filician Mtehengerwa katika Mkutano wa hadhara katika kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha ikiwa ni moja ya mikutano yake katika kata za Jiji hil kutatua changamoto ya vibaka wezi katika kata…

Read More

Na Richard Mrusha. Geita Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mh. Constantine John Kanyasu amewapongeza waandaaji wa Maonesho ya sita ya kimataifa ya teknolojia ya Madini na pia kupata nafasi ya kuwa Mgeni mahususi katika kutembelea mabanda mbalimbali yaliyoko katika Maonesho hayo Amesema Maonesho haya yameandaliwa vizuri na washiriki ni wengi na hii inaleta hamasa, hususani ushiriki wa bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi umeongezeka, pia kuongezewa Kwa makampuni ya Madini hasa wanaonyesha Teknolojia ya Madini. Kanyasu amesema Kwa mara ya kwanza Maonesho hayo yameleta Watanzania wanaochimba madini ya vito ( Tanzanite) kutoka kule Naisinyai Wilaya ya Simanjiro…

Read More

Na Geofrey Stephen Ngoro Ngoro. Mahakama ya Hakimu Mkazi Wilaya ya Ngorongoro Mkoani Arusha imemfunga kifungo cha maisha Shedrack Saitoti baada kukutwa na hatia ya kumlawiti mtoto wa miaka saba . Akisoma hukumu hiyo leo septemba 26 mwaka huu Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Ngorongoro,Kohawa Magreth Mboya amesema kuwa  Saitoti amekutwa na hatia baada ya kuridhishwa na ushahidi wa upande wa Jamhuri na vielelezo vilivyowasilishwa mahakamani hapo na mtumiwa kukutwa na hatia hivyo kupelekea kupata adhabu kali ya kifungo cha maisha. Nae Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Mimutie Women Organization Rose Njilo amesema kuwa wao kama…

Read More

Na Richard Mrusha Geita SERIKALI kupitia Wakala wa Nishati vijijini (REA) imefanikiwa kufikisha nishati ya umeme vijijini katika vijiji 10,987 ambayo karibu asilimia 89 ya vijiji vyote 12318 vilivyopo hapa nchini vimeshafikiwa na umeme. Amesema na mapaka baadhi ya wakandarasi wapo saiti wanaendelea na kazi. Amesema matarajio mpaka mwakani vijiji vyote vitakuwa vimeshafikiwa na umeme lakini vijiji vingi vitapata umeme kabla ya desemba mwaka huu na vingine mwakani. “Kwa hiyo tukimaliza zoezi la kupeleka umeme vijijini tunahamia kwenye vitongoji ingawa mradi ya kupeleka umeme kwenye vitongoji tulikuwa tumeshauanza .”amesema. Kwa mujibu wa Mkurugenzi huyo ,Tanzania Bara ina vitongoji 64,760 ambapo…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Mkurugenzi wa Kampuni ya Avat Consultant bi.Edah Mwanry amepongeza Jitihada mbalimbali zilizowekwa katika Uwekezaji wa Vipaji vya Watoto katika Shule ya Msingi ya Enalepo Ili kuhakikisha kuwa wanafikia ndoto zao . Bi.Mwanry ameyasema hayo katika  mahafali ya 15,iliyofanyika shuleni Darajambili katika halmashauri ya Jiji la Arusha. Amesema kuwa Uwekezaji wa mazingira mazuri ya shule bado hautoshi katika kuhakikisha kuwa wanafunzi wanaendelea vizuri kitaluma bali Msingi mzuri unaowekezwa kwao kitaaluma. Akiwatunuku Vyeti wahitimu hao, Mgeni rasmi Bi.Mwanry amewataka wazazi na walezi kuzungumza na watoto wao,wanaohitimu darasa la Saba Kwa kuwa kuna changamoto kubwa ya Maadili katika Dunia…

Read More

Na Richard Mrusha Geita Waziri WA NCHI ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Dkt. Selemani Jafo amelipongeza Shirika la madini la taifa STAMICO kwa kutekeleza kwa vitendo maagizo aliyoyatoa wakati wa Maadhimisho wa Miaka 50 tokea kuanzishwa kwa STAMICO ya upandaji miti Wakati wa maadhimisho hayo STAMICO walikuja na Kampeni ya STAMICO na Mazingira at 50! kwa lengo la kuhakikisha pamoja na uendeshaji wa shughuli za uchimbaji wa madini lakini kuhakikisha mazingira yanatunzwa kikamilifu. “Nawashukuru sana STAMICO kwa kutekeleza kwa vitendo maagizo yangu ya upandaji miti nimeambiwa mpaka sasa mmeshapanda miti 1650 katika Mkoa wa Dodoma na…

Read More

Na Geofrey Stephen  ARUSHA 25 september 2023  TIMU za kusimamia hospitali za rufaa Nchini zimesisitizwa kuhakikisha kwamba zinasimamia ipasavyo  utendaji wa timu za uboreshaji wa huduma za  afya ngazi za mikoa na Wilaya ili kupatikana huduma bora kwa wananchi.   Msisitizo huo umetolewa Leo na Mkuu wa Mkoa wa Arusha,John Mongela,alipokuwa akifungua mafunzo ya wiki mbili ya timu za usimamizi na uendeshaji huduma za afya hospitali za Kanda Nchini yanayofanyika kwenye Kituo cha maendeleo ya Elimu ya afya CEDHA,Jijini Arusha. Mongela,alisema kuwa  Katika kipindi cha miaka miwili Serikali imefanya uwekezaji mkubwa sana kwenye vifaa na miundo mbinu ya afya …

Read More