Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen Arusha WAKUU wa Idara za Utawala na Rasilimali watu Katika Utumishi wa Umma, wameelezwa  Moja wapo ya sifa ya Utumishi uliotukuka ni kujifunza na kusikiliza changamoto za watumishi waliopo chini yao na kuzitatua badala ya kukumbilia kufanya mabadiliko makubwa  ya haraka kwenye taasisi walizopangiwa au kuhamishwa. Hayo yameelezwa Oktoba 13 na Waziri wa nchi ofisi ya Rais Katiba na Sheria Utumishi na Utawala Bora wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Haroun Ali Suleimani,alipokuwa akifunga kikao kazi kilichodumu kwa  siku tatu kwenye Ukumbi wa mikutano ya kimataifa,AICC Jijini Arusha. Watumishi wanapewa vyeo watambue kuwa wameongezewa majukumu na sio upendeleo. Amesema…

Read More

Na Richard Mrusha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amelitaka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kuhakikisha wananchi waliopo kwenye vitongoji wanapatiwa umeme ili kuharakisha maendeleo yao kiuchumi. Mhe. Dkt. Biteko ameyasema hayo alipokuwa akiwasha umeme kwenye Kijiji cha Ndalibo, Kata ya Mtanana Wilaya ya Kongwa sambamba na kuzindua kisima cha maji ambacho kitakuwa kikitumia umeme kwa manufaa ya wananchi wa eneo hilo. “Ndugu zangu niwahakikishie, Mhe. Rais Dkt. Samia anapambana usiku na mchana kuhakikisha umeme unapatikana na kuinua hali za maisha ya wananchi waliopo vijijini kwani umeme sio anasa…

Read More

NA Richard Mrusha Dodoma MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Dodoma Mariam Ditopile amegawa mitungi 250 ya Taifa gesi ya kupikia kwa Jumuiya ya Wanawake Tanzania( UWT) Wilaya ya Kondoa, lengo likiwa kumtua mama kuni kichwani. Aidha uamuzi huo wa kugawa mitungi hiyo ni kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk.Samia Suluhu Hassan ambaye amedhamiria kuondoa nishati chafu ya kupikia kama kuni na mkaa na jamii itumie nishati safi kama gesi ya kupikia. Mariam amegawa mitungi hiyo leo Oktoba 13, 2023 wilayani Kondoa, wakati akizungumza na wanawake wa UWT ambao wanaadhimisha wiki ya…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha  Chuo cha Ufundi Arusha kwa kushirikiana na Benki ya dunia wamezindua mikakati ya kuwawezesha vijana kuondokana na umaskini na kujikwamua kiuchumi na kujenga uchumi imara katika  nchi za Afrika . Hayo yamesemwa jijini Arusha na Mkuu wa chuo cha Ufundi Arusha ,Dk Mussa Chacha wakati akizungumza  katika maadhimisho ya siku ya vijana duniani. Dk  Chacha amesema ,endapo vijana wataelimishwa namna ya kuweza kutumia ujuzi walioupata vyuoni kutasaidia sana kuweza kuanzisha ajira zao na kuweza kuajiri wengine kwa manufaa yao na nchi kwa ujumla.  “Kwa mwaka huu benki ya dunia imeamua kuwakutanisha vijana kutoka nchi za nne…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv.Pwani. Kaimu Mkurugenzi Idara ya Elimu Msingi kutoka Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Ndg. Josephat Luoga amesema Serikali kwa kushirikiana na Wadau wa Maendeleo imekuwa ikitekeleza program na Mipango mbalimbali ya Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi kwa lengo la kuwa na Watanzania walioelimika na wenye uwezo wa kushiriki katika shughuli za maendeleo yao binafsi na Taifa kwa ujumla. Luoga ametoa kauli hiyo leo Oktoba 12, 2023 wakati akifungua Kongamano la Kitaifa la Maadhimisho ya Juma la Elimu ya Watu Wazima linalofanyika Wilaya ya Kibaha mkoani Pwani, ambapo amesema miongoni mwa program…

Read More

Na. Anangisye Mwateba-Dodoma Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki ( Mb) amekagua jengo la ofisi ya Wizara ya Maliasili na Utalii lililojengwa kwenye mji wa Serikali Mtumba jijini Dodoma. Katika ukaguzi huo aliambatana na Naibu wake Mhe. Dunstan Kitandula na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi amesema kwamba jengo hilo kwa sasa limekamilika kwa asilimia 99.9 na kwamba yamebaki maboresho madogo ambayo yatakamilika ndani ya muda mfupi. Jengo hilo la ghorofa tano limejengwa kwa muda wa miezi 21, na limeshakaguliwa vyombo mbalimbali vya kupima ubora kama OSHA na Zimamoto. Mhe. Kairuki ameipongeza Menejimenti ya wizara kwa usimamizi makini na…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula leo Oktoba 11, 2023 amewahimiza Wananchi kutoka mkoani yote kutumia vema Maadhimisho ya Kitaifa ya Juma la Elimu ya Watu Wazima, kuona mafanikio ya program mbalimbali za Kielimu zinazotplewa na Taadidi hiyo pamoja na Taasisi za Elimu ya Juu, Vyuo vya Kati na vya Ufundi. Dkt. Rwezimula ametoa rai hiyo leo Oktoba 11, 2023 wakati akitembelea mabanda ya maonesho katika juma la Elimu ya Watu wazima linalofanyika katika Viwanja vya Maili Moja wilaya ya Kibaha mkoani Pwani ili kujionea huduma zinazotolewa kuelekea Kilele…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Tanzania na Zambia zimekubaliana kutatua changamoto 8 kati ya 24 za kibiashara na 16 zilizobaki zimewekewa utaratibu wa kuzitatua ifikapo Disemba 31, 2023 ili kurahisisha ufanyaji biashara baina ya Tanzania na Zambia ikiwemo kupunguza msongamano wa malori katika mpaka wa Tunduma. Hayo yamesemwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah Oktoba 10, 2023 akiongea na vyombo vya habari wakati wa Mkutano wa Pamoja wa Kujadili Changamoto za Biashara kati ya Tanzania na Zambia uliofanyika 09 – 10/10/2023 katika Kituo cha Huduma za Pamoja Mpakani- Tunduma, Songwe. Aidha, Dkt. Abdallah amesema…

Read More