Author: Geofrey Stephen

Na Richard Mrusha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dkt. Michael Battle, alipomtembelea leo, Septemba 13, 2023 katika ofisi ndogo za Wizara ya Nishati jijini Dar es Salaam. Dkt. Battle amemtembelea Mhe. Biteko kwa lengo la kumpongeza kwa uteuzi na majukumu yake mapya ikiwa ni pamoja na kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kisekta baina ya nchi hizo mbili. Katika mazungumzo yao Mhe. Biteko ameeleza kuwa, Wizara ya Nishati itaendelea kushirikiana na wadau wa kitaifa na kimataifa katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya Sekta ya…

Read More

Na Richard Mrusha Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji amewataka wawekezaji Wazawa ambao wamepewa zabuni ya kuchimba Makaa ya Mawe katika mradi wa Mchuchuma Wilayani Ludewa Mkoani Njombe kufanya kazi kwa weledi mkubwa ili kufikia malengo ya Serikali ya uendelezaji wa miradi ya Kimkakati.. Waziri Dkt Kijaji amesema hayo Septemba 12,2023 Jijini Dar es salaam wakati wa hafla ya utiaji saini wa Mikataba ya makubaliano kati ya Makampuni matano ya Wazawa na Shirika la Taifa la Maendeleo( NDC) ambayo yatatekeleza mradi wa Liganga na Mchuchuma kwakua ni maendelezo ya maono ya Serikali ya awamu ya sita ya kuendeleza…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Katika kupunguza tatizo la upatikanaji wa mafuta kwa wafanyabiashara binafsi wanaouza mafuta (petroli) ambalo linawapelekea mafuta kukosekana katika vituo vyao na wananchi kuteseka , wafanyabiashara kanda ya kazskani  wametakiwa kuingia mikataba na wafanyabiashara wakubwa wanaoagiza mafuta nje ili wawe na uhakika wa upatikanaji wa mafuta na kuondoka shida ya kukosekana mafuta katika vituo vyao. Hayo yamebainishwa na meneja wa kanda ya kaskazini wa mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA)Lorivii Lon’gidu wakati akiongea na wafanyabiashara binafsi wa mafuta katika kikao kazi kilichoandaliwa na EWURA kikiwa na lengo la kukumbushana taratibu za ufanyaji biashara…

Read More

Na Geofrey  Stephen Arumeru. Katika hali ya kuendeleza kazi ya Mungu Nabii Mkuu Dokta GeoDavie amezindua kanisa la kisasa pamoja na kumkabidhi rasmi Mchungaji Jackob Sabore kwa lengo la kueneza injili ya neno la Mungu. Akiongea na Maelfu ya waumini waliojitokzeka katika shughuli hiyo Nabii Mkuu amesema kazi ya Mungu itaendelea kubarikiwa kwa kuwa watumishi wengi kwa sasa wanatangaza injili kwa kuwapa furaha waumini pamoja na kusaidia kutatuwa matatizo yao katika maisha yao. Zoaezi la kukabidhi kanisa kwa Sabore liliendana na utukufu wa kuwashika wajasiria mali mikono kwa mitaji ambapo zaidi wa wajasiria mali wapatao kumi na tatu walipatiwa mitaji…

Read More

Na mwandishi wetu Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Bagamoyo Mkoani Pwani Shauri Selenda amewatoa hofu Watanzania juu ya taarifa zilizosambaa kuhusu njama za kuvuja kwa mtihani wa taifa wa darasa la saba unaotarajiwa kufanyika wiki hii kote nchini. Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Selenda alisema amepokea taarifa za baadhi ya maafisa wake kuhusishwa na hujuma na wizi wa mtihani wa mwaka 2023 katika shule ya awali na msingi ya Baobao na tayari amechukua hatua za kuwaengeua katika zoezi la usimamizi wa mitihani hiyo ili kupisha uchunguzi kutokana na kutajwa kwenye tuhuma hizo. “Taarifa hizi zimetufikia na tayari…

Read More

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji(Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza uhusiano wa kibiashara na China hususan katika uchakataji wa mazao ya kilimo na Balozi wa China nchini, Mhe. Chen Mingjian katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2023. Tanzania inasafirisha mazao ya kilimo kama parachichi, kahawa, mahindi , ufuta na asali kwenda China. Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amekutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Uturuki hususan katika sekta ya kilimo katika mazao ya Chai, matunda na mazao…

Read More

Na Doreen Aloyce. Askari wahifadhi kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) septemba 11, 2023 walifanikiwa kumuokoa mtoto wa tembo anayekadiriwa kuwa na umri wa wiki nne (4) aliyezama katika shimo lenye matope katika Kijiji cha Kwamsanja kilichopo kata ya kibindu halmashauri ya Chalinze jirani na Pori la Akiba Wamimbiki. Taarifa za Mtoto huyo wa tembo aliyetelekezwa na kundi lake kutumbukia shimoni zilitolewa na raia mwema aitwaye Manase Thomas Baha mkazi wa Kijiji cha Kwamsanja na kumlazimu Kamanda wa Pori la Akiba Wamimbiki Emmanuel Lalashe kutuma timu ya askari wanne (4) walioshirikiana na askari wa Jeshi la Akiba (migambo)…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa,Tundu Lissu amezungumza na vyombo vya Habari mara baada ya kumaliza mahojiano na jeshi la polisi Mkoani Arusha na kudai amehojiwa kuhusu kufunga barabara ambapo alikanusha madai hayo kwa kile  alichoeleza kuwa yeye alikuta barabara hiyo imeshafungwa na polisi waliovaa kiraia wakilenga kumzuia asiende kwenye mikutano yake Ngorongoro. Lissu amesema mikutano yake katika Jimbo la Ngorongoro iko pale pale pamoja na karatu itafanyika mara baada ya mapumziko ya siku chache  hivyo wananchi wavute subira watatangaziwa siku na wapi mikutano itafanyika tena . amesema vibali vya kufanya mikutano Ngorongoro avitoki kwa jeshi…

Read More