Author: Geofrey Stephen

Na Richard Mrusha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kufanyia kwa ufanisi majukumu yake ya msingi ambayo ni kupanga, kupima na kumilikisha ardhi ili kuondoa migogoro ya ardhi inayotokea nchini na kuifanya Wizara husika kuishughulikia mara kwa mara. Ameyasema hayo tarehe 9 Septemba, 2023 jijini Dodoma wakati wa hafla ya kuzindua kituo cha Taifa cha Ubunifu na Mafunzo ya taarifa za kijiografia kwa niaba ya Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa. “ Kazi za Wizara hii ni tatu, ambazo ni kupanga, kupima na kumilikisha ardhi, sasa tujipime…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amewataka viongozi wa kijamii na Machifu kuendelea kudumisha misingi ya Mila sanjari na kutunza Amani mshikamano na Umoja wa Watanzania. Aidha filamu ya Royal Tour imeleta mafanikio makubwa katika kusukuma biashara na ustawi wa jamii kwa Watanzania Moja ya kabila lililobeba urithi huo Kwa muda mrefu Pamoja na changamoto za mabadiliko ya Mfumo wa maisha ni Wamaasai. Yamesemwa hayo Kwa niaba yake na Katibu Tawala Msaidizi Mkoa wa Arusha David Lyamongi wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Utamaduni wa Wamaasai (Maasai Festival )linanalofanyika siku tatu kuanzia Tarehe 8-10…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv . Serikali imesema lango la kuingilia watalii kupitia maeneo ya Kilangali na Tindiga Wilaya ya Kilosa litafungua fursa ya watalii watakaosafiri na treni ya mwendokasi kutoka Dar es Salaam na Dodoma kuingia Hifadhi ya Taifa Mikumi kwa urahisi. Haya yamesemwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Dunstan Kitandula alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Mikumi Mhe. Dennis Lazaro Londo, ambaye alitaka kujua Serikali imefika hatua gani katika mchakato wa ujenzi wa Geti jipya la kuingilia Hifadhi ya Mikumi kutokea Kilangali na Tindiga. Awali Mhe. Kitandula alisema kuwa Serikali imekamilisha tathmini ya awali kwa ajili…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa ameitaka Wizara ya Maliasili na Utalii kuendelea kutumia sheria na taratibu zilizopo kulinda Wanyama waliohifadhiwa katika hifadhi za taifa pamoja na mapori ya akiba hapa nchini. Mhe. Waziri Mkuu ameyasema hayo leo tarehe 07 Septemba, 2023 wakati akijibu swali la Mbunge wa Mwanga Mhe. Joseph Anania Thadayo wakati wa maswali kwa Waziri Mkuu ambapo alitaka kujua kuwa Serikali ina mkakati gani wa kuhakikisha inapitia upya sheria za uhifadhi ambazo ziliwekwa kwa ajili ya kulinda uhifadhi lakini poa sheria hizo ziwalinde wananchi hata ikibidi kujitoa…

Read More

Na Richard Mrusha Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali amekutana na kuzungumza na Ujumbe kutoka Ubalozi wa Marekani nchini katika ziara iliyolenga kuzungumzia masuala mbalimbali katika shughuli za uchimbaji na maendeleo ya Sekta ya Madini, Mji wa Serikali jijini Dodoma. Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika leo Septemba 7, 2023, Katibu Mkuu Mahimbali amesisitiza kuimarisha ushirikiano katika uchimbaji wa madini hususan ya kimkakati, kujengewa uwezo wataalam mbalimbali wa Sekta ya Madini ili mnyororo mzima wa shughuli za madini unufaike. Amesema kuwa Wizara ya Madini imeweka vipaumbele katika maeneo manne ili kuimarisha zaidi Sekta hiyo, maeneo hayo ni pamoja na Utafiti…

Read More

Na Richard Mrusha Imeelezwa kuwa Madini ya Vito aina ya Spinel yanayochimbwa Mahenge Tanzania ni miongoni mwa bidhaa inayotafutwa kwa kiasi kikubwa na Wanunuzi na Wauzaji Wakubwa wa Madini ya Vito na Usonara wanaoshiriki na kutembelea katika Maonesho ya 68 ya Vito na Usonara yanayoendelea katika jiji la Bangkok eneo la Queen Sirikit nchini Thailand. Hayo yamebainishwa Septemba 9, 2023 na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ruby International Limited Mhe. Salim Hasham ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Mahenge Mkoa wa Morogoro ambaye kampuni yake inashiriki katika maonesho hayo. Kampuni hiyo inajishughulisha na uuzaji, uchimbaji na ununuzi wa madini…

Read More