Kamishna Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA), Aretas Lyimo, amesema kuwa katika operesheni maalum iliyofanyika mkoani Arusha, mamlaka hiyo ilifanikiwa kukamata pembe moja ya ndovu pamoja na risasi 11 za moto. Aidha, katika tukio jingine mkoani humo, mtu mmoja alikamatwa akiwa ameotesha miche ya bangi ndani ya nyumba yake kwa kutumia glasi za plastiki (disposable). Kamishna Lyimo amebainisha kuwa biashara haramu ya dawa za kulevya mara nyingi inahusiana na uhalifu mwingine, ikiwa ni pamoja na usafirishaji haramu wa silaha. Katika kipindi cha Januari hadi Februari 2025, DCEA ilikamata jumla ya kilogramu 98.55 za bangi,…
Author: Geofrey Stephen
mamlaka ya Serikali Mtandao (e-GA) imetoa tuzo kwa Taasisi za Umma zilizofanya vizuri katika utekelezaji wa Serikali Mtandao ikiwa ni sehemu ya mipango ya Serikali ya kuchochea matumizi TEHAMA Serikalini ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi. Akizungumza wakati wa ugawaji wa Tuzo hizo katika Kikao kazi cha 5 cha Serikali Mtandao kilichofanyika jijini Arusha, Meneja wa Usimamizi wa Udhibiti na Viwango vya Serikali Mtandao Bi. Sultana Seiff. amesema Mamlaka iliweka vigezo mbalimbali ambavyo vilizingatiwa katika upatikanaji wa Taasisi zilizofanya vizuri katika Utekelezaji wa Serikali Mtandao. Amesema Tuzo hizo ziligawanyika maeneo makuu matatu (3) ya utekelezaji wa Serikali Mtandao ambayo ni…
Karibu Arusha24tv leo feb 18 Mwaka 2025 kutazama kilicho andikwa katika magazeti ya Tanzania mbele na nyuma hii ni A24tv . Mwisho.
Na Bahati Siha . Katibu wa Jumuiya ya Wazazi wa chama cha mapindizi(CCM),Wilaya ya Siha Abdallah Chumu,amewashukuru Wadau wa michezo Wilayani humo kwa kufanikisha kwa kiasi kikubwa kumalizika kwa Ligi ya Samia Wazazi cup Siha kwa mafanikio Kauli hiyo ameitoa February 16 2025,mara baada ya mashinda hayo kufikia ukingo katika uwanja wa ccm SanyaJuu Wilayani humo na yalianza mwaka jana,kushirikisha timu 17. Akizungumza na waandishi wa habari uwanjani hapo wakati timu zikikabidhiwa zawadi ,amewashuru Wadau hao wa michezo kwa kuona umuhimu na jitihada za kuona michezo inasonga mbele Wilayani humo. “Ni kweli lazima niwapa kongole wale wote waliotusaidia kufanikisha michezo…
Na Mosses Mashala Zanzibar . Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema Chama cha Mapinduzi (CCM) ameisisitiza UVCCM kuendeleza kasi ya uhamasishaji uandikishaji wa Daftari la kudumu la wapiga kura na kuhakikisha vijana wengi wanajiandikisha litakapoanza kwa upande wa Unguja hivi karibuni. Ametoa wito kwa vijana kutobaki nyuma siku ya kupiga kura ili CCM ipate ushindi wa kihistoria na kuendelea kushika Dola. Dkt.Mwinyi ameyasema hayo alipozungumza baada ya kuweka jiwe la msingi la Bweni la Vijana wa Kiume wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM). Aidha Dkt.Mwinyi…
Na Richard Mrusha Morning Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde amepiga marufuku raia wa kigeni kuingia na kufanya shughuli kwenye leseni za uchimbaji mdogo; hii ni kufuatia changamoto zilizobainika katika uingiaji mikataba ya utoaji wa misaada ya kiufundi kati ya wamiliki wa leseni ndogo za uchimbaji madini na raia wa kigeni. Amesema hayo leo Februari 17, 2025 wakati akifungua Kikao Kazi cha kupokea maoni kutoka kwa wadau kuhusu mapendekezo ya kuandaa Rasimu ya Kanuni za Madini za Utoaji Msaada wa Kiufundi kwa Wamiliki wa Leseni Ndogo za Uchimbaji Madini za Mwaka 2025 kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Edema Hoteli…
Juma Tatu ya leo tarehe 17 mwaka 2025 karibu Arusha24tv kutazama kikicho Andikwa katika Magazeti ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24tv . C m Mwisho .
Na Geofrey Stephen Arusha . Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Paul Christian Makonda, ameongoza wananchi na viongozi mbalimbali wa Mkoa huo katika kampeni maalum ya usafi wa mazingira na upandaji miti Kata ya Ambureni, Halmashauri ya Meru. Tukio ambalo limefanyika leo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku yake ya kuzaliwa. Katika kampeni hiyo, Mhe. Makonda amesisitiza umuhimu wa kutunza mazingira kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho huku akiwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika shughuli za usafi na kuhakikisha wanapanda miti kwa wingi ili kusaidia kuhifadhi vyanzo vya maji na kupunguza athari za mabadiliko ya tabianchi. “Leo nina…
Siha, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro Paschal mboto, amesema athiri iliyokuwepo katika hospital hiyo ni Watumishi 6 walioajiriwa kutoa hudumia kwa watu wenye vvu mishahara yao ilisitishwa baada ya tangazo la Trump Kauli hiyo imekuja baada ya Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Dancan Urasa kutaka kufahamu baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kusitishwa kutoa misaada katika maeneo ya afya kuna athari yeyote imejitikeza katika Wilaya yetu Mganga Mkuu huyo Akizungumza February 14 2025,kwenye Baraza la madiwani halmshauri hiyo, amesema athari iliyopo ya watumishi 6 mikataba kusitishwa na kukosa mishahara,wale ambao walikuwa wanalipwa na shirika la (USAID)la kimarekani…
Juma Mosi ya leo tarehe 15 Mwezi wa Pili Mwaka 2025 karibu kutazama kilicho Andikwa katika Magazeti ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24tv . Mwisho .