Author: Geofrey Stephen

Na mwandishi wetu Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, amesema kuwa watanzania wanahitaji kupata huduma ya umeme wa uhakika na kwamba ameridhishwa na kazi kubwa ya utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP). Balozi Kusiluka ameeleza hayo tarehe 6 Septemba, 2023 wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa JNHPP ili kuona maendeleo ya Mradi huo unaotarajiwa kuzalisha Megawati 2115 za Umeme ambao unatekelezwa katika Mkoa wa Pwani. Amewasisitiza wataalamu wanaotekeleza mradi huo kuwa wahakikishe kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati kwani watanzania wanausubiri kwa hamu kubwa na wanataka kunufaika na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali yao.…

Read More

Na Doreen Aloyce, Dodoma Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika utakaofanyika Jijini Arusha kuanzia Oktoba 23 hadi 27 mwaka 2023. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi wakati akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano huo kilichohudhuriwa na Makatibu Wakuu ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu masuala muhimu yatakayojadiliwa. Dkt. Yonazi amesema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisema Nchi wanachama wa…

Read More

Na Mwandishi wetu Dodoma Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amefungua mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara za Kisekta, Taasisi za umma pamoja na sekta binafsi zinazotoa huduma za Ustawi wa Jamii nchini na kutoa maelekezo mahsusi yatakayofanya sekta hiyo kuwa imara na kutoa huduma bora katika Taifa. Dkt.Doto Biteko amefungua Mkutano huo tarehe 6 Septemba, 2023 jijini Dodoma ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, Naibu Waziri, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Dodoma Serikali imesema inaendelea na jitihada za kudhibiti mimea vamizi katika maeneo ya Hifadhi na Mapori ya Akiba kwa lengo la kurejesha uoto wa asili nchini ambao ni tegemeo kwa wanyamapori. Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula wakati akijibu swali la Mbunge wa Donge, Mhe.Mohamed Jumah Soud aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kupunguza upoteaji wa uoto wa asili nchini unaosababisha kupoteza hadhi kwa Hifadhi na Mapori ya Akiba. Mhe. Kitandula ametaja sababu kubwa ya kupotea kwa uoto wa asili katika Hifadhi na Mapori ya Akiba kuwa ni ongezeko…

Read More

Na Mwanfishi wa A24tv . Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali inayolenga kuendeleza, kukuza na kutangaza vivutio vya utalii nchini ikiwemo vivutio vilivyopo Kisiwa cha Ukerewe kama Mapango ya Handebezya na Jiwe linalocheza. Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ukerewe Mhe. Joseph Mkundi aliyetaka kujua mkakati wa Serikali kuvifanya vivutio vya Mapango ya Handebezya na Jiwe linalocheza kuwa na tija kwa Taifa. Amefafanua kuwa moja ya mikakati hiyo ni pamoja na  kutangaza vivutio hivyo kwa kutumia vyombo  mbalimbali vya habari. “Wizara…

Read More

Matukio ya uhalifu ,ubakaji na wizi yazidi kutikisa kata ya Daraja mbili mkoani Arusha . Na Geofrey Stephen Arusha . Matukio ya uhalifu katika kata ya Daraja Mbili Mkoani Arusha yamezidi kushika kasi mara baada ya Mtendaji wa kata hiyo John Joseph kunusurika kuchomwa kisu cha ubavuni na kibaka wakati akiwa katika harakati za kumwokoa msichana aliyetambulika kwa jina la Caren Nyangasa (20) aliyenusurika kufanyiwa kitendo cha ubakaji na kibaka aliyetambulika kwa jina la Bolo young . Akizungumzia tukio hilo,Mtendaji wa kata hiyo amesema toka mei mwaka huu hadi sasa hivi kata yake imekuwa na matukio makubwa ya uvunjifu wa…

Read More