Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi Wetu Rufiji, Pwani. MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba Nchini (TMDA) Kanda ya Mashariki imetoa tahadhari kwa wananchi juu ya utupaji holela wa dawa zinazobaki majumbani kutokana na hatari zake kwa afya ya binadamu na mazingira. Akizungumza wakati wa zoezi la kutoa elimu katika shule ya Sekondari ya wasichana Bibi Titi Mohamed iliyopo Halmashauri ya Rufiji Mkoa wa Pwani, Mkaguzi wa Dawa Kanda ya Mashariki Bw Japhari Saidi ameeleza kuwa dawa zinazobaki majumbani hazipaswi kutupwa jalalani, chooni, kwenye vyombo vya kukusanya taka au kuchomwa moto katika maeneo ya wazi badala yake zirudishwe kwenye vituo vya kutolea huduma za…

Read More

Na Richard Mrusha. Ruangwa WAWEKEZAJI nchini wameshauriwa kusajiri miradi yao kupitia kituo cha uwekezaji TIC ili waweze kupata msamaha wa kodi inayotolewa na Serikali kupitia TIC. Akizungumza leo 24 Aug 2023 katika maonyesho ya madini yanayofanyika katika viwanja vya soko jipya kilimahewa wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Afisa muwekezaji mkuu TIC Kanda ya Mashariki Griyson Mtimba amesema kuwa wapo katika maonyesho ya madini na uwekezaji yanayofanyika katika Wilaya ya Ruangwa Mkoani Lindi kwa ajili kufutia na kuhamasisha wawekezaji wa ndani na wa nje waweze kuwekeza Tanzania lakini pia katika mkoa wa Lindi. Amesema pia hao kama TIC wana jukumu wanafanikisha…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha WAKALA wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) inatoa mafunzo ya siku tatu kwa wafanyabiashara wa mazao nje ya nchi ili waweze kurasimisha biashara zao. Mafunzo hayo yanatolewa jijini Arusha kuanzia leo, Agosti 24 mpaka 26,2023 kwenye ukumbi wa hoteli ya GoldenRose. Akifungua mafunzo hayo, Kaimu Katibu Tawala mkoa wa Arusha, Ramadhani Madeleka amewataka wadanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo ya kusajili makampuni na majina ya biashara zao  ili zitambulike na wafanye kazi ya usafirishaji nje ya nchi bila vikwazo. Amesema mafunzo hayo yanagharamiwa na serikali na elimu watakayoipata iwawezeshe kuwa tija kwenye shughuli zao baada ya kuelewa…

Read More

Na Mwandishi Wetu, Kigali, Rwanda. MAMLAKA ya Dawa na vifaa Tiba Tanzania (TMDA) imechaguliwa kuwa Kitivo cha Kikanda katika udhibiti wa dawa za chanjo Barani Afrika katika mkutano wa taasisi za udhibiti wa dawa barani Africa (AMRC) mapema leo tarehe 24 Agosti, 2023. Katika tukio hilo, Mkurugenzi wa Uendeshaji Huduma kutoka TMDA, Chrispin Severe alipokea barua ya utambuzi wa TMDA kama Kitivo cha Kikanda (Regional Centre of Regulatory Excellence – RCORE) katika udhibiti wa dawa za chanjo kutoka kwa Mkurugenzi wa AUDA – NEPAD wa Utumishi na Maendeleo ya Taasisi za Udhibiti, Bw. Symerre Grey-Johnson. Kwa TMDA kuchaguliwa kuwa RCORE…

Read More

Na mwandishi wa A24Tv Arusha. Jopo la wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 21 wa kanisa la kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) umemchagua kwa kishindo  askofu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dr Alex Malasusa kuwa mkuu mteule mpya wa KKKT kupokea nafasi ya Askofu Dkt Frederick Shoo aliyestaafu baada ya kumaliza muda wake wa uongozi  wa kanisa la Kkkt . Mwenyekiti wa uchaguzi huo iliyofanyika Arusha Askofu Amon Mwenda alisema Askofu Malasusa ameshinda Kwa kura 167 sawa na asilimia 69.3 ya kura zote 241 zilizopigwa huku askofu Abednego kesho Mshahara akipata kura 73 sawa na asilimia 30.3. Askofu Malasusa anarejea…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Chuo cha Ufundi Arusha (ATC) kupitia Umoja wa Wakandarasi wazawa Tanzania (ACCT) kimepongezwa kwa jitihada za kuendesha kituo cha mafunzo ya vitendo kwa mafundi mchundo wa fani mbalimbali za ujenzi chenye lengo la kurasimisha ujuzi wao ili uweze kutambulika kwenye soko la ajira. Pongezi hizo zimetolewa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Prof. Adolf Mkenda (Mb) alipotembelea Chuo hicho na kufanya ziara kwenye kituo hicho. Prof. Mkenda amesema kwamba kinachofanyika hapo ndio ndoto ya serikali ya kukuza ujuzi kwa vitendo. “Kinachofanyika hapa ndio ndoto ya serikali na hata ukikumbuka ahadi ya Mhe. Rais…

Read More

na Richard Mrusha. Ruangwa MKURUGENZI wa kampuni ya vifaa vya ujenzi ya SHEVA HARDWARE MaryStella Temba amewaasa wachimbaji wadogo kutumia vifaa vya usalama sehemu za migodi kwa kufanya hivyo watakuwa salama. Amesema kuwa wamekuwa kwenye biashara hiyo kwa muda mrefu na wamegundua kuwa iko haja ya wachimbaji wadogo kutumia vifaa bora haswa kutoka kwao kwasababubu vinaubora wa hali ya juu na vinagaratiii. kauli hiyo imetolewa Leo Agosti 24 na mkurugenzi wa kampuni ya Sheva Hardware MaryStella Temba katika maonyesho ya madini ambayo yanafanyika wilayani Ruangwa mkoa wa Lindi amesema kuwa wao kama Sheva Hardware wanawakaribisha wananchi kwenye Banda la Kampuni…

Read More

Na Richard Mrusha. Nachingwea Jumla ya Vijiji vipatavyo 11 kutoka Kata 4 Naipanga, Chiumbati, Rahaleo na Stesheni Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi vinatarajia kunufaika na mradi wa huduma ya maji safi na salama wa Naipanga wenye jumla ya thamani ya sh.bil.1,187,057,785 Hayo yalibainishwa jana na Meneja wa Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA ) Wilayani hapo na Mhandisi Sultan Ndoliwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuutambulisha mradi huo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohamed Moyo, na wajumbe wa Halmashauri kuu ya Vijiji hivyo. Mhandisi Ndoliwa amesema mradi wa Maji wa Naipanga upo katika kata ya…

Read More