Author: Geofrey Stephen

Na Richard Mrusha. Nachingwea Jumla ya Vijiji vipatavyo 11 kutoka Kata 4 Naipanga, Chiumbati, Rahaleo na Stesheni Wilayani Nachingwea Mkoani Lindi vinatarajia kunufaika na mradi wa huduma ya maji safi na salama wa Naipanga wenye jumla ya thamani ya sh.bil.1,187,057,785 Hayo yalibainishwa jana na Meneja wa Wakala wa Maji na usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA ) Wilayani hapo na Mhandisi Sultan Ndoliwa wakati akizungumza na waandishi wa habari kuutambulisha mradi huo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea Mohamed Moyo, na wajumbe wa Halmashauri kuu ya Vijiji hivyo. Mhandisi Ndoliwa amesema mradi wa Maji wa Naipanga upo katika kata ya…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb.) ameiagiza Menejimenti ya Wizara na Taasisi zake kuhakikisha Mipango yote inayopangwa kila mwaka inaendana na mwelekeo wa Viongozi Wakuu wa Nchi, Mipango ya Kitaifa na Kimataifa, Ilani ya Uchaguzi pamoja na kufanya ufuatiliaji na tathimini ili kujua viwango vya utekelezaji wake. Kigahe ameyasema hayo Agosti 23, 2023 alipokuwa akifungua Kikao Kazi cha Menejimenti na Wakuu wa Taasisi zilizochini ya Wizara kilichofanyika katika Ukumbi wa CAMARTEC, Arusha kwa lengo la kujadiliana na kuimarisha ushirikiano katika utatuzi wa changamoto na utekelezaji wa jitihada mbalimbali za kuendeleza Sekta ya…

Read More

Na Richard Mrusha. Ruangwa JESHI la Zimamoto na Uokoaji limewataka wananchi kuwa na vifaa vya kuzimia moto wa awali ili kuokoa maisha ya watu pamoja na kuzuia uharibufu mkubwa wa mali zao hata kabla Jeshi hilo halijafika katika eneo la tukuo. Hayo yamesemwa na Stafu Sajenti Enock Mapunda kutoka Jeshi la Zimamoto na Ukoaji mkoa wa Lindi wakati wa maonyesho ya Madini yanayoendelea mkoani humo. “Lengo la kukabiliana na moto wa awali ni kusaidia Jeshi la Zimamoto na Ukoaji kuuzima moto na pia kusaidia mali na maisha ya wananchi kuwa katika hali ya usalama.”amesema Mapunda Aidha ameongeza kuwa,Jeshi hilo limejipanga…

Read More

Na Richard Mrusha Ruangwa ZAIDI ya shilingi bilion kumi na moja zimetumika katika mwaka wa fedha 2021/2022 katika ujenzi wa barabara zinazoelekea katika maeneo migodi Wilayani Rwangwa mkoani Lindi. Akizungumza na waandishi wa habari katika maonesho ya madini yanayoendelea katika wilaya ya Rwangwa ,Meneja Tarura Wilaya ya Rwangwa Mashaka Narubi amesema kuwa pia mwaka huo huo wa fedha 2021/2022 wamejenga barabara za lami maeneo ya mji wa Rwangwa mjini ambazo zinaelekea maeneo yote ya migodi ambapo zimegharimu shilingi bilioni 5.2. Amesema lengo la ujenzi wa barabara hizo ni kurahisisha shughuli za uchimbaji wa madini unaoendelea Wilayani humo ili ziweze kupitika…

Read More

Na Richard Mrusha Ruangwa MOJA ya changamoto inayoikabili sekta ya chumvi nchini ni ubora wa chumvi,masoko,mitaji na upatikanaji wa vifaa vinavyohusika katika uzalishaji wa bidhaa hiyo . Hayo yamesemwa na Meneja Uwezeshaji,Uchimbaji mdogo wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Tuna Bandoma wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maonyesho ya Madini yanayoendelea katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi. Bandoma amesema kuwa chumvi imekuwa ni kilio kikubwa na serikali imekuwa na mikakati mingi ambapo mojawapo ya mkakati wa serikali ni kukaa na wadau ili kujadili kwa kina changamoto zilizopo pamoja na kujua kwa pamoja suluhu mbalimbali ambazo zinazotokana na sekta…

Read More

Na GEOFREYSTEPHEN ,Mirerani Sakata la uvamizi wa Mgodi wa Madini ya Tanzanite katika Kitalu C unaomilikiwa na serikali katika Mji wa Mirerani wilayani Simanjiro Mkoani Manyara sasa umeingia sura mpya baada ya Kampuni ya Tanzanite Exploler kukaidi maagizo yaliyotolewa na afisa mfawidhi wa madini RMO na kuomba msaada kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara. Kampuni ya Tanzania Exploler inayomilikiwa na Victor Mkenga na kampuni nyingine ikiwemo ya Saniniu Mining inayomilikiwa na Bilionea Saniniu Laizer na Kampuni ya Manga Gems{T] ltd inayomilikiwa na familia ya Mathias Manga zinatuhumiwa kuingia katika mgodi wa serikali wa kitalu C kinyume na sheria na kuvuna…

Read More

Na Doreen Aloyce,Dodoma. Katibu Mkuu Mahimbali aeleza Mipango Kabambe kuendeleza Sekta ya Madini, aeleza Miradi Mingine Mbioni kupewa Leseni Katibu Mkuu Wizara ya Madini Kheri Mahimbali ameieleza Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuwa hadi kufikia Juni, 2023 miradi ya uchimbaji mkubwa wa madini ambayo Serikali ina hisa imechangia mapato ya Serikali ya jumla ya Shilingi *Trilioni 1.53* ambayo yametokana na tozo na kodi mbalimbali. Mahimbali ameyasema hayo Agosti 21, 2023 jijini Dodoma kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakati akiwasilisha taarifa kuhusu hali ya uendeshaji wa migodi ambayo Serikali ina hisa na…

Read More