Author: Geofrey Stephen

Arusha  Na Geofrey Stephen Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mohamed Mchengerwa ameitaka Bodi mpya ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), kwenda kuondoa utendaji wa mazoea ili kuweka misingi ambayo itaifanya Tanzania kuwa namba moja Afrika na dunia katika sekta ya utalii. Waziri Mchengerwa ameyasema ayo  2023 jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) na Bodi ya Wadhamini ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA). Aidha, ameitaka Bodi ya TTB kukaa na Menejimenti ili kufanya mapitio ya Sheria ili kuleta mapinduzi makubwa katika sekta ya utalii. Waziri Mchengerwa ameitaka Bodi…

Read More

Na Ahmed Mahmoud RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amekabidhi tuzo mbili Kwa Shirika la bima la Taifa ikiwa ni kutambua mchango wao Kwa ufanisi mkubwa wa kifedha na kiuendeshaji pia mabadiliko makubwa ya kiutendaji kuongeza ufanisi tija na ubora wa huduma katika kipindi kifupi. Hayo yameelezwa Mara baada ya kupokea tuzo hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Taifa la Bima nchini Dkt.Elirehema Dorie wakati wa Kikao Kazi cha wenyeviti wa Bodi na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma nchini kinachoendelea Kwa siku tatu Jijini Arusha. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji huyo tuzo zinaakisi…

Read More

Na Ahmed Mahmoud SHIRIKA la Mawasiliano Tanzania (TTCL) limeanza kujidhatiti kupamba na mabadiliko ya kiuchumi ya Teknolojia ya Tehama  duniani kwa kuanza kutoa huduma ya intaneti majumbani na maeneo ya wazi. Mkurugenzi wa Biashara Shirika la Mawasiliano nchini TTCL ,Vedastus Mwita amesema hayo leo jijini Arusha alipohudhuria kikao Kazi cha wenyeviti wa Bodi na watendaji wakuu wa Taasisi za Umma,na Binafsi. Mwita alisema kuwa TTCL imejipanga kuhakikisha intaneti inapatikana majumbani na maeneo ya wazi ili kumwezesha mwananchi kupata mawasiliano popote alipo na hilo limewezekana kwa shirika hilo kuweka huduma hiyo katika Mlima Kilimanjaro na intaneti kuwa na kasi kubwa. Alisema…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeng’ara katika kikao kazi cha Wenyeviti na Watendaji wa Mashirika ya Umma baada ya kuibuka mshindi wa kwanza katika Taasisi za umma zilizofanya mabadiliko makubwa ya kiutendaji na yenye tija kwa mwaka 2023. (Turn Around Company in Financial and Operational Performance as of June 2023) Pia STAMICO imenyakua tuzo ya pili katika kundi la mashirika ya umma ambayo yametoa gawio kwenye Mfuko Mkuu wa Serikali. (Outstanding Dividends payment SOE Category as of June 2023. Tuzo hizo zimekabidhiwa leo jijini Arusha na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan aliyefungua kikao kazi hicho…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Arusha . Kesi ya madai ya sh,milioni 123 inayoikabili kampuni ya Mabasi ya Kilimanjaro Track co.ltd dhidi ya Msanii wa kizaźi kipya,Nuni Suleiman(35) Mkazi wa Dar es salaam, imeunguruma katika mahakama ya wilaya Arusha. Shahidi wa kwanza katika shauri hilo la Madai namba 36 la mwaka 2022,  Nuni Suleimani,mbele ya Hakimu Mwandamizi Wilaya ya Arusha,Bitony  Mwakisu ,amedai  mahakamani hapo kuwa kampuni hiyo ya Kilimanjaro imejinufaisha kwa kutumia nyimbo yake ya Tabasamu Tanzania kujitangaza kibiashara kupitia mitandao ya kijamii bila idhini yake na kudai fidia ya kiasi hicho cha fedha. Alidai hayo wakati akiongozwa na wakili wake,Lillian…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha RAIS Samia Suluhu Hassan,Augosti 19 anatarajiwa kufungua kikao kazi cha Wenyeviti na Wakurugenzi wa mashirika ya umma na Taasisi za Serikali,utakaofanyika katika  Ukumbi wa mikutano ya kimataifa,AICC Jijini Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Arusha,John Mongela,ameyasema hayo  Augosti 18 alipokuwa akitoa taarifa ya maandalizi ya kikao hicho kwa vyombo vya habari na  kusema mbali na Rais,Viongozi wengine watakaokuwepo ni pamoja na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa,Spika wa Bunge,Dkt Tulia Acksoni na mawaziri wa wizara mbali mbali . Ameongeza kuwa Augosti 21, Rais Samia,atakuwa mgeni rasmi kwenye madhimisho ya miaka 60 ya Kanisa la Kiinjili la kiluthelu Nchini,KKKT yatakayofanyika kwenye…

Read More

Na Geofrey Stepgen Arusha . Mamlaka ya udhibiti usafiri Ardhini LATRA mkoani Arusha, imetangaza kumalizika kwa mgomo wa daladala uliodumunkwa takribani siku mbili katika jiji la Arusha  na kusababisha adha kubwa kwa wananchi, wafanyabiashara na wanafunzi. Aidha mamlaka hiyo imepiga marufuku kwa chombo cha usafiri cha Bajaj  kufanyabiashara ya kupakia abiria kama daladala badala yake imewataka kufanyabiashara hiyo kwa kukodishwa  na sio kwenda wakiokota abiria. Akiongea na vyombo vya habari afisa mfawidhi Latra mkoa wa Arusha, Joseph  Michael,  amewahakikishia wananchi kuwa  hakuna mgogoro wowote kwa sasa baina ya daladala na bajaj na tayari vituo vipya 50 vya daladala  vimepangwa kutumika…

Read More