Author: Geofrey Stephen

Na Geofrey Stephen Arusha CHUO cha Uhasibu Arusha (I.A.A),kimeeleza  mafanikio makubwa ya elimu yaliyotokana na  ongezeko la mitaala na kufanya pato la ndani kufikia sh,bilioni 26 sawa na ongezeko la sh,bilioni 15 kutoka mwaka wa fedha wa  2021/22. Mkuu wa chuo hicho Profesa Eliamani Sedoyeka,amebainisha  hayo  wakati alipokuwa akizindua  ripoti ya Chuo hicho na kuyataja mafanikio hayo kuwa ni pamoja na kujengwa Kituo kikubwa cha kisasa cha Habari na mawasiliano kwa nchi za afrika (ICT)ambacho kitaanza kufanyakazi mwakani . Alisema mafanikio hayo yametokana na ongezeko la wanafunzi kukua na kufikia 13,000 na lengo ni kufikisha wanachuo wapatao 16,000. Mafanikio mengine…

Read More

Arusha Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha  imemwamuru Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Monduli,Isack Joseph maarufu kwa jina la Kadogoo kumlipa shilingi milioni 250 Mkuu wa Mkoa Mstaafu,Loota Sanare kwa kumkashfu,kumdhalilisha na kumchafua kwa jamii kwa kumwita mwizi. Uamuzi huo ulitolewa na Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha Aisha Ndosi baada ya kusikiliza ushahidi wa pande zote na kujilidhisha pasipokuwa na shaka yoyote kuwa Joseph alitamka maneno ya kashfa dhidi ya Sanare aliyewahi kuwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro. Ndosi katika hukumu yake alisema kuwa utetezi uliotolewa na Joseph hakuwa na nguvu kwani ushahidi uliosikilizwa toka kwa mlalamikaji ulikuwa…

Read More

Na Richard Mrusha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewasihi Wafanyabiashara wa mafuta ya dizeli na Petroli nchini kuwa waaminifu wakati wakiendelea kutoa huduma kwa Watanzania. Dkt. Biteko ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na Wafanyakazi wa EWURA jijini Dar es Saalam Septemba 14, 2023 na kukukumbushia kuwa, pamoja na kuwa ni Wafanyabishara lakini pia wanatoa huduma kwa Wananchi. ‘’Naomba Wafanyabiashara wenye leseni za biashara ya mafuta nchini watambue kuwa wana wajibu wa kuhudumia watanzania ili wapate bidhaa hiyo, tunajua kuwa kiwango cha uagizaji wa mafuta kutoka nje ya nchi kimepungua lakini Serikali inaendelea kulifanyia kazi,”…

Read More

Na Geofrey Stephe,Arusha VIJANA wanaohitimu masomo yao mbalimbali kwenye vyuo wapewa mbinu za kuachana na utegemezi wa ajira za serikali, badala yake wajiunge na kozi ya ubaharia na  uhandisi zenye watalamu wachache duniani, ili kupata ujuzi utakaowasaidia kujiajiri na kuajiriwa kiurahisi. Ushauri huo umetolewa Jijini Arusha na  mmoja wa Wataalamu wa masuala ya ufuatiliaji na tathimini kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Ajira na Watu Wenye Ulamavu,James Mallya, wakati akizungumza na vyombo mbalimbali  vya habari, katika kongamano  la pili  la kitaifa, la wiki ya ufuatiliaji  na tathimini.⁷ Alisema  kwa Tanzania vijana hawana sababu ya kukosa mafunzo hayo, sababu tayari kuna Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI)…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati Dkt.Dotto Biteko  amesema Mtu asiyejifanyia Tathmini atakuwa mtu wa kuduwaa wakati wote au mtu asiyejifanyia tathmini atakuwa mtu wa kushangaa tu au kushangaza wengine…. nnachataka kusema ni kwamba serikali kama haitafanya tathmini ya shughuli zake haitapata uwezo wa kujipima imefanikiwa au imekwama wapi. Aidha haitagundua vihatarishi vya utekelezaji wa mipango yake na ndio maana mh.Rais kama mnavyomsikiliza Moja ya jambo analolizungumza kwa nguvu zote na ambalo anatupa Kazi ya kulifanya ni sisi serikali kuwa na uratibu wa shughuli zetu tunazozifanya. Ameyasema hayo wakati…

Read More

Na Ahmed Mahmoud Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Dkt.Doto Biteko ameiagiza Idara ya Ufuatiliaji na Tathmini ya Utendaji Iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu kuzifanyanyia  tathimini taasisi zote za umma na Wizara bila ya uoga wala kumhofia yeyote katika ofisi hizo kwani ni za Watanzania wote. Dkt. Dotto Biteko ametoa maelekezo hayo kwa niaba ya Waziri Mkuu jijini Arusha wakati  kongamano la wiki ya kitaifa ya Ufuatiliaji, Tathimini na Mafunzo inayofanyika kwa siku tatu katika kituo cha mikutano cha AICC jijini huo. Amesema kwamba mjue serikali inatokana na wananchi, na wakati mwingine wananchi wanatufanyia tathmini sisi kuliko…

Read More

NAIBU  Waziri wa Habari, Mawasiliano na Tenkolojia ya Habari,Mhandisi Mathew Kundo amesema Tanzania ipo mbioni  kuweka sera, zinazoendana na mabadiliko ya teknolojia katika uendelezaji wa miji maridadi Duniani. Akizungumza jana jijini Arusha,katika mkutano wa siku kumi wa  Kimataifa wa Shirika la Mawasiliano la Kimataifa la (ITU),uliokutanisha wataalamu wa teknolojia na mawasiliano kutoka ndani na nje ya nchi,Mhandisi Kundo alisema, uchumi wa kidigitali ndio utakaowezesha kuendanana na miji ya kisasa duniani. Alisema sera hizo zitawezesha nchi ya Tanzania kujipanga zaidi na kuweka sera zinazoendana na mabadiliko ya teknolojia hiyo, kwani Dunia kwa  sasa, inakwenda kwenye uchumi wa dijitali wa kupata huduma…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv ,Arusha . Tume ya Nguvu za Atomu Tanzania (TAEC) Kanda ya kaskazini kudhibiti matumizi salama ya vyanzo vya mionzi vinavyo patikana katika mboga za majani ambazo hulimwa katika sehemu zenye madini ya urani ambayo humpelekea mtumiaji kupata madhara  kwa upimaji udongo huku ikitajwa kuwa madhara hayotokani na viuatilifu wanavyo tumia kulimia mazao. Wakizungumza katika ziara ya kamati ya kudumu ya bunge ya bajeti ilipotembelea ofisi za tume ya nguvu za atomu Tanzania [TAEC] Kanda ya kaskazini Peter Pantaleo  ambaye ni mtaalamu wa mazingira . Amesema kwenye mazingira ya kawaida kuna mionzi ambayo inatokana na madini ya…

Read More