Na Richard Mrusha Katibu Mkuu Wizara ya Madini, Kheri Mahimbali amekutana na kuzungumza na Ujumbe kutoka Ubalozi wa Marekani nchini katika ziara iliyolenga kuzungumzia masuala mbalimbali katika shughuli za uchimbaji na maendeleo ya Sekta ya Madini, Mji wa Serikali jijini Dodoma. Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika leo Septemba 7, 2023, Katibu Mkuu Mahimbali amesisitiza kuimarisha ushirikiano katika uchimbaji wa madini hususan ya kimkakati, kujengewa uwezo wataalam mbalimbali wa Sekta ya Madini ili mnyororo mzima wa shughuli za madini unufaike. Amesema kuwa Wizara ya Madini imeweka vipaumbele katika maeneo manne ili kuimarisha zaidi Sekta hiyo, maeneo hayo ni pamoja na Utafiti…
Author: Geofrey Stephen
Na Richard Mrusha Imeelezwa kuwa Madini ya Vito aina ya Spinel yanayochimbwa Mahenge Tanzania ni miongoni mwa bidhaa inayotafutwa kwa kiasi kikubwa na Wanunuzi na Wauzaji Wakubwa wa Madini ya Vito na Usonara wanaoshiriki na kutembelea katika Maonesho ya 68 ya Vito na Usonara yanayoendelea katika jiji la Bangkok eneo la Queen Sirikit nchini Thailand. Hayo yamebainishwa Septemba 9, 2023 na Mkurugenzi wa Kampuni ya Ruby International Limited Mhe. Salim Hasham ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Ulanga, Mahenge Mkoa wa Morogoro ambaye kampuni yake inashiriki katika maonesho hayo. Kampuni hiyo inajishughulisha na uuzaji, uchimbaji na ununuzi wa madini…
Na mwandishi wetu Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka, amesema kuwa watanzania wanahitaji kupata huduma ya umeme wa uhakika na kwamba ameridhishwa na kazi kubwa ya utekelezaji wa mradi wa kuzalisha umeme wa Julius Nyerere (JNHPP). Balozi Kusiluka ameeleza hayo tarehe 6 Septemba, 2023 wakati wa ziara ya kutembelea mradi wa JNHPP ili kuona maendeleo ya Mradi huo unaotarajiwa kuzalisha Megawati 2115 za Umeme ambao unatekelezwa katika Mkoa wa Pwani. Amewasisitiza wataalamu wanaotekeleza mradi huo kuwa wahakikishe kuwa mradi huo unakamilika kwa wakati kwani watanzania wanausubiri kwa hamu kubwa na wanataka kunufaika na uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali yao.…
Na Doreen Aloyce, Dodoma Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa Jukwaa la Majaji Wakuu wa Nchi Wanachama kutoka Kusini na Mashariki mwa Afrika utakaofanyika Jijini Arusha kuanzia Oktoba 23 hadi 27 mwaka 2023. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi wakati akiongoza kikao cha maandalizi ya mkutano huo kilichohudhuriwa na Makatibu Wakuu ili kuwa na uelewa wa pamoja kuhusu masuala muhimu yatakayojadiliwa. Dkt. Yonazi amesema mgeni rasmi katika mkutano huo anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa, Dkt. Samia Suluhu Hassan akisema Nchi wanachama wa…
Karibu Arusha24Tv leo September 7 kutazama habari kubwa zilizo Andikwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania mbele na nyuma Hii ni A24Tv .
Na Mwandishi wetu Dodoma Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amefungua mkutano wa mwaka wa kiutendaji wa Maafisa Ustawi wa Jamii kutoka Wizara za Kisekta, Taasisi za umma pamoja na sekta binafsi zinazotoa huduma za Ustawi wa Jamii nchini na kutoa maelekezo mahsusi yatakayofanya sekta hiyo kuwa imara na kutoa huduma bora katika Taifa. Dkt.Doto Biteko amefungua Mkutano huo tarehe 6 Septemba, 2023 jijini Dodoma ambapo mkutano huo ulihudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima, Naibu Waziri, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala…
Na Mwandishi wa A24Tv Dodoma Serikali imesema inaendelea na jitihada za kudhibiti mimea vamizi katika maeneo ya Hifadhi na Mapori ya Akiba kwa lengo la kurejesha uoto wa asili nchini ambao ni tegemeo kwa wanyamapori. Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula wakati akijibu swali la Mbunge wa Donge, Mhe.Mohamed Jumah Soud aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kupunguza upoteaji wa uoto wa asili nchini unaosababisha kupoteza hadhi kwa Hifadhi na Mapori ya Akiba. Mhe. Kitandula ametaja sababu kubwa ya kupotea kwa uoto wa asili katika Hifadhi na Mapori ya Akiba kuwa ni ongezeko…
Juma Tano ya September 6 tunakukaribisha Arhsha24Tv kutazama habari kubwa katika Magazeti ya leo ya Tanzania kilicho andikwa mbele na nyuma ya magazeti Hii ni A24tv Mwisho .
Na Mwanfishi wa A24tv . Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii inaendelea kutekeleza mikakati mbalimbali inayolenga kuendeleza, kukuza na kutangaza vivutio vya utalii nchini ikiwemo vivutio vilivyopo Kisiwa cha Ukerewe kama Mapango ya Handebezya na Jiwe linalocheza. Hayo yamesemwa leo na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb) alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Ukerewe Mhe. Joseph Mkundi aliyetaka kujua mkakati wa Serikali kuvifanya vivutio vya Mapango ya Handebezya na Jiwe linalocheza kuwa na tija kwa Taifa. Amefafanua kuwa moja ya mikakati hiyo ni pamoja na kutangaza vivutio hivyo kwa kutumia vyombo mbalimbali vya habari. “Wizara…
Jumanne ya leo September 5 Hii ni Arusha24Tv karibu kutazama gavari kubwa katika magazeti ya leo ya Tanzania kilicho andikwa mbele na nyuma Hii ni A24Tv . Mwisho .