Na Bahati Hai
Mwenyekiti wa chama cha mpira wa miguu Wilayani Siha mkoani Kilimanjaro Hassani Karata,amekemea maswala ya siasa kutokuingizwa kwenye michezo.
Haya amesema katika uwanja wa michezo wa Matadi kilimahewa Kata ya Indumet wakati wa uzinduzi wa West Champions Ligi ,
Amesema Swala la siasa ndani halitakiwi kwenye michezo ,kanuni ya mpira wa miguu haufungamani na chama cha siasa,Dini au Serikali kabisa
Kwa maana mpira ni furaha ,ajira na Amani,lakini mpira unapoingia na siasa tayari mpira unaharibika
Erick Joshua ,katibu wa bodi ya wadhamini West Champions Ligi ,amesema ligi hiyo inaendelea vizuri,Ambapo amesema timu 16 zinashiriki mashindano hayo mbili kati ya hizo zinatoka wilaya ya Hai mkoani hapa.
Bantazar Mmar kwa niaba ya Antony Mallya ambaye ndiyo mdhamini wa mashindano hayo,amesema ameshukuru Wananchi kujitokeza kwa wingi kuja kuangalia mashindano hayo
Kwamba michezo unafanya mambo mengine,watu wanajumuhishwa kuwa wamoja ,kufahamiana ,Afya ,Ajira na kujenga Taifa lenye nguvu na imara na mambo mengine mengi
Mwisho