NaGeofrey Stephen , Arusha
Serikali itaendelea kuimarisha huduma za utalii ikiwemo kutatua changamoto wanazokutana nazo wakala wa usafirishaji watalii Mkoa wa Arusha ili waweze kukua zaidi na kutoa huduma hizo ndani na nje ya Nchi.
Aidha serikali itaendelea kuhuisha huduma za pamoja za utalii kwa Nchi za Afrika Mashariki(EAC) pamoja Nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).
Hayo yalisemwa jana Jijini Arusha na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Misaile Mussa Wakati akizungumza na katika mkutano wa majadiliano kati ya Mawakala wa Usafirishaji Watalii Mkoa wa Arusha na Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri Ardhini(LATRA)
Alisema mawakala hao ni watu muhimu katika sekta ya usafirishaji kwani hutoa huduma za utalii kwa kusafirisha watalii na kwenda kutangaza vivutio vingine vya utalii kupitia usafiri wa magari
Alisema idadi ya wasafirishaji wa utalii waliopo hadi sasa katika Mkoa wa Arusha ni zaidi ya 10,72 hivyo sekta hiyo ni muhimu kwani miongoni mwao kunawatoa huduma za utalii kwa wadogo ,wakati na wakubwa.
“Serikali imechukua changamoto zenu na itafanyia kazi lengo ni kuhakikisha sekta ya utalii inakua zaidi”
Alieleza licha ya mkoa kuwa kitovu cha utalii serikali inakusudia kufikisha watalii zaidi ya milioni 5 kufikia mwaka 2025 .
Naye Mkurugenzi Udhibiti Usafiri wa Barabara kutoka (LATRA),Johansen Kahatao alisema mamlaka hiyo imekutana na wadau hao ili kujua changamoto wanazokutana nazo
“Latra imebeba changamoto za wadau wa utalii na itazifanyia kazi”
Kwa upande wao wadau wa utalii,kutoka taasisi na kampuni mbalimbali walisema uwepo wa utitiri wa tozo nyingi husababisha watalii kukatisha safari zao kuja nchini.
Ambapo mdau wa Utalii,Isabela Munisi Kashasha aliomba wadau wa usafirishaji kuingia mkataba na kampuni za ndege ili kutangaza vivutio vya utalii mikoa ya Kusini kwani usafiri wa magari ni mrefu na changamoto kubwa ni miundombinu ya barabara lakini usafiri wa ndege ukaanza kwa mikoa ya kusini itasaidia kupunguza gharama za watoa huduma za utalii.
Mwisho.