Author: Geofrey Stephen

Na Richard Mrusha Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imeweka wazi mikakati mbalimbali ya kuongeza watalii katika Hifadhi ya Taifa Ruaha ikiwa ni pamoja kuanzisha na kuboresha miundombinu ya barabara za ndani ya Hifadhi kwa kiwango cha changarawe na kuboresha barabara kuu kutoka Iringa Mjini mpaka hifadhini. Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) ameyasema hayo Bungeni Jijini Dodoma leo Mei 26,2023 kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Grace Tendega aliyetaka kujua idadi ya Watalii waliotembelea Hifadhi ya Taifa Ruaha kwa mwaka 2019/2020 na mikakati…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Matukio ya kushamiri kwa wivu wa mapenzi mkoani Arusha yaanza kutikisa tena mara baada ya Mwanamke Mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Jackline Mnkonyi{38} mkazi wa Sombetini Jijini Arusha mei 23 mwaka huu majira ya saa 5 usiku alipata kipigo kikali kutoka kwa mume wake ikiwa ni pamoja na kung’olewa meno mawili na kutobolewa jicho kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi. Akizungumza  na waandishi wa habari nyumbani kwa wazazi wake eneo la Sinoni kata ya Daraja Mbili Jijini Arusha,Jackline alisema kuwa baada ya kupata kipigo hicho alichukuliwa bila kujitambuwa na kupelekwa nyumbani kwa wazazi…

Read More

Na Geofrey Syephen , Ngorongoro Madiwani wa Baraza la Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro Mkoa wa Arusha,wameikataa rasimu ya mpango wa matumizi ya Ardhi ya wilaya hiyo, wakidai si shirikishi na inalenga kumega ardhi yao ya malisho na  kuliingiza kwenye hifadhi kitendo ambacho kitaathiri ustawi wa wananchi . Madiwani hao walitoa kauli hiyo katika baraza hilo la madiwani baada ya kuwasilishwa kwa ajenda namba nne katika kikao hicho iliyolenga kujadili na kupitisha mpango wa matumizi ya Ardhi wa miaka 20 kuanzia mwaka huu 2023 hadi 2043. Diwani wa kata ya Nainokanoka,Edward Maula alisema hawakubaliani na rasimu hiyo kwa kuwa imelenga…

Read More

Na Richard Mrusha Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema imekuwa ikiendelea kuchukua hatua mbalimbali za kutatua migogoro baina ya maeneo ya Hifadhi na Wananchi huku ikisisitiza kuwa itaendelea kuchukua hatua kali za kisheria kwa wale wote wanaovamia maeneo ya Hifadhi. Hayo yamesemwa leo Mei 25 2023 na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe.Mary Masanja kwa niaba ya Waziri wa Maliasili na Utalii alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Momba, Mhe.Condester Sichalwe aliyetaka kujua mpango wa Serikali wa kutatua migogoro kati ya wananchi na maeneo ya Hifadhi za Taifa. Amefafanua kuwa moja ya hatua zinazochukuliwa na Serikali kutatua…

Read More

Na Doreen Aloyce,Dodoma SERIKALI imekutana na wadau wa kuzalisha mafuta ya kupikia kwa ajili ya kujadili changamoto zinazosababisha kushuka kwa bei ya mafuta na alizeti nchini. Kikao hicho kilicho kimefanyika leo tarehe  23 Mei, 2023 kilichowakutanisha mawaziri watatu kutoka wizara tatu ,waziri wa Uwekezaji, Viwanda , Biashara Mhe. Dkt Ashatu Kijaji , Waziri wa Kilimo Husssein Bashe na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt.Mwigulu Nchemba. Akifungua kikao   hicho Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) amesema lengo la kikao hicho ni kuongea kwa pamoja , kuboresha maisha kuchangia uchumi wa Taifa na hatimaye kuzalisha mafuta ambayo…

Read More

Na Geofrey Steohen .ARUSHA Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi amesema kuwa elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi ni muhimu sana katika kuandaa nguvukazi yenye ujuzi unaohitajika katika kuendeleza uchumi wa taifa. Amebainisha hayo wakati akifunga maonesho ya pili ya elimu ya ufundi na mafunzo ya ufundi stadi (TVET) katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jijini Arusha. Naibu Waziri Katambi ameeleza kuwa elimu hiyo itasaidia kuwajenga vijana kuwa na uwezo na ujuzi wa kufanya kazi mbalimbali za kiufundi, kuunda bidhaa na hata kuwa wajasariamali wakubwa. “Baraza la Taifa…

Read More

Na Mwandishi wetu. Sakata la mgogoro wa Mgodi wa Gem & Rock Venture uliopo Kitalu B katika Madini ya Tanzanite Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara limeingia sura Mpya baada ya Kamishina wa Madini Nchini,Dkt Ibraharman Mwanga kusema kuwa rufaa ya kupinga kufungiwa kwa Mgodi huo amemtumia Mkurugenzi wa Mgodi  huo Joel Mollel maarufu kwa jina la Saitoti  wakati Saitoti anasema hana taarifa yoyote juu ya Maamuzi ya rufaa yake. Mnamo Machi 13 mwaka huu wachimbaji wa Mgodi wa Gem & Rock Venture Uliopo Kitalu B Wakiongozwa na Saitoti walivamia mgodi wa kitalu C zaidi ya mita 650 kinyume na utaratibu…

Read More