Author: Geofrey Stephen

Na Mwandishi wa A24Tv . Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) amewakaribisha wawekezaji wenye nia kutoka India kuja kuwekeza nchini katika sekta mbalimbali hususani viwanda vya kutengeneza dawa na vifaa tiba, uchumi wa bluu na viwanda vya kuongeza thamani mazao ya kilimo kama Parachichi na Mbaazi zinazohitajika kwa wingi katika soko la India. Dkt. Kijaji ameyasema hayo alipokutana na kufanya mazungumzo kuhusu kuendeleza uhusiano wa kibiashara na uwekezaji baina ya Tanzania na India na Balozi wa India nchini Mhe. Binaya Srikanta Pradhan Machi 27, 2023 katika Ofisi ndogo ya Wizara, jijini Dar es Salaam. Katika…

Read More

Na. Salim Bitchuka Imeelezwa kuwa muamko mdogo wa vijana katika fani ya ubaharia ndio chanzo kinachopelekea taifa la Tanzania kutokuwa na Mabaharia Vijana wa kutosha. Hayo yamebainishwa hivi karibuni jijini Dar es Salaam na mkurugenzi wa huduma za Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Rajabu Mabamba wakati wa hitimisho la mafunzo kwa walimu wa Mabaharia nchini Akimuwakilisha mkurugenzi wa TASAC, Mabamba alisema muamko umekuwa ni mdogo kwa vijana kutokana na kukosa kutengenezewa ufahamu wa kutosha kuhusu fursa zipatikanazo katika eneo hilo. “Kwa kutambua kuwa nchi kama nchi wakati tukielekea uchumi wa Buluu kwa kushikiana na DMO tuligundua kwamba kulikuwa…

Read More

Na Pamela Mollel Arusha . Diwani wa Kata ya Baray Wilayani Karatu. Mhe Elitumain Magnus leo tarehe 25 March amechuku na kurejesha fomu ya kuwania nafasi ya Mjumbe wa NEC Mkoa wa Arusha. Elitumaini ni mtaalamu katika maswala ya uongozi na mahusiano ya jamii akiwa na shahada ya juu kutoka chuo kikuu cha Mzumbe. Kiongozi huyo ambaye kwa Sasa ni Diwani wa kata ya Baray Wilayani Karatu, amewahi pia kushika nyadhifa mbali mbali katika chama cha Mapinduzi Ikiwa ni pamoja na Mjumbe wa Kamati ya utekelezaji jumuiya ya vijana Wilaya ya Karatu na mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM mkoa…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha . Thomas Munisi akiwa katika Mavazi ya chama kikamanda zaidi  Kada wa chama chamapindhzi Ccm Thomas Munis maarufu kwa jina la Brigedia munisi achukua na kurejesha form ya kugombea nafasi ya halmashauri kuu ya Ccm Taifa (Nec) Munisi kwa sasa ni Mwenyekitii wa Ccm kata ya themi na ni Mjumbe wa halmashauri kuu ya Ccm wilaya ya Arusha ni mjumbe wa mkutano Mkuu Ccm Mkoa wa Arusha amekuwa Makamu mwenyekiti Taifa wa wafanyabiashara wa madini tanzania na ni mchimbaji na Mfanyabiashara maarufu wa madini na utali tanzania bara na Zanzibar. Munisi licha ya kujaza fomu yake…

Read More

Na Geofrey Stepben Mfanyabiashara Maarufu Jijini Arusha,Richard Poul maarufu kwa jina la Marcas amajitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi Moja ya Mjumbe wa Halmashauri Kuu{NEC} Mkoa wa Arusha akisema kuwa lengo lake kuu ni kuwaunganisha wanachama wa Chama Cha Mapinduzi{CCM} kuwa kitu kimoja na ili kiweze kuendelea kushika dola. Marca alisema na kuwataka wajumbe wa Uchaguzi kuangalia sifa za mgombea na kuacha mara moja kuchagua mgombea kwa rushwa kwani rushwa kwake ni adui wa haki na kamwe hawezi kufanya hivyo kwani anajiamini kuwa anatosha. Alisema na kusisitiza kuwa uchaguzi huo wa marudio uligubikwa na rushwa na ndio maana viongozi wa…

Read More

Na Mwandishi wa A24Tv .Arusha Ni katika Muendelezo wa Ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Monduli Ndugu Kisioki Lengoje Moitiko Katika kata ya Moita ambayo Jumla ya vikundi vilivyopo katika kata hiyo ni 47. Akizungumza na Wanachama wa CCM na jumuiya zake ,ndugu Kisioki amesema lengo la ziara ni kushukuru baada ya kuchaguliwa na ni muendelezo wa ziara yake ambapo lengo kubwa ni kuwafikia wanachama wote , lakini pia kuwazesha Vikundi vya wanawake (vikundi,Vkoba) kiuchumi. “Niwashukuru sana wanamoita kwani kati ya kata nilizotembelea yenye wanachama hai Moita ni Miongoni, lakini pia kina mama nawashukuru sana vikundi viko vingi sijui…

Read More