Author: Geofrey Stephen

Sheikh Shafi Muhammad Memon wa Mikoa wa Arusha, Kilimanjaro na Manyara. Jumuiya ya Waislamu Wa Ahmadiyya Ameshauri wananchi kwa ujumla  kwamba katika mazingira yoyote na hali yoyote, daima Kauli hiyo ametoa wakati wa kufunga maonyesho ya wakulima nane nane yaliofanyika katika viwanja vya taso njiro Jijini Arusha  jitahidini kuwakilisha picha halisi ya Islam katika kila mwenendo na tabia yenu. Muwe na mwenendo sahihi na mjaribu kuonyesha mfano wa tabia bora kabisa kama wananchi katika nchi mnamoishi. Daima muwe watii kwa taifa lenu na msipingane na serikali yenu kwa namna ambayo itakuwa ni kinyume na sheria za nchi. Muwe watii kamili…

Read More

Na Geofrey Stephen .ARUSHA Mfanyabiashara maarufu wa Madini jijini Arusha,Thomas Munisi amefanikiwa kutetea nafasi yake ya mwenyekiti wa ccm kata ya Them baada ya kushinda kwa kishindo akiwa safarini . Katika nafasi hiyo iliyokuwa na ushindani mkali ndani ya chama hicho, Munisi alishinda kwa asilimia 99 na kuwagaragaza wagombea wenzake wawili waliomfuatia kwa mbali. Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo,msimamizi wa uchaguzi,Kibuzo Senga alimtangaza Munisi kuwa mshindi wa nafasi hiyo na kuwashinda wagombea wengine ambao ni Feruz Ramadhani aliyepata kura 2 na Erick Mhalila aliyepata kura 2. Senga alisema kuwa uchaguzi huo ni mwendelezo wa chaguzi za ndani za ccm ngazi…

Read More

mwandishi wetu,Rombo Rombo, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mhandisi Clement Kivegalo, amemuagiza Mkandarasi Kampuni ya Best One Ltd, inayotekeleza miradi miwili ya miwili ya wilaya ya Rombo itakayogharimu jumla ya Sh. 5.3 bilioni kuikamilisha kwa wakati ili shida ya maji Rombo imalizike. Akizungumza baada ya kukagua utekelezaji wa miradi hiyo, Mhandisi Kivegalo alisema Miradi hiyo, ambayo inatekelezwa kwa pamoja baina RUWASA na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Rombo ni lazima ikamilike kwa wakati ili wananchi wa Rombo wapate huduma muhimu ya maji. “nimekuja Rombo na wataalam wangu kuona utekelezaji wa miradi…

Read More

Halmashauri ya jiji la Arusha imeanza kutekeleza kwa kishindo agizo la waziri mkuu Kasimu Majaliwa,la kuweka umeme katika soko namba 68 la Wamachinga, Kilombero Sanjari na kuongeza idadi ya malango ya kuingilia ndani ya soko hilo. Waziri mkuu Majaliwa alitoa maelekezo mwezi Julai mwaka huu alipofanya ziara ya kutembelea soko hilo ambapo aliagiza uongozi wa halmashauri ya jiji la Arusha kuweka umeme pamoja na kuongeza idadi ya malango ya kuingilia katika soko hilo kama njia mojawapo ya kuliboresha na kurahisisha shughuli za wafanyabiashara hao jambo ambalo limetekelezwa. Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Arusha,Hargeney Chitukulo  amefanya ziara ya kutembelea…

Read More

Na Geofrey Stephen Arusha Taasisi ya uhandisi na usanifu mitambo nchini (TEMDO) imebuni mtambo mpya wa kisasa wa kuchakata mafuta ya alizeti ambayo yatasafishwa katika ubora kwa kiwango cha juu kwa  ajili ya matumizi ya binadamu. Taasisi hiyo imeutambulisha mtambo huo kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya sikukuu za wakulima nchini (Nane Nane) yanayoendelea katika viwanja vya Nanenane eneo la Njiro jijini Arusha. Akizungumza na waandishi wa habari mkuu wa kitengo cha mawasiliano na masoko katika taasisi hiyo,dkt Sigisbert Mmasi alisema kwamba mtambo huo mbali na kuchakata mafuta ya alizeti lakini utayasafisha mafuta hayo na kisha kutawekea virutubisho. Alisema…

Read More